Tafuta

Vatican News
Ufaransa; harakati za kupinga nyanyaso za kijinsia na kudai heshima kwa akina mama na mabinti. Ufaransa; harakati za kupinga nyanyaso za kijinsia na kudai heshima kwa akina mama na mabinti.  

Monsinyo Wachowski; Atoa Tamko la kupinga nyanyaso za kijinsia!

Monsinyo Miroslow Wachowski, amewataka wanachama wa Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo OSCE kufanya kampeni ya kutokomeza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia katika mifumo ya kiteknolojia dhidi ya wasichana na akina mama. Pia kupambana na utamaduni wa ngono kwa mabinti na akina mama na kujenga heshima ya mwanamke katika jamii.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican

Monsinyo Miroslaw S Wachowski, mwakilishi rasmi wa Vatican katika Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo, OSCE katika mkutano uliofanyika kati ya tarehe 19 na 20 Septemba, 2019 huko Warsaw Poland unaohusu kuchukuliana na siyo kubaguana, haki sawa kwa wanawake na wanaume, utekelezaji wa mpango mkakati wa OSCE kwa ajili ya haki sawa kwa wote, na unyanyasaji kwa wanawake. Akieleza mada hiyo Monsinyo Miroslaw S Wachowski amesema, jitihada zinazochukuliwa na Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo OSCE katika kutekeleza mikakati iliyojiwekea ya mwaka 2018 dhidi ya unyanyasaji wa wanawake zinaonekana. Hata hivyo nchi wanachama wanapaswa kuendelea kujengeana uelewa katika kampeni ya kutokomeza vitendo vya kiunyama vinavyotendeka katika mifumo ya kiteknolojia dhidi ya wasichana na akina mama.    Aidha maamuzi yaliyochukuliwa na Vatican ni pamoja na kupambana na utamaduni wa ngono ambao umeanza kuzoeleka katika jamii ya mitandao, sehemu zenye burudani na katika makundi jamii. Utamaduni huo unawazalilisha mabinti na akina mama na ni lazima kushirikiana katika kuupinga.

Sababau kuu za kuupinga zikiwa ni utamaduni unoshusha heshima ya mwanamke na kuwa chombo cha ngono, wanawake wanapaswa kutokubaliana na mtamo huo. Pia mifumo ya kandamizi inayowafanya mabinti na akina mama wateseke katika jamii kwa sababu tu ya jinsia yao, kama vile tatizo la utoaji mimba linavyomwandama mwanamke bila hata ya kuhoji ushiriki wa wanaume. Utekelezaji wa maazimio ni mbinu sahihi ya kufikia malengo wanayojiwekea na hasa katika kuwatetea wanawake wanaoishi katika mazingira yenye migogoro mikubwa ya kifamilia. Mwanamke anapaswa pia kuamka na kujitetea katika Nyanja za kisiasa na kiuchumi. Aidha, Vatican inaliomba Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo, OSCE kusimamia malengo yake madhubuti linayojiwekea, kuhakikisha haki sawa inapatika katika familia na kukomesha vitendo vya nyanyaso za kijinsia. Pia Vatican inaiomba OSCE kutumia lugha inayokubalika kwa wote.  

03 October 2019, 15:37