Tafuta

Vatican News
Maisha ya ibada katika familia ni kati ya haki msingi za binadamu: Familia ya kihindu wakiwa katika ibada ya sala. Maisha ya ibada katika familia ni kati ya haki msingi za binadamu: Familia ya kihindu wakiwa katika ibada ya sala.   (©WONG SZE FEI - stock.adobe.com)

Askofu Mkuu Ghallagher; OSCE "Heshimuni uhuru wa kuabudu!"

Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher amesema, uhuru wa kuabudu, uhuru wa kifikra, uhuru wa ki-dhamiri ni taswira ya uhuru wa kweli katika jamii. Kila mtu ana uhuru wa kuisikiliza dhamiri yake inayomwelekeza katika ibada kuimarisha mahusiano bora na Mwenyezi Mungu. Uamzi huo unapaswa kuheshimiwa katika jamii, na OSCE kuzingatia uhuru wa kuabudu kama haki za binadamu.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican

Askofu mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican katika mahusiano ya kimataifa, amelitaka Shirikisho la ushirikiano wa Kimataifa, Usalama na Maendeleo, OSCE kuzingatia uhuru wa kuabudu kama moja ya haki za binadamu. Ameyasema hayo katika mkutano wa 22 wa OSCE uliofanyika mnamo tarehe 19 Septemba 2019 huko Warsaw nchini Poland.  Akieleza mada hiyo Askofu mkuu Paul Richard Gallagher amesema, uhuru wa kuabudu, uhuru wa kifikra, uhuru wa ki-dhamiri ni taswira ya uhuru wa kweli katika jamii. Kila mtu ana uhuru kuisikiliza dhamiri yake inayomwelekeza katika ibada kuimarisha mahusiano bora na Mwenyezi Mungu. Uamzi huo unapaswa kuheshimiwa katika jamii. Askofu mkuu Paul Richard Gallagher amesema, katika mazingira ambayo kuna utawala wa mabavu uhuru huo unawekewa vipingamizi vingi katika kuweka vigezo vinavyoongoza jumuiya za kidini. Vizingiti hivyo hudhofisha mahusiano ya kijamii na hivyo kunahitajika kuwepo tena ulinzi dhidi ya haki ya kuabudu ambayo ilikuwepo katika historia ya OSCE na ilikuwa miongoni mwa vipengere vya haki za binadamu vilivyolifanya Shirikisho la ushirikiano wa kimataifa, usalama na maendeleo kutofautishwa na vitengo vingine vya kimataifa.

Haki hiyo ya kuabudu ni haki msingi katika kuboresha na kulinda mafao ya kijamii. Mwandamu anapaswa kuwa huru kuabudu, kufundisha imani yake bila bugudha yeyote. Askofu mkuu Paul Richard Gallagher amesema, OSCE kama chombo cha kimataifa katika usalama na maendeleo ya kinapaswa kutoa miongozo na kuzitambua kisheria jumuiya za kidini zilizosajiliwa na kuhamasisha heshima na nafasi yake katika jamii.   Aidha Asko mku akitoaa angalisho kwa Shirikisho hilo la kimataifa amesema, kushindwa kutoa uhuru wa kuabudu, uhuru wa kifikra na uhuru wa ki-dhamiri ni  kunajenga hisia za mashaka juu ya uongozi unaoweka mipaka inayomfunga mtu binafsi na kuharibu undani wake na kumfanya ajibu hisia yake katika kuvunja maadili na sharia za nchi. Askofu Mkuu Gallagher ameendelea amesema, nchi ambazo zimetoa uhuru wa kuabudu katika misingi sharia zimepiga hatua kubwa katika katika majadiliano, maendeleo na ulinzi wa mafao ya pamoja. Askofu mkuu Paul Richard Gallagher ameendelea kusema, ili kuipata thamani ya kiraia kila mtu anahitaji kupokea asili ya mwingiliano wa kidini ndani ya jamii unaotambua na kuheshimu uhuru wa kila jumuiya. Kwa hiyo kila mmoja anawajibika kushiriki katika ulinzi wa haki za binadamu na ujenzi utamaduni fungamano.     

  

03 October 2019, 14:02