Tafuta

Vatican News
Wanawake Tanzania wanahimizwa kujihusisha katika siasa katika uchaguzi ujao, kwa maana wanao uwezo hata katika masuala ya kukuza uchumi kitaifa Wanawake Tanzania wanahimizwa kujihusisha katika siasa katika uchaguzi ujao, kwa maana wanao uwezo hata katika masuala ya kukuza uchumi kitaifa 

Tanzania:wanawake wanahimizwa kushiriki sera za kisiasa katika matarajio ya uchaguzi mdogo na 2020!

Wanawake nchini Tanzania wanahamasishwa kujikita katika sera za kisiasa kwa kuwania nafasi za uongozi,kwa maana wanayo fursa katika kukuza hata uchumi wa nchi.Ni mwaliko kutoka kwa Baraza la Maaskofu Katoliki chini Tanzania kwenye ya semina ya viongozi wa kidini kati ya Wakatoliki,makanisa ya kikristo na Bakwata hivi karibuni katika matazamio ya uchaguzi mdogo wa Novemba 2019 na uchaguzi mkuu 2020.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katiba ya Jamhuri ya Munguno wa Tanzania inathibitisha kuwa viongozi na udhibiti wa watu na wanawake wote, wanayo haki ya kishiriki katika kukuza uchumi wa nchi. Hii ina maana yake katika rasimu ya katiba inayotarajiwa, amesema Padre Charles Kitima, ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), katika Semina iliyoandaliwa kwa siku tatu hivi karibuni na Baraza la Maaskofu Katoliki, Baraza la Wakristo Tanzania (CCT) na Baraza la Kiislam (Bakwata),semina iliyowaona washiriki 100 wanawake kutoka pande zote za nchi.

Semina hii imefika wakati Tanzania inajiandaa kufanya uchaguzi mdogo wa viongozi  wa ngazi za chini kunako Novemba 2019 na uchaguzi Mkuu wa 2020, ambapo katika semina hiyo wamesistizia juu ya ushiriki wa wanawake katika sera za kisiasa. Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa zilizowafikia shirika la Habari za Kimisionari Fides, ni kwamba, Wanawake wanajihusisha katika sehemu kubwa ya sekta ya uchumi wa kawaida na wanapaswa kushika zaidi ngazi ya serikali na hatimaye kuweza kukuza maendeleo ya uchumi wa Jumuiya. Ni wakati sasa ambapo wanawake wanaweza kuongoza taifa, amesisitiza Padre Kitima.

Kama viongozi wa dini anasema Padre Kitima, wanatakiwa wabadilishe fikra za kijamii zisemazo kwamba, wanawake ni wadhaifu. Na badala yake wanawake ni watu wenye nguvu na uwezo wa uongozi. Kutokana na hilo ni matumanini ya Padre Kitima kwamba kunawezekana kabisa uwepo wa wanawake katika Bunge ambalo lina nafasi mbalimbali katika taasisi  na kwa ajili ya maendeleo ya nchi yao. "Ni wakati sasa wa kuonyesha umuhimu wa wanawake katika siasa, kufanya mchakato wa maamuzi na uongozi wa mataifa", amesisitiza Padre  Kitima  na kuongeza kuwa, "hata viongozi wa dini katika nchi na kati yao wakristo na waislam, wanao uwajibu wa kukuza nafasi  ya wanawake wenye uwezo na ujasiri.

Naye Mchungaji Benjamin Maila wa (CCT)  katika semina hiyo amethibitisha kuwa, iwapo wanawake watachaguliwa, ni shukrani yao kwa sababu ya mfungamano  wao ambao unaweza kuleta mabadiliko kiuchumi. Aidha naye rais wa shirikisho la kitaifa la wanawake waislam ameshauri wanawake wote achangamkie fursa bila kurudi nyuma, huku akiwa na matarajio kwamba wanawake walio vijana wanaweza kweli kujikita kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya uchumi na utamaduni wa kitaifa!

Kwa niaba ya serikali, naye mjumbe wa sekretarieti ya uchaguzi ya Ofisi ya Rais ametoa pongezi kwa viongozi wa dini katika kuandaa semina hiyo, huku akiwahimiza wanawake kusimama kidete kama wagombea katika uchaguzi ujao. Pia amesema kuwa, serikali inatarajia kuendesha uchaguzi huru na wa wenye haki.

09 September 2019, 15:58