Tafuta

Kanisa ni kitovu cha kijamii na ndiyo pia kiini cha mafunzo ya mtu.Maisha kwa mujibu wa maandiko matakatifu yanatakiwa kuyatunza na kuyalinda daima Kanisa ni kitovu cha kijamii na ndiyo pia kiini cha mafunzo ya mtu.Maisha kwa mujibu wa maandiko matakatifu yanatakiwa kuyatunza na kuyalinda daima 

Bara la Afrika linahitaji kuanzisha mchakato wa huduma shufaa!

Askofu mkuu Vincenzo Paglia,Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II,akiwa nchini Rwanda amezungumzia juu ya familia katika mkutano na mapadre,waamini walei na wahuduma wa kichungaji wa Jimbo Kuu Katoliki la Kigali.Kanisa ni kitovu cha kijamii na ndiyo kiini pia cha mafunzo ya mtu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Familia na ulinzi wa maisha ndiyo mada ambayo Askofu mkuu Vincenzo Paglia, Rais wa Taasisi ya Kipapa kwa ajili ya maisha na Mkuu wa Taasisi ya Kipapa ya Ndoa na Familia ya Yohane Paulo II, akiwa nchini Rwanda ameweza kuzungumzia katika mkutano na mapadre, waamini walei na wahudumu wa kichungaji wa Jimbo Kuu Katoliki la Kigali. Katika hotuba yake amesisitiza ni jinsi gani, changamoto za muungano wa familia zinafanana katika ulimwengu mzima. Pamoja na kuwa na nguvu za utamaduni mahalia barani Afrika, familia sasa inaishi kwa tishio la utengano wa umoja huo wa familia, msongo wa kiuchumi na kijamii, ongezeko na kupungua  kwa watoto na  upoteza nguvu ya maono ya Kanisa. Pamoja na hayo yote, Askofu Mkuul  anabainisha kwamba, Kanisa ni kitovu cha kijamii na ndiyo pia kiini cha mafunzo ya mtu.

 Askofu Mkuu Paglia aidha kutokana na hiyo amebainisha kwamba maisha kwa mujibu wa maandiko matakatifu ni kuhusu kutunza na kulinda daima katika utamaduni wa Kanisa na si kwamba maisha yapo kwa maana ya hali halisi, ambayo siyo ukweli wa kawaida na kama muktadha au kama wazo. Maisha ya mwanadamu  kwa kifupi, daima ni maisha halisi, kwa wakati na mahali popote anapoishi kila mmoja  na ubinadamu mzima katika kuishi leo na kesho. Na ndiyo mantiki inayokita katika uhusiano ambao unatoa fursa ya kufikiria kwa namna ya dhati katika mjadala mkubwa wa mada kuu ya familia na ya maisha.

Askofu Mkuu Paglia katika  hotuba yake, amekumbuka  Baba Mtakatifu kwamba alitambua vema juu ya uhusiano huo wa kina na ambapo kwa ngazi ya kitaasisi akaunganisha kiini cha tafafari mbili za elimu kuhusu familia na ya maisha  ya Taasisi ya Yohane Paulo II na Taasisi ya Elimu kwa ajili ya Maisha ambazo kwa pamoja ziliungaishwa na kuundwa kwa  Baraza moja la kipapa kwa ajili ya ufanisi mzuri wa kazi ya kichungaji ambalo linaitwa Baraza la Kipapa la Maisha, ndoa na Familia. Hata hivyo amesema, inakuwa tasa na haina haja ya  kuzungumza au kutetea familia yenyewe, bila kuzingatia mada halisi, mahali na nyakati ambazo muungano huo wenye rutuba unakua, kama inavyosisitizwa katika Wosia wa  Amoris Laetitia namba 3.

Ubora wa sasa wa kibinadamu ambao unaunda familia na utatoa fursa ya maisha ndilo jibu kubwa zaidi katika mazoezi yote yanayohusu kisiasa, kijamii hadi kufikia ya kidaktari na ambao wakati mwingine wanataka kutenganisha kizazi kutoka katika upendo unao fanya sisi kuwepo na kulindwa. Kurudisha maisha ya mwanadamu katika muktadha wa familia kwa asili na katika kazi inamaanisha kutamka neno lenye nguvu dhidi ya utamaduni huu ambao unavamia nchi za Magharibi, lakini pia  bara la Afrika haliwezi kudai kuwa halijaguswa, yaani suala la  ubinafsi kabisa, yaani kujifunga binafsi  na uhusiano na wengine. Hakuna mtu ambaye ni kisiwa, ameongeza kusema Askofu Mkuu Paglia. Sisi sote tumeunganishwa kati yetu. Na sisi sote ni washirika wa uhusiano wa kifamilia na sisi sote ni watoto, ndugu wote na dada wa kila mmoja."

23 September 2019, 13:01