Maaskofu Nicaragua wametangaza kusali kwa ajili ya amani na haki kuanzia tarehe 8 hadi 15 Septemba 2019 katika kilele maadhimisho ya siku ya uhuru wa nchi hiyo Maaskofu Nicaragua wametangaza kusali kwa ajili ya amani na haki kuanzia tarehe 8 hadi 15 Septemba 2019 katika kilele maadhimisho ya siku ya uhuru wa nchi hiyo 

NICARAGUA:Maaskofu kutangaza wiki ya maombi ya amani na haki!

Kuanzia tarehe 8-15 Septemba 2019 nchini Nicaragua,Baraza la Maaskofu katoliki nchini humo wametangazia waamini na watu wenye mapenzi mema kuomba kwa ajili ya Amani na Haki ya nchi hiyo,kufuatia na matarajio ya maadhimisho ya siku ya uhuru,itakayofikia kilele chake siku ya Dominika tarehe 15 Septemba.Nchini Nicaragua inaishi kipeo kikubwa cha kisiasa na kijamii!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baraza la Maaskofu nchini Nicaragua (CEN) limetengaza Wiki ya maombi kwa ajili ya kuombea nchi, maombi yanayoongozwa na Kauli mbiu “Haki na amani zitagusana” iliyotolewa katika Zaburi ya 85. Wiki ya maombi inaanza tarehe 8 Septemba katika sikukuu ya kukumbuka kuzaliwa kwa Bikira Maria na kuhitimishwa tarehe 15 Septemba siku ambayo inakwenda sambamba na Siku Kuu ya kitaifa, wanapokumbuka kupata uhuru wao, na ambapo maaskofu wanawaalika wasali kwa Mungu kwa ajili ya amani na haki ya nchi.

Askofu Jorge Solórzano Pérez, wa Jimbo katoliki Granada, ametangaza kuwa wiki ya sala itafunguliwa na Misa kuu Takatifu katika kanisa Kuu Jumapili tarehe 8 Septemba. Hata hivyo kila Jimbo linaweza kuandaa wiki hiyo ya sala kwa mujibu wa hali halisi iliyopo mahalia, hata kama maaskofu wametoa mwelekezo na ushauri kwamba kila siku pangekuwapo nia ya kusali kwa njia ya makundi  maalum yanayohusika  kwa mfano:Dominika tarehe 8 septemba watoto na makatekista; Jumatatu 9 Septemba, kwa ajili ya wazalendo wote; Jumanne 10 Septemba Makleri, watawa na wahudumu wa kichungaji: Jumatano 11 Septemba,  Vyama vya kitume vya kilei; Alhamisi tarehe 12 Septemba, famiglia zote; Ijumaa 13 Septemba, maadhimisho ya kitubio kwa ajili ya wote; Jumamosi 14 Septemba kwa ajili ya wagonjwa; na Jumapili 15 Septemba kwa ajili ua  vijana na sala kwa ajili ya viongozi washika  madaraka ya nchi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika la habari za kimisionari Fides linathibitisha kwamba katika  mantiki hiyo inawezekana kwa hakika kusali kwa ajili ya  nchi yote ya Nicaragua kwa ujumla kwa ajili ya hali halisi ambayo nchi ya Nicaragua inaishi, kama vile mapambanodhidi ya haki, uhuru, maisha ya kidemokrasia ya nchi, kwa ajili ya matendo ya hali ya wafungwa wasio na hatia.

Naye Askofu Rolando Josè Álvarez Lagos, wa Jimbo katoliki la Matagalpa aidha amewaalika waamini  kuadhimisha misa kwa ajili ya nchi bila kuwa na hofu. Kwa hakika tarehe 15 Septemba nchini Nicaragua wanasheherekea siku ya uhuru kitaifa. Ndiyo maana Askofu Álvarez Lagos anawalika watu wote kupeperusha hata  bendera za nchi kama ishara ya uzalendo, wakati wa wiki hii ya maombi  na kwa ajili ya mwezi mzima, huku akiwashauri wafanye matendo ya upendo kwa ajili ya  maskini wao wote, wenye njaa, na wale ambao wametengwa na jamii, hata na wale wenye kujidai kuwa na mabavu zaidi, kwa kufanya hivyo ni kama kuwa mshiriki halisi wa hali halisi ya nchi amethibitisha.

Wiki ya maombi kwa ajili ya sala  nchini Nicaragua, itaendeshwa katika hali ambayo iko na mivutano  kwa waamini kwa sababu ya mfumo wa  utawala wa mabavu wa Rais Ortega dhidi ya Kanisa, maaskofu na wanaamini  ambao wanazisi kupinga hali ya udikiteta.  Kwa mujibu wa mahojiano ya hivi karibuni, Askofu Juan Abelardo Mata, wa  Jimbo Katoliki la Estelí na  Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Nicaragua, alikuwa amekubali kuwa, Kanisa Katoliki linahisi kuteswa na nguvu za kijeshi za serikali na kwa  jinsi gani ameweza kujionea yeye mwenyewe huko Masaya. Askofu Mata, katika mahojiano hayo tarehe 26 Agosti 2019, amesasisha tena  kuhusu nafasi ya Baraza la Maaskofu katika mtazamo wa mazungumzo na serikali. Katika mahojiano hayo alithibitisha kwamba, nafasi yao itaendelea kuwapo hadi kufikia hupatikanaji wa uwazi na ukweli, kwa maana, kila majadiliano yanakuwa ni majanga, hakuna ujenzi wa amani au ujenzi wa taifa. Na kwamba kufanya Majadiliano hayana maana ya kufanya kile ambacho wewe unataka na kana kwamba  mimi ninapaswa nijiweke chini ya mapenzi yako au wewe ya kwangu. Hapana, kufanya majadiliano au mazungumzo maana yake ni kutafuta jambo linalounganisha pande zote mbili na mwishowe kukuza ule wema wa pamoja, lakini kinyume na hiyo Askofu amebainisha hawawezi kuamini katu juu ya hilo.

MAASKOFU NICARAGUA
07 September 2019, 11:15