Vatican News
Katika fursa ya ufunguzi wa Mwaka wa Shule,tarehe 3 Septemba 2019 umefanyika Mkutano Mkuu wa 26 wa Baraza la Shule Katoliki nchini Lebanon Katika fursa ya ufunguzi wa Mwaka wa Shule,tarehe 3 Septemba 2019 umefanyika Mkutano Mkuu wa 26 wa Baraza la Shule Katoliki nchini Lebanon  

LEBANON:Mkutano wa Shule Katoliki kuhusu kipeo cha shule zisizo za kiserikali!

Tarehe 3 Septemba 2019,umefanyika mkutano mkuu wa 26 wa mwaka,uliotishwa na Sekretarieti ya Shule katoliki nchini Lebanon kwa kuongozwa na kauli mbiu"tuelimishe kwa pamoja".Mkutano huo umejikita kutazama kwa namna ya pekee juu ya kipeo cha taasisi zisizo za kiserikali.

Na Padre Angelo Shikombe – Vatican News

Wakati wa kufungua Muhula mpya wa mwaka wa masomo, Baraza la shule Katoliki nchini Lebanon limetoka kifua mbele na kaulimbiu ya Tuelimishe kwa Pamoja”, wakati wa  mkutano wake wa  26 wa  mwaka ulioitishwa na sekretarieti ya shule katoliki nchini Lebanon, tarehe 3 septemba 2019 katika chuo cha Mama yetu wa Louaiz, huko Zouk Mosbeh, kilichoko kilomita 12 kaskazini mwa mji wa Beirut.

Kwa miaka mitatu mfululizo shule Katoliki nchini Lebenon zimejadili katika mkutano tatizo la kiuchumi linalozikumba shule nyingi binafsi, tatizo    hilo linaloweza kuwa pia linasababishwa na sheria ambayo iliwekwa na serikali katika viwango vya mishahara kwa wafanyakazi wa sekta za kijamii, pamoja na kuzingatia hadhi ya shule. Kwa mara ya kwanza, wakufunzi wamelipokea suala hili kwa namna tofauti tofauti. Taarifa hii  kutoka Shirika la habari za kimisionari, Fides ikipembua kwamba, Baraza kuu la shule Katoliki huko Lebanon wamefikia muafaka wa kutoa kaulimbiu inayohamasisha ushirikiano katika ya uongozi wa serikali na shule binafsi katika jitihada za kumkomboa mwanadamu katika dimbwi la ujinga, umaskini na maradhi. Taasisi hizo binafsi zinazojikita katika utoaji wa huduma ya Elimu ili kumwingiza mwanadamu katika mwanga wa kristo zinahitaji ushirikiano wa pamoja kutoka Serikali na asasi zisizo za serikali.

Hadi mwisho wa mkutano huo mjadala uliotawala ni    namna ya kutatua matatizo ya utegemezaji wa shule nyingi za kikatoliki hasa zilizoko pembezoni mwa nchi. Pamoja na sheria iliyopitishwa ya mwaka 2017 juu ya mishahara na ruzuku za walimu na wafanyakazi wengine katika shule binafsi. Aidha Serikali ya Lebanon imeonekana kuendeleza msimamo wake wa kuzitaka shule binafsi kubeba majukumu yao ikiwemo ni pamoja na kuwategemeza walimu na wafanyakazi wengine.

Patriaki wa kimaroniti Berchara Boutros Rai amesema, Serikali itachukuwa wajibu wake.  Katika hotuba yake amerudia ombi la kutokushindana na serikali na shule za kitaifa, hivyo kila shule inapaswa kubeba wajibu wake. Aidha Patriaki amewatuhumu wanasiasa wa Lebanon kwa kuweka viwango katika shule binafsi ambazo zina haki ya kutumia lasimali za jamii ambazo kwa sasa ni lazima zitegemeze shule ya binafsi zilizoko katika peo.  Aidha Shirika la Habari za kimisionari, fides linatoa taarifa kuwa huko Lebanon shule katoliki hadi sasa zinachukuwa takribani laki mbili ya wanafunzi, (200,000) hivyo  wanashawishika kutoitekeleza sheria ya mishahara inayoweza kutatuliwa kwa njia ya majadiliano na makubaliano. Mjadala wa sheria iliyopitishwa mwaka 2017 juu ya Mishahara ya wafanyakazi, huenda ukaingizwa katika mapendekezo ya  kamati ya ushauri (l’Lcc)ya  mkutano wa umoja wa Mataifa  utakaofanyika Ginevra Mei 2020.

SHULE KATOLIKI LEBANON
05 September 2019, 12:58