Tafuta

Vatican News
Hospitali ya Sant'Egidio di Zimpeto" ni chemchemi ya matumaini kwa watu wa Mungu nchini Msumbiji katika mchakato wa mapambano wa maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI. Hospitali ya Sant'Egidio di Zimpeto" ni chemchemi ya matumaini kwa watu wa Mungu nchini Msumbiji katika mchakato wa mapambano wa maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI.  (Vatican Media)

Hija ya Papa Francisko Msumbiji: Mradi wa DREAM: UKIMWI

Mradi wa “DREAM” ulipata chimbuko lake nchini Msumbiji na kwa sasa unaendelea kutoa tiba kwa wagonjwa zaidi ya 500, 000 katika nchi 10 za Kiafrika. Hii ni taarifa fupi ya Dr. Cacilda Massango, Mratibu wa Mradi wa “DREAM” nchini Msumbiji. Wanawake waliopata fursa ya kujifungua bila ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, wakishakupona na wao pia wanajiunga katika huduma!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Hospitali ya “Santo Egidio de Zimpeto” ilizinduliwa tarehe 7 Juni 2018 na Rais Filipe Jacinto Nyusi wa Msumbiji. Inaendesha mradi mkubwa wa kuzuia maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto unaojulikana kama “DREAM” yaani “Disease Relief Through Excellent and Advanced Means”. Huu ni Mradi mkubwa uliozinduliwa na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kunako mwaka 2002 na kwa sasa unatekelezwa katika nchi 10 za Kiafrika. Lengo ni kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa Mama mjamzito kwenda kwa mtoto pamoja na kuendelea kudhibiti magonja nyemelezi. Wanawake wengi wajawazito waliokuwa wameambukizwa Virusi vya Ukimwi, wakajifungua bila watoto wao kuathirika, wanaliona jambo hili kuwa ni muujiza mkubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Mradi wa “DREAM” ulipata chimbuko lake nchini Msumbiji na kwa sasa unaendelea kutoa tiba kwa wagonjwa zaidi ya 500, 000 katika nchi 10 za Kiafrika. Hii ni taarifa fupi ya Dr. Cacilda Massango, Mratibu wa Mradi wa “DREAM” nchini Msumbiji. Wanawake waliopata fursa ya kujifungua bila ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, wakishakupona na wao pia wanajiunga katika mchakato wa huduma kwa wagonjwa, kwa kuwasindikiza katika safari yao ya matibabu. Dr. Cacilda Massango, Mratibu wa Mradi wa “DREAM” nchini Msumbiji ni kati ya wanawake waliopata bahati ya kujifungua watoto bila maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, leo hii ni kati ya wafanyakazi wa Hospitali hii wanaotoa huduma kwa waathirika wa Ugonjwa wa Ukimwi. Hii ni familia mpya ambayo imemwezesha kupata tiba na kurudisia tena utu na heshima yake kama binadamu na kwamba, anayo matumaini kwa leo na kesho iliyo bora si tu kwake binafsi, bali hata kwa watoto wake. Kwa njia ya Mradi huu, wananchi wengi wa Msumbiji wamepata matumaini mapya!

Mradi Dream

 

06 September 2019, 15:06