Tafuta

Askofu mkuu Francisco Chimoio amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwatembelea na kuonana na watu wa Mungu nchini Msumbiji mubashara kabisa Askofu mkuu Francisco Chimoio amemshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kuwatembelea na kuonana na watu wa Mungu nchini Msumbiji mubashara kabisa 

Hija ya Papa Francisko Msumbiji: Furaha ya watu wa Mungu!

Kanisa nchini Msumbiji litaendelea kutangaza na kushuhudia upendo wa Kiristo unawao wabidiisha. Familia ya Mungu nchini Msumbiji inamshukuru Papa Franciskokwa kujishusha kabisa na kuwainamia wagonjwa ili kuwafariji; amewatia shime wakleri, watawa na makatekista kusonga mbele kwa moyo mkuu ili kutangaza na kushuhudia furaha ya Injili, jambo ambalo si rahisi hata kidogo.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Askofu mkuu Francisco Chimoio wa Jimbo kuu la Maputo kwa niaba ya familia ya Mungu nchini Msumbiji, Ijumaa, tarehe 6 Septemba 2019 amemshukuru Baba Mtakatifu kwa kuwatembelea na kuonana nao mubashara kama kumbu kumbu ya miaka thelathini na moja, tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipotembelea Msumbiji. Hija hii ya kitume imejenga na kuimarisha umoja, upendo na mshikamano wa kirafiki. Wanamshukuru kwa uwepo wake wa karibu Msumbiji ilipotumbukia kwenye majanga na maafa makubwa na kwamba, hija hii imekuwa ni chemchemi ya matumaini, alama ya upatanisho na amani. Mapigano yaliyojitokeza hivi karibuni huko Cabo Delgado yanatishia mchakato mzima wa upatanisho wa kitaifa nchini Msumbiji, bila kusahau umaskini wa kanuni maadili na utu wema unaoendelea kusigina maisha ya wananchi wa Msumbiji.

Kanisa nchini Msumbiji litaendelea kutangaza na kushuhudia upendo wa Kiristo unawao wabidiisha. Familia ya Mungu nchini Msumbiji inamshukuru Baba Mtakatifu kwa kujishusha kabisa na kuwainamia wagonjwa ili kuwafariji; amewatia shime wakleri,watawa na makatekista kusonga mbele kwa ari na moyo mkuu ili kutangaza na kushuhudia furaha ya Injili, jambo ambalo si rahisi hata kidogo. Baba Mtakatifu amekazia mchakato wa upatanisho kama sera kwa viongozi wa kisiasa na zaidi ya yote, amekazia utunzaji bora wa mazingira nyumba ya wote kama zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kile kijacho. Kimsingi, Baba Mtakatifu amekazia umoja na udugu; furaha na matumaini yanayobubujika kutoka kwa Kristo Yesu. Familia ya Mungu nchini Msumbiji itaendelea kujizatiti katika mchakato wa ujenzi wa mshikamano na udugu wa kibinadamu, wakifuata mfano wa Kristo Yesu. Itakuwa ni vigumu sana kwa familia ya Mungu nchini Msumbiji kusahau hija hii ya kitume!

Askofu mkuu Francisco

 

 

06 September 2019, 16:45