Tafuta

Vatican News
Katiba ya Kitume "Vultum Dei Quaerere" yaani "Kuutafuta Uso wa Mungu" ni nyenzo msingi katika mchakato wa kupyaisha uaminifu wa karama sanjari na kusikiliza kilio cha walimwengu. Katiba ya Kitume "Vultum Dei Quaerere" yaani "Kuutafuta Uso wa Mungu" ni nyenzo msingi katika mchakato wa kupyaisha uaminifu wa karama sanjari na kusikiliza kilio cha walimwengu.  (Vatican Media)

Hija ya Papa Francisko nchini Madagascar: Kuutafuta Uso wa Mungu: Uaminifu & Usikivu

Katiba ya Kitume “Vultum Dei Quaerere” Yaani “Kuutafuta Uso wa Mungu” inayowachangamotisha kupyaisha uaminifu wao kwa karama za mashirika yao ya kitawa, sanjari na kujiweka wazi kusikiliza na kujibu kilio cha familia ya Mungu sehemu mbali mbali za dunia. Muunganiko wao katika Kristo na Kanisa lake, ni chemchemi ya furaha kwa baraka na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kuna haja ya kudumisha majiundo makini; umuhimu wa tafakari ya Neno la Mungu; vigezo muhimu kwa Jumuiya ya Kimonaki kuweza kujitegemea pamoja na uwezekano wa kuunda Shirikisho la Wamonaki ndani ya Kanisa. Haya ni kati ya mambo ambayo Baba Mtakatifu Francisko anayapatia kipaumbele cha pekee katika Katiba ya Kitume “Vultum Dei Quaerere” Yaani “Kuutafuta Uso wa Mungu” Waraka ambao unafupishwa kwa herufi “VDQ”, uliotiwa sahihi na Baba Mtakatifu Francisko wakati wa maadhimisho ya Sherehe ya Watakatifu Petro na Paulo miamba wa imani hapo tarehe 29 Juni 2016 kwa ajili ya Wamonaki wa Mashirika ya Taamuli.

Sr. Maria Maddalena dell’Annunciazione, Mama mkuu wa Shirika la Wakarmeli wa ndani nchini Madagascar, Jumamosi, tarehe 7 Septemba 2019, katika risala ya kumkaribisha Baba Mtakatifu Francisko kusali pamoja na watawa wa Mashirika ya ndani, kwa niaba yao wote amemshukuru kwa kuwapatia Katiba ya Kitume “Vultum Dei Quaerere” Yaani “Kuutafuta Uso wa Mungu” inayowachangamotisha kupyaisha uaminifu wao kwa karama za mashirika yao ya kitawa, sanjari na kujiweka wazi kusikiliza na kujibu kilio cha familia ya Mungu sehemu mbali mbali za dunia. Muunganiko wao katika Kristo na Kanisa lake, ni chemchemi ya furaha kwa baraka na neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hii imekuwa ni fursa makini ya kusali kwa ajili ya kuombea familia ya Mungu nchini Madagascar.

Ni katika sala na tafakari ya kina, ndimo wanamoweza kuchota nguvu inayowaunganisha kwa pamoja. Watawa hawa wana mshukuru na kumpongeza Baba Mtakatifu Francisko kwa kutenga muda wa sala na tafakari kama kielelezo cha upendo kwa Kristo na Kanisa lake. Shirika la Wakarmeli wa ndani nchini Madagascar, linajiandaa kwa ajili ya kuadhimisha Jubilei ya Miaka 100 ya uwepo na utume wao! Kumbe, wamemwomba Baba Mtakatifu Francisko kuwapatia baraka yake ya kitume kama sehemu ya maandalizi haya.

Watawa Madagascar

 

07 September 2019, 16:37