Tafuta

Vatican News
Shirika la Roho Mtakatifu Jumapili ya tarehe 29 Septemba 2019 limeadhimisha Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo nchini Gabon. Shirika la Roho Mtakatifu Jumapili ya tarehe 29 Septemba 2019 limeadhimisha Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo nchini Gabon.  

Gabon:Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa Shirika la Roho Mtakatifu

Askofu mkuu Francisko Escalante Molina Balozi wa Kitume wa Vatican nchini Gabon na Congo Brazzaville tarehe 29 Septemba 2019 ameongoza misa ya maadhimisho ya Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Shirika Shirika la Roho Mtakatifu nchini Gabon.

Na Padre Angelo Shikombe, - Vatican

Shirika la Roho Mtakatifu Jumapili ya tarehe 29 Septemba 2019 limeadhimisha Jubilei ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa Shirika hilo nchini Gabon. Askofu mkuu Francisko Escalante Molina Balozi wa Kitume wa Vatican nchini Gaboni na Congo Brazzaville amesema, maadhimisho hayo yameanza mwaka 2018 ambapo kila jimbo lilipata fursa ya kusali na kumshukuru Mungu na kuna Mapadre na Mashemasi waliopewa Sakramenti ya Dararaja Takatifu. Kilele hicho cha Jubilei ya miaka 75 ya umisionari nchini Gabon kiliweza pia kuhudhuriwa na Askofu mkuu Giovanni Pietro Katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu. 

Akiendelea kuelezea namna maadhimisho yalivyofanyika, Askofu mkuu Francisko Escalante Molina alifurahishwa na namna mikutano mbalimbali ya kichungaji na ki-utamadunisho ilivyofanyika kwa ufanisi mkubwa na jumuiya za wakleri, watawa na walei kuonesha ushirikiano mkuu. Askofu mkuu Francisko Escalante Molina liweza kuwapongeza pia taifa la Mungu la Gabon kwa namna walivyohitimisha Jubilei hiyo kwa kishindo kikubwa.  Askofu mkuu Francisko Escalante Molina ameonesha kuguswa zaidi na ushirikiano wa Maaskofu kwa namna kila Askofu alivyo jibidisha kuhuisha roho ya uinjilishaji jimboni mwake na hatimaye kujumuika katika kilele cha Jubilei hiyo iliyo fanyika Jumapili ya tarehe 29 Septemba 2019.

Katika ngazi ya kitaifa, maadhimisho hayo yalilenga kuhamasisha utoaji wa huduma msingi katika uwanja wa kisiasa, sekta za elimu na afya, na kulikuwepo na uhamasishaji wa waamini walei kushirika katika utuoji wa huduma jamii. Katika maadhimisho hayo kumekuwepo pia uwakilishi wa Baraza la Maaskofu wa Afrika ya Kati yaani (ACERAC) kutoka nchi ya Cameroon, Congo Brazzaville, Gaboni, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Guinea ya Equator.

Kwa mujibu wa habari kutoka Shirika la habari la kimisionari duniani (Fides) zimesema, Askofu mkuu Giovanni Pietro, Katibu msaidizi wa Baraza la kipapa la Uinjilishaji wa watu, aliwapongeza wanashirika la Roho Mtakatifu kwa hatua kubwa waliyopiga na kwa zawadi kubwa walizopata kutoka kwa Mungu hasa kuwapata Maaskofu wa Shirika hilo. Pia Askofu mkuu Francisko Escalante Molina amewashukuru Taifa lote la Mungu na ametoa ujumbe wake akihamasisha juu ya umuhimu wa uenezaji wa kimisionari ulimwenguni. Hata hivyo, amesisitiza kuwa bado kuna umuhimu wa kuendelea na shughuli za umisionari nchini Gabon.  

30 September 2019, 12:03