Serikali nchini Eritrea imetaifisha baadhi ya shule katoliki, kama ilivyokuwa imetaifasha tayari mahospitali Serikali nchini Eritrea imetaifisha baadhi ya shule katoliki, kama ilivyokuwa imetaifasha tayari mahospitali 

Eritrea:Serikali yataifisha shule na hospitali za Kanisa Katoliki!

Maaskofu nchini Eritrea, wamemwandikia barua Waziri wa Elimu mara baada ya kutaifishwa kwa shule zinazomilikiwa na Kanisa Katoliki nchini humo. Hii pia imefuatia mara baada ya kutaifisha majengo ya vituo vya afya nchini humo. Katika barua yao wanabainisha juu ya dhuluma na nyanyaso za Serikali ya Asmara dhidi ya Kanisa Kanisa Katoliki nchini humo.

Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Taasisi ya kihistoria, ambayo kwa kipindi cha karne imejikita katika jukumu muhimu la kiutamaduni na kiroho, katikakuhudumia Kanisa na nchi kwa ujumla. Baadaye kutaifisha majengo ya afya na kubinafsisha zaidi zahanati 21 na baadaye tarehe 3 Septemba kutaifisha mashule matatu muhimu ya shule ya msingi, na sekondari, zilizokuwa zinaendeshwa na Ndugu wa Lassalliano huko Cheren na Ndugu wadogo wa Kapuchini huko Addi-Ugri - Massawa.

Maandamano ya halali na halali ya Wakatoliki

Katika hatua hizo zote, maaskofu wanaandika katika barua iliyotumwa kwa waziri wa elimu ya umma kwa  Eritrea, kwamba wanao ulazima wa kuandamana kihalali.  Katika waraka wake wanatumia maneno mahiri ya kulaani kazi ya serikali ya Asmara uliotiwa sahini na Menghisteab Tesfamariam, Askofu mkuu wa kanisa Kuu la  Asmara, Thomas Osman, Patriaki wa Barentu, Kidane Yebio, patriaki wa Cheren na Fikremariam Hagos, epark wa Segheneyti.

Kansa Katoliki na Makanisa mengine ya kikirato yamekuwa na jumumu daima la utume kwa ajili ya wema wa Nchi, ambayo  daima imekuwa ikijitolea kuhamasisha na kukuza fungamani ya mwanadamu. Hawa wamekuwa wakijikita katika mantiki ya elimu, afya na mandeleo ya kijamii kwa ujumla, na siyo kwa ndani tu katika msunguko wa mambo matakatifu, lakini katika makambi yaliyo funguliwa katika shule, zahanati na hospitali, mahali popote. Hii ni dhahiri kwa wanaume na wanawake kudai haki na mahitaji ya kutibiwa,kuelimishwa na Kanisa linahitaji kuhisi uwezo wake wa  kuchangia ustawi wao ndani na nje ya nchi. Kama ambavyo imekuwa katika miaka  2000 ya historia, Kanisa leo hii linatafuta haki yake na kati ya haki hizo ni mali zake ambazo zinasaidia kuendeshe utume wake. Na kwa kuwa ni suala la haki ambazo ni asili na ambazo Mwenyezi Mungu mwenyewe aliwakabidhi. Kwa maana hiyo,Maaskofu wa Eritrea wanatoa ushauri kurudishiwa mali zao!

Mchango wa shule katoliki ni wenye thamani ya kuhamasisha ufungamani wa kibinadamu

Kuhusiana na mtazamo wa seikali kutaifisha shule, Maaskofu wanasisitiza kuwa hakuna lengo lolote ambalo linaweza kupendekezwa kwa Kanisa katika uendeshaji wa taasisi zake za elimu kama siyo ule ukarimu, usahihi na shauku ya kuchangia kuhamasisha mfungamano wa binadamu leo hii. Hii wanaweza kuhushudia bila udanganyifu kwa wanaume na wanawake wa kila dini na katika harakati za maisha ambao wamepitia katika madarasa yao na wanapokea mafundisho ya maisha na leo hii wametawanyika duniani kote. Aidha wanakumbusha  nafasi ya kihistoria ambayo imejikita katika elimu ya dini na siyo katoliki tu bali ya kiorthodox , kiislam na kiyahudi ambao wametoa mchango wa mafunzo, katiba na ufafanuzi wa utambulisho na utamaduni. Aidha mifumo ya kisasa ya kiutawala, mabadiliko ya utambuzi wa kisiasa na tamaduni ya fasihi, maendeleo ya lugha, vimepata wasomi wao bora wa Eritrea ambao wametoka katika shule zinazoendeshwa na Kanisa Katoliki na madhehebu mengine ya kidini yaliyo msingi nchini humo. Hata hivyp  Maaskofu  Lakini wanawakumbusha kuwa  haipaswi kusahauliwa michango yao katika michakato ya kisiasa na katika mapambano ya uhuru na ambayo wanachukua nafasi muhimu katika historia ya Eritrea.

Maswali ya maaskofu

Maaskofu wanauliza baadhi ya maswali kwamba je ni jinsi gani ya kuliumba suala hili la kutaifishia Kanisa taasisi zake za elimu, vifaa ambavyo  kwa kina vimechangia sana ukuaji, maendeleo na maendeleo ya wazalendo wote? Je! Ni ni misingi gani wamethubutu kutangaza, kwa matendo badala ya maneno bila kuwa na jina lolota na kila haki ya kudai dhidi ya taasisi hizi? Ikiwa hii siyo chuki dhidi ya imani na dini, kuna nini kingine? Kwa kuondoa watoto na vijana kutoka katika miundo inayoweza kufunda kwa viwango vya juu vya kumcha Mungu na sheria ya maadili, ni vizazi vipi vijavyo wanataka kujiandaa kwa ajili ya mustakabali endelevu wa nchi hii? Hata hivyo katika barua hiyo, maaskof wa Eritrea wanabainisha kwa jinsi gani mara kwa mara wametamani kukutana na viongozi wa serikai kufanya mazungumzo  juu ya kila kitu kuhusu hali ya Kanisa, bila jibu au kuzingatia lolote lile. Kufuatia na hili, viongozi wa Asmara wanasema hawakusema kutoa sababu yoyote msingi ya kutengewa siku moja ya kukutana. Aidha katika taasisi zao hakuna ukiukwaji wa kanuni za usimamizi wa shule au ukiukwaji wa sheria au upungufu wa sheria au kuwa na hatia ya upungufu wa masomo au ksa la tume kutotimiza wajibu wao. Na  badala yake,  maaskofu wanadai  kuwa shule zao  zimejitofautisha kwa ubora na kiwango", kwa kufanikiwa kuwa na matokeo bora  zaidi katika mitihani ya kitaifa na  ambayo inapaswa kutambuliwa na kutiwa moyo. Vitu hivi,  wanasema maaskofu  Serikali inajua, na ikiwa inafaa, inaweza kusemwa wazi na kuchukua mikononi mwao ripoti ambazo zimetumwa kila wakati katika wizara ya elimu kwa miaka yote.

Mahali ambapo hakuna uhuru na sheria 

Hata hivyo maaskofu wa Eritrea wanathibitisha kwa  siyo tatizo linaloangaikiwa na  Kanisa katoliki tu ,kwa maana katika kuzuia kwa dhati jamii ya watu na Kanisa kuendeleza utume wao kwa faida ya wanaume na wanawake wa nyakati hizi katika nchi ni kuishia kulazimisha au kuondoa nafasi ya zoezi hali ya uhuru na haki msingi za mtu ulimwenguni. Wakati kila kitu kinapotawaliwa na Serikali, basi uhuru wa mtu mwenyewe unakataliwa na shughuli zake zinalemazwa. Na mahali ambapo uhuru na sheria vinakataliwa, hakuna nafasi zaidi ya  amani, au ya uhuru, au ya sheria . Lazima iwe wazi kwa wote, wanapendekeza maaskofu, na kwamba, wakati taasisi hizi zitaifishwa  na haki za Kanisa zinakiukwa, matokeo ya uharibifu yatakuwa makubwa  katika mabega ya watu wote na kwa taifa zima. Kufuatia na hilo ombi lao la haki halitasimama kwasabubu barua yao inahitimishwa kwamba kwa sababu maazimio ya hivi karibuni ya serikali  yamekwenda kinyume na haki na uhuru halali wa Kanisa lazima waliangalie suala hili na kulifunga mara moja. Na kama suala hili halitapata suluhisho kwa muda mrefu katika Kanisa la Eritrea na waamini wake hawataacha kudai haki kutoka kwa wale wanaoshikilia nguvu ya kuisimamia madaraka. https://nemo.vaticannews.va/editor.html/content/vaticannews/sw/church/news/2019-06/eritrea-sala-kwa-ajili-ya-nchi-ya-aritrea-kufuatia-kufungwa.html

https://www.vaticannews.va/sw/church/news/2019-07/sekretarieti-kuu-kanisa-katoliki-eritrea-ercs-utaifishaji-afya.html

12 September 2019, 15:12