Vatican News
Dhoruba Dorian bado inazungukia visiwa vya Marekani na watu saba wamekufa huko Bahamas Dhoruba Dorian bado inazungukia visiwa vya Marekani na watu saba wamekufa huko Bahamas  (AFP or licensors)

BAHAMAS:Watu 70elfu wamekumbwa na dhoruba Dorian!

Askofu Mkuu Patrick Christopher Pinder wa jimbo Katoliki la Nassau,amesema kwamba wana zoezi kubwa sasa mbele yao kwa mahitaji ya msaada mkubwa katika jimbo peke yake lililoko katika Kisiwa cha Bahamas,mahali ambapo wakatoliki wanawakilisha karibia asilimia 14 ya watu wote. Watu 70,000 hawana mahali pa kukaa na wakati huo watu saba wamekufa kufuatia na dhoruba Dorian inayoendelea kuzungukia visiwa vya Marekani.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican News

Kimbunga kiitwacho Dorian chenye nguvu zaidi kimepiga visiwa vya Bahama nchini Marekani na kuvunja rekodi ya vimbunga vyote vilivyowahi kupiga na kusababisha maafa makubwa. Hii ni dhoruba ya pili katika rekodi ya bahari ya atlantiki ambayo imeweza kustahimili mawimbi mpaka kufikia 285 kilometa kwa saa, kwa mujibu wa wataalam. Dhoruba Dorian ya Bahamas ikiwa katika safari yake kuelekea  upande wa bahari ya Atlantiki imesababisha vifo vya watu saba na kuwajeruhi wengine 21. Na Kimbunga hicho kinaendelea kusonga taratibu magharibu na kinaweza kufika mashariki ya bahari ya Marekani, majimbo ya Marekani ya Florida, Georgia na South Carolina yote. Dhoruba hii inavuma vya kasi ndogo ambayo inasafiri toka magharibi ambayo ni kilometa 9 kwa saa ambayo ni sawa na mph 6.

Askofu Mkuu Pinder anaomba msaada kwa ajili ya waathirika wa Dorian: Naye Askofu Mkuu Patrick Christopher Pinder wa jimbo Katoliki la Nassau, amesema kwamba wana zoezi kubwa sasa mbele yao na watahitaji msaada mkubwa katika jimbo ambalo ni peke yake lililoko katika Kisiwa cha Bahamas, mahali ambapo wakatoliki wanawakilisha  karibia asilimia 14 ya watu wote. Na wakati huo huo matukio ya dhoroba ya Dorian, bado hayajatulia. Dhoruba isiyosemekana anasema Askofu Mkuu Pinder, imefika Kaskazini Magharibu mwa Bahamas tangu Jumapili na bado inaendelea kuvuma na upepo mkubwa na mvua. Imekuwa dhoruba kali yenye nguvu na uharibifu mkubwa! Upepo huo mkubwa unaelekea katika visiwa vya Abaco na Grand Bahama. Zaidi ya watu 70,000 wameathiriwa na kwa bahati mbaya, habari zinathibitisha kuwa watu saba wamefariki kufutia na dhoruba hiyo amesema Askofu Mkuu Pinder.

Jimbo Kuu katoliki linahitaji msaada wa kibinadamu: Wakati dhoruba  inaendelea na kasi zake, ni lazima kufikiria kwa namna bora ya haraka kwa ajili ya kuwasaidia watu waliopatwa na janga hili. Kwa sasa, Askofu Mkuu anasema, hali ya hewa bado haijawezesha kutoa tathimini zaidi kuhusiana na athari za Dorian. Kwa uhakika kazi ya kukarabati itahitaji muda, lakini wakati huo ni wazi kwamba lazima kufikiria watu hao waliopatwa na mkasa huo. Jibu hili linatakiwa kuwa na zoezi kubwa na lenye rasilimali sana. Maji, chakula vifaa vya usafiri, kwa ajili ya watoto, mambo hayo na mengine ni muhimu sana na ukarabati utahitajika.

Ni dhoruba ya kihistoria kwa mujibu wa wataalam: Wataalam na wanasayansi wametaja kuwa kimbunga hicho ni kimbunga kikubwa katika historia ya Bahamas kuwahi kutokea. Waziri mkuu wa Bahamas Hubert Minnis amethibitisha vifo vya  watu hao na 21 waliojeruhiwa. Uharibifu mkubwa wa mali  umetokea katika eneo ambalo limekumbwa na dhoruba hiyo. Kwa mujibu wa  kituo maalum cha janga la kimbunga kimesema kuwa kimbunga hicho kilipiga majira ya saa kumi, dhoruba hiyo ilitokea pembezoni mwa mashariki mwa Bahama, na kutua katika kisiwa cha Abaco. Grand Bahama ina jumla ya idadi ya watu takribani 50,000, wanaoishi umbali wa kilometa 100 mashariki mwa pwani ya Palm huko Florida. ' Mpaka sasa hakuna kauli rasmi kutoka kwa maafisa wa visiwa vya Bahamas juu ya majanga hayo. Ingawa kuna ripoti ambayo imetolewa kuwa maeneo yaliyoathirika Bahamas yanakumbwa na changamoto ya umeme na shida ya mtandao.

 

04 September 2019, 16:06