Tafuta

Vatican News
Waandamanaji nchini Afrika ya Kusini kupinga ghasia dhidi ya ubaguzi ambapo Rais Ramaphosa ametoa ahadi ya kudhibiti hali hii,wakati huo huo maaskofu wa A.Kusini wanashutumu vikali matendo hayo Waandamanaji nchini Afrika ya Kusini kupinga ghasia dhidi ya ubaguzi ambapo Rais Ramaphosa ametoa ahadi ya kudhibiti hali hii,wakati huo huo maaskofu wa A.Kusini wanashutumu vikali matendo hayo  (ANSA)

AFRIKA KUSINI:ghasia dhidi ya wageni Afrika Kusini na Nigeria!

Maaskofu wa Afrika Kusini,wanashutumu vikali juu ya ghasia dhidi ya wageni nchini mwao.Kwa mujibu wa msemaji,Askofu Mkuu Buti Joseph Tlhagale na mhusika wa Ofisi ya Baraza la Maaskofu katika kitengo cha uhamiaji na wakimbizi anathibitisha kupokea habari mbaya za viongozi wake kutolinda waathirika.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican  

Inazidi kuongeza mivutano kati ya Nigeria na Afrika Kusini kufuatia na ghasia dhidi ya jumuiya ya Nigeria wanaoishi nchi za Afrika ya Kusini. Hata hivyo nchini Nigeria imetangaza kufunga ofisi zake za huduma ya kidiplomasia kwa muda, kwa sababu ya usalama katika utume wa o wa Kidiplomasia katika jijini Lagos na Abuja baada ya kufuatia ghasia dhidi makampuni huko  Afrika ya Kusini  kwa kushambuliwa duka la mgeni  huko Johannesburg.  Hivi karibuni kwa dhati nchini Afrika ya kusini kumetokea mfulizo wa ghasia za ubaguzi na kusababisha watu saba  kufariki dunia na zaidi ya watu 300 kuwekwa mbaloni na polisi katika siku mbili tu. Hata hivyo Viongozi wa Afrika ya kusini wanashutumiwa vikali, kwa sababu ya kutolinda jumuiya ya watu wageni katika nchi  yao na bila kutuliza hata kidogo matukio ya ghasia hizo.

Maaskofu washutumu vikali tendo la viongozi wa raia kutojali ghasia hizi

Maaskofu mahalia wanashutumu vikali kwa njia ya msemaji wao, Askofu Mkuu Buti Joseph Tlhagale, wa Jimbo kuu katoliki la Johanenesburg na mhusika wa kitengo cha  ofisi ya wahamiaji na wakimbizi cha Baraza la Maaskofu Afrika Kusini.  “Kwa mara nyingine tena anasema tunapokea taarifa kuwa viongozi wa madaraka wametenda kidogo sana kulinda waathirika” anasema Askofu Mkuu Tlhagale na kuongeza, wanadai kuwa si suala la ubaguzi bali ni suala la uhalifu, kama walivyo kuwa wamesema hapo. Lakini hii ni lazima kutafuta uwazi wake. Kwa maana hili si suala la raia wa Afrika ya kusini kuangaikia kuwafukuza wageni  katika miji yao kwa sababu ya madawa ya kulevya. Hii ni kazi ya wahalifu walio wachache. Huu ni ubaguzi wa kweli na rahisi, amesisitiza. Iwapo kazi hii ingekuwa inahusika kwa wale wahalifu, ni kwanini wasivamie maduka ya watu waafrika ya kusini? Ni swali anauliza Askofu Mkuu Tlhagale.

Sisi sote tu wamoja katika Yesu Kristo

Mafundisho ya Kanisa ni ya wazi na moja kwa moja bila kupinda. Zaidi ya asilimia 80% ya waafrika Kusini wanathibititisha kuwa ni wakristo, anakumbusha. Je viongozi wetu wa kidini wanafundisha nini kwa watu wote wanaojaza makanisa yetu kila Jumapili? Aidha ameongeza kusema: Mtakatifu Paulo kwa Wagalatia anasema “hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mume wala mke, na  kwa Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Yesu Kristo (Gal 3,28). Na kwa maana hiyo hakuna mwafrika ya kusini na wala Mnaigeria ,wala mwethiopia, kwa maana wote tumekuwa wamoja katika Yesu Kristo.Soma zaidi: http://sacbc.org.za/9008.

Na Umoja wa Mataifa unalaani ghasia dhidi ya wageni Afrika Kusini

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vitendo vya ghasia dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini vinavyoenda sambamba na mashumbulizi dhidi ya raia wa kigeni pamoja na uharibifu wa mali. Taarifa iliyotolewa tarehe 3 Septemba 2019 jijini New York, Marekani na msemaji wa Umoja wa Mataifa, imemnukuu Katibu Mkuu akitambua kauli ya Rais Cyril Ramaphosa ya kulaani vikali vitendo hivyo na wito wake wa kutaka kuimarisha uwajibikaji kwa mujibu wa maadili ya Afrika Kusini yaliyoainishwa kwenye katiba. Bwana Guterres aidha  ametoa wito kwa viongozi wote wa kisiasa kulaani na kukataa wazi wazi matumizi ya ghasia. Vyombo vya habari vinaripoti ya kwamba ghasia hizo zinazozidi kushamiri kila kuchao zimeshika kasi zaidi kwenye miji ya Pretoria na Johannesburg ambapo watu wapatao saba wameripotiwa kuuawa na huku  mamia kadhaa wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuhusika na fujo hizo. 

UBAGUZI A.KUSINI
07 September 2019, 15:09