Vatican News
Katika kilele cha mwezi wa kuenzi kazi ya uumbaji kuanzia Mosi Septemba hadi 4 Oktoba,Maaskofu wa Uingereza na Galles wameandika ujumbe wao kwa waamini ili kusasisha jitihada zao Katika kilele cha mwezi wa kuenzi kazi ya uumbaji kuanzia Mosi Septemba hadi 4 Oktoba,Maaskofu wa Uingereza na Galles wameandika ujumbe wao kwa waamini ili kusasisha jitihada zao 

Wito wa Maaskofu wa Uingereza katika kipindi cha kuenzi kazi ya Uumbaji,Mosi Septemba-4Oktoba!

Jitahada za Kanisa la Uingereza na Galles linaendelea katika kulinda nyumba yetu ya pamoja.Katika ujumbe wao uliotolewa kwa waaamini kufuatia na mtazamio wa mwezi wa kipindi cha kuenzi kazi ya Uumbaji,Maaskofu wanapyaisha mwaliko kwa waamini wote ili kujikita kwa kina na ari kukabiliana pamoja kipeo cha sasa cha ekolojia duniani na kusasisha jitihada zaidi kwa ajili ya ekolojia endelevu.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican Kubadili mtindo wetu wa maisha

Tasaufi ya ekolojia ya kikristo inaanza na maisha ya mtu binafsi na familia. Kanisa la Uingereza linasasisha jitihada kwa ajili ya kazi ya uumbaji na kuwaalika waamini wote wajitahidi kwa ari na mali na zaidi binafsi ili kuweza kukabiliana na dharura ya sasa ya mazingira na tabianchi. “Jitihada hizi zinaanza na mabadiliko ya mtindo wa namna ya kushi kwa kila mmoja, wanaandika maaskofu wa Uingereza na Galles katika ujumbe wao kwenye mtazamio wa Kipindi cha kazi ya Uumbaji ambacho kinajikita katika  sala na matendo ya kiekumene kwa ajili ya kulinda nyumba yetu ya pamoja. Hiki  ni kipindi ambacho kinatazamia kuanza tarehe Mosi Septemba hadi tarehe 4 Oktoba wakati wa kuadhimisha Sikukuu ya Mtakatifu Francisko wa Assisi, mdau wa kwanza katika kusifu kazi ya uumbaji wa Mungu, na kwa wimbo wake maarufu wa  “Laudato Si”. Katika ujumbe wao maaskofu wanaandika kwamba,“kwa matendo yetu tunaweza kuonesha kwa  pamoja uongozi wetu “ huku wakitaja ujumbe  wa Laudato si wa Baba Mtakatifu Francisko ambaye anaonesha dharura ya sasa ya kipeo cha mazingira na uharibifu wake na ambacho kimesababisha   na matumizi mabaya  ya mwanadamu kwa kuharibu uzuri wa kazi ya Mungu ambao aliuweka katika ardhi hii!

Makanisa na mashule  4 500 ya Wakatoliki Uingereza yanatumia nishati mbadala

Kulingana na wito huu wa kulinda nyumba yetu ya pamoja, ndipo mwaliko kwa waamini wote ili kujifunza juu ya mipango na mazingira iliyowekwa katika uwanja wa jumuiya katoliki  nchini Uingee  rza, Jumuiya ambayo ni kijani kibichi kila wakati. Kwa mujibu wa  muuzaji wa Biashara ya Gesi nchini Uingereza, makanisa zaidi ya 4,500 Katoliki na shule tayari zimebadilisha nishati mbadala, ambayo inafanya Kanisa Katoliki kuwa moja ya watumiaji  wakubwa na wenye vyeti vya kijani nchini humo. Hata hivyo pongezi pia kwa kituo cha mafuta cha majimbo (Inter-Diocesan Fuel Management (IFM), ambacho ni mtandao wa majimbo  unaosimamia usambazaji wa nishati ya majimbo  ya Uingereza, ambacho kimeungana kwa ujasiri kwa mwaliko wa Baba Mtakatifu  Francisko kuhamasisha  ubadilishaji kutoka nishati ya mkaa na kuingia  nishati safi ya kulinda nyumba yetu ya pamoja.

Tuzo ya “LiveSimply”, ni ya kuhamasisha ecolojia edelevu

Na ili kuwatia moyo wakatoliki waweze kubadilika katika mtindo wa maisha ya ekolojia endelevu, Kanisa la Uingereza hata limetoa tamko la kutoa tuzo  maalum, iitwayo “LiveSimply Award”. Tuzo hii imependekezwa na Cafod, yaani ni  shirika la maaskofu kwa ajili ya misaada katika Dunia ya Tatu. Tuzo hiyo wanapewa jumuiya hizo ambazo zinaonyesha kuishi kwa kiurahisi, kuwa na mshikamano na maskini na kwa njia endelevu na mazingira. Hadi sasa washindi ni 59 ambapo  parokia ni 50, shule 7, chuo kikuu na Shirika moja Katoliki, wakati parokia 120 na shule kwa sasa zimesajiliwa kama “LiveSimply”.

Kituo kipya cha Laudato Si’:jimbo la Salford

Katika matazamio ya kuhamasisha waamini kuhusiana na mada za kukabiliana na Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko, wa Laudato si, vilevile wameweza kuingiza tamko jingine la kuanzishwa kwa Kituo cha “Laudato Si” katika Jimbo la Salford. Anaye hamasisha  kituo hicho ni Askofu John Arnold mahalia na mhusika wa Kitengo cha mazingira katika Umbu la Baraza la Maaskofu Uingereza na Galles. Kadhalika yanafuatia mambo mengine ya kuanzishwa ambayo yalipendekezwa na Mjesuit wa kingereza ambaye mwaka jana alifungua kituo kingine  cha Laudato Si, katika Chuo Kikuu cha Oxford kwa lengo la kuhamasisha utafiti wa tasnifu (interdisciplinare) juu ya matatizo ya mazingira ambapo kama alivyosisitiza Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake kwamba, zipo athari nyingi za ekolojia, kijamii, kiteknolojia, kisiasa, kiuchumi, kifalsafa na kidini.

22 August 2019, 15:44