Kuhamasisha thamani ya Injili,kufutilia mbali kabisa kila mawazo potofu ya uandishi wa habari na kupambana na habari za kugushi ndiyo ilikuwa mada ya mkutano wa waandishi wa habari katoliki Kuala Lumpur nchini Malesia Kuhamasisha thamani ya Injili,kufutilia mbali kabisa kila mawazo potofu ya uandishi wa habari na kupambana na habari za kugushi ndiyo ilikuwa mada ya mkutano wa waandishi wa habari katoliki Kuala Lumpur nchini Malesia 

Waandishi wa habari katoliki barani Asia kwa pamoja kutangaza thamani ya Injili!

Uandishi wa amani katika utamaduni wa mitandaoni ndiyo ilikuwa tema ya mkutano ulioandaliwa na Signis ya Asia huko Kuala Lumpur nchini Malesia kwa ushiriki wa waandishi wa habari katoliki kutoka nchi 12 duniani.Kiini cha kazi hiyo imejikita kutazama kwa kina changamoto za mawasiliano katoliki katika kipindi cha mitandao ya kijamii na katika muktadha mgumu wa kijamii na kisiasa katika mabara yote.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Kuhamasisha thamani ya Injili, kufutilia mbali kabisa kila mawazo potofu ya uandishi wa habari na kupambana na habari za kugushi (fake news) ndiyo ilikuwa mada nyeti ya  mkutano wa waandishi wa habari katoliki uliomalizika hivi karibuni huko Kuala Lumpur nchini Malesia. Ni katika mkutano ulioandaliwa na Signis - Asia, kitengo cha bara la Asia cha Shirikisho la kimataifa Katoliki la uandishi ambacho kinaunganisha wahudumu na makundi yanayo jihusisha na mawasiliano ya kijamii na vyombo vya habari katoliki kutoka nchi 140 duniani kote. Katika mkutano huo aliundhuria Padre Paul Samasumo wa Vatican News ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa Signis ambaye amethibitisha kwamba,wanaandishi 18 katoliki walishiriki wakiwakilisha chini 12 za Asia na ili kutafakari kuhusu tema ya “uandishi wa amani katika utamaduni wa mitandaoni”.

Wasiwasi wa wakati ujao wa vyombo katoliki barani Asia

Katika mwendelezo wa mkutano wao, washiriki wameweza kushirikishana hali halisi ya utamaduni na siasa jamii katika nchi zao kwa ajili ya kuwahabarisha waandishi wenzao juu ya mantiki hizi. Ushirikishwaji wa wazo umefungua njia ya kuweza kuzungumzia changamoto zilizokabiliwa na waandishi katoliki katika huduma yao. Mkutano huo umezingatia baadhi ya wasiwawsi wa pamoja ambao kwa hakika inawahusu hata wasomaji katika mantiki ya vyombo vya habari kijamii, uwepo wa vizingiti vya mamlaka kisiasa, kipeo cha uchumi, ukosefu wa lazima wa utaalam na mafunzo kwa waandishi wa habari katoliki. Washiriki wa mkutano wamezungumzia hata umuhimu wa uwepo wa Kanisa katika mktadha kijamii na siasa ngumu mara nyingi inakuwa hata kizingiti.

Pasiwepo na hisia mbaya na habari za kughushi

Aidha katika hitimisho la mkutano wao,wameafikiana na kuthibitisha kwamba watendelea kutangaza habari njema kwa kuwa wote ni wabatizwa na wanaotumwa huku wakitupilia mbali kabisa na hisia mbaya za unandishi wa habari na taarifa za kugushi katika utuangazaji wao na pia kuwa na msimamo wa kujitahidi kuheshimu thamani ya kiinjili ambayo ni ukweli, uaminifu na uwazi katika shughuli yao  kama waandishi. Hata hivyo uthibitisho wao wa mwisho unaangazia  tema ya Mwezi maalum wa Kimisionari uliotishwa  na Baba Mtakatifu Francisko Mwezi Oktoba 2019 utakao ongozwa na kauli mbiu: “ Mmebatizwa na kutumwa: Kanisa la Kristo katika utume duniani”. Hii ina maana ya Kanisa kutaka kuendelea utume wake wa kutangaza na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu wa Kristo hadi pande zote za dunia. Kwa mujibu wa maelekezo ya Mwezi huo, ni  kutaka  kudumisha sala, katekesi, tafakari na matendo ya huruma kwa kila mbatizwa na anayemkiri Kristo Bwana.

Mapendekezo ya kuundwa kwa taasisi ya “Catholic Press Association-Asia”

Hatimaye katika mkutano wao, Signis ya Asia imependekeza kuunda kitengo cha mafunzo kwa ajili ya waandishi vijana. Jitihada zao ni kutaka kuhamasisha umoja na amani kati ya wanachama, pia kati ya wazalendo wa nchi hizo, kwa kukazia zaidi ushirikiano wa kiekumene na kidini. Mkutano aidha umependekea kuunda taasisi moja itakayoitwa  “ Catholic Press Association-ASIA” chini ya uongozi wa Signis ya barani  Asia kwa ushirikiano na kitengo cha Mawasiliano katika umbu la Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia.

WAANDISHI ASIA
21 August 2019, 14:05