Tafuta

Vatican News
Ni uzoefu mzuri sana wa Jumuiya ya kiekuemene ya Taize nchini Ufaransa kuunganisha vijana wengi wenye umri kuanzia 18-35 kukutana pamoja kwa sala na tafakari Ni uzoefu mzuri sana wa Jumuiya ya kiekuemene ya Taize nchini Ufaransa kuunganisha vijana wengi wenye umri kuanzia 18-35 kukutana pamoja kwa sala na tafakari  

TAIZE:Mkutano wa majadiliano na urafiki kati ya vijana wakristo na waislam!

Mwishoni mwa wiki hii Jumuiya ya kiekumene ya Taize huko Ufaransa inafanya mkutano wa vijana wakristo na waislam kutoka pande zote za dunia juu ya mazungumzo na urafiki kwa kujikita katika Hati ya Udugu kibinadamu,uliotiwa sahini mwezi Februari mwaka huu na Baba Mtakatifu Francisko pamoja na Imam Mkuu Ahmad Al-Tayyib wa Al-Azhar huko Abu Dhabi.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Siku tatu kwa ajili kudumisha urafiki kati ya waislam na wakristo kwa vijana kati ya miaka18 na 35 ambao wameanza mkutano kuanza tarehe 23-25 Agosti 2019 na ili kufikiria kwa pamoja juu ya Hati ya Udugu  wa Kibinadamu iliyotiwa sahini  huko Abu Dhabi kwa kuongozwa na mada ya makaribisho na juu ya uzoefu wa mazungumzao na urafiki ambao tayari upo. Ni vijana wengi wasichana kwa wavulana kutoka pande mbali mbali ya dunia wamefika katika jumuiya ya Kiekumene ya Taize nchini Ufaransa kuishi uzoefu huo wa nguvu ya sala na majadiliano kwa mwaliko wa Jumuiya hii ya sala ijulikanayo duniani kote.

Kutafakari ya Hati ya Udugu kibinadamu

Ijumaa asubuhi  23 Agosti vijana hao wamejikita katika tafakari ya pamoja kuhusu Hati juu ya udugu wa kibinadamu  kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja, ambayo ilitiwa shaini tarehe 4 Februari 2019 na Baba Mtakatifu Francisko na Imam Mkuu Ahmad Al-Tayyib wa  Al-Azhar huko  Abu Dhabi.  Hati hiyo imewakilishwa na Imam Mohamed-Soyir Bajrafil wa Paris Ufaransa na Padre mmoja wa Lione, Christian Delorme.Vijana wamealikwa baadaye kufanya majadiliano na kushirikishana juu yake. Hati ya Udugu wa Kibinadamu, kama isemavyo katika utangulizi wake ni tamko la nia njema na uhalisia wa utashi na ambapo ni kama vile kuwaalika watu wote ambao wanabeba ndani ya mioyo yao imani katika Mungu na imani katika udugu wa kibinadamu kuungana na kufanya kazi pamoja, ili iweze kuwa mwongozo kwa vizazi vipya kuelekea katika utamaduni wa kuheshimiana, katika heshima, katika kuelewa wa  neema kuu ya Mungu ambayo inawafanya wanadamu wote kuwa ndugu.

Tema ya ukarimu na majadiliano

Jumamosi 24 Agosti 2018 Watazungumza juu ya mada ya ukarimu na kwa mantiki hiyo mjadala utaongozwa na watu wa imani tofauti za kidini, kwa mfano Imam Mohamed Bachir Ould Sass na padre Christophe Roucou wa  Marsiglia. Hata hivyo majira ya mchana kwa siku mbili ya Ijumaa na Jumamosi,tafakari zitafanyika kwa njia ya semina na katika uzoefu tofauti wa majadiliano na urafiki ambao kama Jumuiya ya Taize tayari inaendelea kuishi barani Ulaya na katika sehemu mbalimbali za dunia kwa mfano uzoefu uliofanyika nchini Lebanon, Senegal na  Bangladesh.

Sala mbalimbali katoliki na za kiislam

Vijana waislam wataweza kusali kandoni kidogo, katika sehemu iliyoandaliwa kwa ajili yao, lakini hata hivyo  wote watakuwa na fursa za kushiriki sehemu ya sala na ndugu wa Jumuiya ya kiekuemene ya Taize ambayo mara nyingi imeandwa kwa nyimbo za tafakari na sehemu kubwa ni kutoka katika Biblia Takatifu. Na kila mmoja anaweza kuhisi uhuru wa kuimba au hapana kwa maana hawalazimishi. Na kwa wakristo pia kutakuwa na uwezekano wa kushiriki hata sala na waislam bila kizuizi chochote.

Wiki ya tafakari kwa vijana wa miaka 18-35

Kuhusiana na suala hili la tafakari, hata hivyo lengo la kuwaalika vijana wenye umri wa miaka 18-35  katika tafakari na jumuiya ya kiekumene ya Taize ni kuwawezesha  vijana wenye umri huo ili  kukutana na kujadiliana kati yao kuhusu wakati wao uliopo na endelevu katika mwanga wa imani. Kila siku baada ya sala ya asubuhi ni kuanza na utangulizi wa Biblia kwa ajili ya wote katika Kanisa.  Mpango mzima unaunganisha makundi ya majadiliano hasa katika masuala ya kiroho, kiuchumi, kisiasa, sanaa na kijamii. Washiriki wote wataalikwa hasa kushirki katika makundi mbalimbali ya matendo ya mshikamano, mashirika ya kimataifa, jumuiya ya kikristo vijana tofauti kutoka mabara yote, madada wa Mtakatifu Andrea na mafrateli wa Taize. Mambo mapya ya 2019 ni yale ya kufuata mpango maalum unaojikita katika masuala ya ekolojia.

23 August 2019, 15:00