Tafuta

Vatican News
Kwa mara nyingine tena nchini Nigeria,ameuwawa padre mwingine Davis Tankos,  wa jimbo la  Jalingo, serikali ya Taraba Mashariki ya Nigeria akiwa anakwenda kupatanisha makabila Kwa mara nyingine tena nchini Nigeria,ameuwawa padre mwingine Davis Tankos, wa jimbo la Jalingo, serikali ya Taraba Mashariki ya Nigeria akiwa anakwenda kupatanisha makabila 

NIGERIA:Siku ya sala kwa ajili ya amani na wakati huo,padre mwingine ameuwawa!

Katika siku ya kuombea Amani,wameshtushwa na habari za kuuwawa kwa padre mwingine wa Nigeria ambaye alikuwa anakwenda kufanya upatanishao kati ya makundi mawili ya makabila.Askofu wa jimbo anaondoa jukuma lolote kwa vikundi vyenye msimamo mkali.Katika fursa ya sala ya amani,Maaskofu wameandika ujumbe unaoongozwa na kauli:kuweni na nguvu,msiongope.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Baada ya mauaji ya mwisho ya padre, katika mikono ya kikundi cha Boko Haram, sasa ni Padre mwingine ambaye ameuwawa lakini jukumu hili limetokana na  makabila mawili ya kikristo, kwa maana hiyo ni mwathirika wa malumbano kati ya makabila. Padre Davis Tankos,  wa jimbo la  Jalingo katika serikali ya Taraba Mashariki ya Nigeria alikuwa ni paroko wa  Ahmadu,  ameuwawa na watu wasio julikana na ambao wamejaribu kutaka hata kuchoma mwili wake ndani ya gari lake. Padre Tankos alikuwa anajihusisha na shughuli ya upatanishaji kati ya makundi mawili ya kabila la TIv na Jukun, ambayo yote mawili ni ya kikristo wakiwa na idadi kubwa ya wakatoliki. Padre Tanko alikuwa anakwenda kukutana  nao kwa lengo kutafuta maridhiano kati yao. kwa mujibu wa  Askofu Charles Hammawa, wa Jimbo la Jalingo, anaondoa kabisa kila aina aina ya jukumu la  makundi ya Boko Haram. Na kwa maana hiyo amewaalika waamni wasifanye aina yoyote ya kulipiza visasi na kutangaza mazishi padre Tankos kufanyika siku ya Jumane ijayo tarehe 3 Septemba 2019.

Mwezi mmoja uliopita aliuwawa padre Clement Eziagu wa Jimbo Katoliki la Enugu

Mauaji hayo yamefika wakati ni mwezi mmoja tangu auwawe Padre Clement Eziagu wa Jimbo Katoliki la Enugu, mwathirika katika  jaribio la kutekwa nyara. Na kama ilivyo kwa raia wengi nchini Nigeria hata mapadre kwa mara nyingine tena wamekuwa ni  waathirika wa vitendo vya ukatili katika  vyanzo tofauti; na siyo wakati wote nia ni kupinga ukristo au, kwa hali yoyote, sio ya kupinga Ukristo tu.

Siku ya kuombea amani Nigeria

Maaskofu wa Jimbo la Katoliki la  Owerri lenye kuunganisha majimbo ya Aba, Ahiara, Okigwe, Orlu  na  Umuahia  nchini Nigeria wamandika barua, kufuatia na tukio la  Siku ya kuombea amani waliyoitangaza iwe tarehe 30 Agosti 2019. Katika barua yao maaskofu wanashutumu vikali hali mbaya iliyomo katika maeneo nchini humo kwamba  idadi ya watu wengi wapo kati ya mapigano mawili ya moto: kwanza kuondolewa kwa wanasiasa, wanajeshi na watekelezaji wa sheria, na kwa upande mwingine, vurugu na uvamizi wa wachungaji wa kifulani, majambazi wengine na wengineo wenye asili tofauti.

Kuweni na nguvu, msiogope na janga la ukosefu wa ajira kwa vijana

Aidha maaskofu kwa  ujumbe kupitia barua yao yenye kauli mbiu “ kuweni na nguvu msiogope”, wanasema kuwa watu wako katika vitisho visivyosemekana. Aidha wanaadika kuwa: “Kila siku, katika majimbo yetu yote, tunasikia hadithi zenye kusikitisha za utekaji nyara, ubakaji, ukeketaji, ujambazi, unyang'anyi wa ardhi, mauaji na uharibifu wa maisha ya watu. Tunaendelea kutumaini bure kuwa wahusika wa umma na mawakala  wa usalama watalinda raia wetu kama inavyokusudiwa na kupitishwa na Katiba”. Hali nyingine ya kutisha inayooneshwa na maaskofu katika barua yao ni “ukosefu wa fursa za ajira kwa vijana mbao wengi wao hujaribu kupata pesa za  haraka na bila hata kujiuliza, na hata kwa gharama ya maisha yao, badala ya kutafuta kazi za ubunifu,na zenye kuleta manufaa ya maisha yao”. Maaskofu kwa namna hiyo  wanawahimiza waamini kubaki imata katika imani na kuamini Mungu ambaye ndiye kisima cha nguvu, lakini pia wanatoa onyo kwamba hawapaswi kutumia vibaya mtazamo ulio wa wazi na wa kindani wa Wakristo au usichukuliwe kwa urahisi na kimchezo.

Serikali ilinde wazalendo la sivyo raia watachukua jukumu hilo 

“Serikali ya Nigeria na viongozi wake wanapaswa kuchukua jukumu la lazima kwa mujibu wa Katiba ya nchi kulinda na kutetea kila mzalendao wa Nigeria, kuanzia moja kwa moja na imani yake na kidini au kabila". Wanaandika Maaskofu na kuongeza, "Bila kufanya hivyo, hakuna maana ya umoja kitaifa wa Nigeria ,na wala  umoja hausaidi. Mahali ambapo serikali inashindwa kulinda na kuwatetea watu wake, raia wake wanatalazimika kujilinda wenyewe", wanabainisha. Maskofu katika barua yao pia wanatoa ushauri kwa wakristo wote kusali na kubaki makini hasa katika kuhamasisha mtazamo wa kikristo kwa lengo la kupinga kila aina ya itikadi mbaya za chuki, ujambazi na vurugu. Na kwa njia hiyo tarehe 30 Agosti katika Jimbo kuu wanamefanya siku maalum ya sala kwa ajili kuombea amani Nigeria. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti hii: https://nigeriancatholicreporter.com/be-strong-fear-not/

30 August 2019, 16:30