Tafuta

Vatican News
Kumbuka kila wakati kuwa Mungu amekukabidhi kazi nzuri;yaani jukumu la kuwa mwandishi wa habari.Na kama watu waliobatizwa na kuwa na sifa ya kuwa wakatoliki,jitahidi  kuwa mtaalam katika fani yako Kumbuka kila wakati kuwa Mungu amekukabidhi kazi nzuri;yaani jukumu la kuwa mwandishi wa habari.Na kama watu waliobatizwa na kuwa na sifa ya kuwa wakatoliki,jitahidi kuwa mtaalam katika fani yako 

MALAWI:Waandishi katoliki wahimizwa kuwa mawakala wa ukweli!

Waandishi wa Habari Katoliki nchini Malawi wamehimizwa kila wakati kujitahidi kulinda nchi hasa kuwa na jukumu la kinabii na kutekeleza zaidi katika uwajibikaji wa utoaji wa habari za Kanisa na kijamii kwa ujumla nchini humo zenye ukweli bila kugushi!Mhusika wa Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Malawi amesema:Kumbuka kila wakati Mungu amekukabidhi kazi nzuri;yaani jukumu la kuwa mwandishi wa habari timiza vema taaluma yako.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tatu wa Mwaka (AGM) wa Chama cha Wanahabari katoliki (ACJ) huko Blantyre Malawi  mwishoni mwa wiki iliyopita, Askofu  anayehusika na  Mawasiliano ya Kijamii katika Baraza la Maaskofu  Malawi (ECM), amesisitiza kwamba uhuru wa kujieleza na waandishi wa habari ni muhimu kwa nchi. Askofu wa Jimbo la Mangochi amesema: “kumbuka kila wakati kuwa Mungu amekukabidhi kazi nzuri; yaani jukumu la kuwa mwandishi wa habari. Na kama watu waliobatizwa na kuwa na sifa ya kuwa wakatoliki, jitahidi kila wakati kuwa mtaalamu katika kazi yako”.  Aidha ameongeza kusema:“Kanisa linategemea  kazi yako kuripoti bila kuchoka juu ya kazi za kijamii na za kiroho zinazofanyika nchini Malawi”,. kwa kuweka msisitizo zaidi amenukuu maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II ambaye alisema, “Kanisa liko upande wako, uwe wewe ni Mkristo au la, kila wakati jaribu kutafuta katika Kanisa heshima na utambuzi wa uhuru wa waandishi wa habari”.

Jukumu lako ni kumpambana dhidi ya maneno ya chuki na taarifa za kughushi

Askofu Stima akiendelea na mafundisho yake kwa waandishi wa habari katoliki amesisitiza kwamba: “Jukumu lako ni kupambana dhidi ya maneno ya chuki  na habari za kugushi ( fake news). Badala yake, unapaswa kuripoti juu ya shida za wakimbizi wanaostahili, yatima, wahitaji na kuwa upande wa watu hawa zaidi kwa maana ya wao ni thamani ya maadili ya kanisa Katoliki na zaidi ya yote, kuwa mtaalamu katika kazi yako”.

Pongezi kwa umoja wa chama cha waandikishi katoliki Malawi

Kwa upande wake, kiongozi mpya wa Tume  ya Utendaji Kitaifa (NEC), Rais wa ACJ, George Kasakula amewapongeza waandishi wote wa habari Katoliki nchini Malawi kwa umoja ambao umeona Chama chao kikiendelea kukua na kufikia mahali kilipo sasa. Hata hivyo pia aliongeza kusema kuwa uongozi mpya unataka kuifanya ACJ iwe nzuri zaidi na ya kwanza katika kuhamasisha na kuendeleza harakati za kusajiri ili kuongeza wanachama wake kitaifa. Amesema :"Tunataka kila mwanahabari Katoliki awe mwanachama wa Chama hiki. Tunataka Mafundisho Jamii Katoliki yatekelezwe kwenye kazi yetu na kutufanya tuwe wazuri, hadi  Mungu aogope waandishi wa habari”.

23 August 2019, 15:19