Kuhamasisha utume wa kimisionari wa Kanisa nchini Malawi ndiyo ilikuwa mada ya Mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Kipapa cha matendo ya Kimisionari (Pom)  hivi karibuni kwa siku tatu ya mafunzo kitaifa kwa viongozi wa Utoto mtakatifu kimisionari Kuhamasisha utume wa kimisionari wa Kanisa nchini Malawi ndiyo ilikuwa mada ya Mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Kipapa cha matendo ya Kimisionari (Pom) hivi karibuni kwa siku tatu ya mafunzo kitaifa kwa viongozi wa Utoto mtakatifu kimisionari 

MALAWI:POM yawataka viongozi wa Utoto mtakatifu wapyaishe jitihada za kimisionari!

Kuhamasisha utume wa kimisionari wa Kanisa nchini Malawi ndiyo ilikuwa mada ya Mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Kipapa cha matendo ya Kimisionari (Pom) hivi karibuni kwa siku tatu kitaifa kwa viongozi wa Utoto mtakatifu kimisionari.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican News

Kuhamasisha utume wa kimisionari wa Kanisa nchini Malawi ndiyo ilikuwa mada ya Mafunzo yaliyoandaliwa na Chama cha Kipapa cha matendo ya Kimisionari (Pom) hivi karibuni kwa siku tatu ya mafunzo kitaifa kwa viongozi wote wa Utoto mtakatifu kimisionari. Katika siku hizo wamepata fursa ya kutafakari juu ya imani yao ili iwawezeshe kuwasindikiza na kuwaongoza watoto katika safari yao ya maisha!

Enendeni kutangaza Injili

Kozi ya mafunzo imefanyika katika Sekondari ya wasichana ya Jimbo Kuu la Lilongwe Malawi, ambayo ilizinduliwa na Mkurugenzi wa Kitaifa wa POM, padre Vincent Mwakhwawa, na ambaye aliweza kutoa mafunzo yake na kuwatia moyo viongozi hao kwa shughuli yao ya kusindikiza utoto mtakatifu. “Mungu anashirikishana na sisi utume wake kwa sababu anataka kushikisha na sisi utukufu wake, kwa maana hiyo aliwaamuru mitume wake kama ninyi waendelee kutangaza Injili duniani kote. Kama viongozi wa watoto, kwa namna ya pekee mmepokea amri hiyo ya kuweza kushirikishana na utoto ile imani katoliki na thamani za kibinadamu” alisema Padea Mwakhwawa.

Katika mwaka 2020, Kongamano la kwanza la kimisionari kitaifa kwa ajili ya watoto

Katika ya tema za tafakari wakati wa mafunzo yao ilikuwa pia ni kuhusu suala la maandalizi ya Kongamano la kwanza la kimisionari kitaifa kwa ajili ya Utoto Mtakatifu  nchini Malawi. Ni Kongamano linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 12 -17 Agosti 2020 huko Lilongwe. Katika kongamano hili wanatazamia kushiriki watoto 1500 kutoka katika majimbo yote katoliki nchini Malawi. Kazi ya Kongamano hiyo itajumuisha kozi ya katekesi juu ya sala, ya sakramenti, tafakari kuhusu upendo na sadaka ya kimisionari, pamoja na mikutano meingine kuhusu utunzaji wa kazi ya uumbaji sambamba na Wosia wa Baba Mtakatifu Francisko wa Laudato Si kuhusu utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja.

23 August 2019, 15:55