Tafuta

Vatican News
Wanawake nchini Mexico tarehe 16 Agosti 2019 waliandamana kupinga kila aina zozote za manyanyaso ya kijinsia,muaji ya kila aina,ukosefu wa haki na usalama Wanawake nchini Mexico tarehe 16 Agosti 2019 waliandamana kupinga kila aina zozote za manyanyaso ya kijinsia,muaji ya kila aina,ukosefu wa haki na usalama 

Maaskofu wa Mexico wanatoa tahadhari ya kusitisha kutumia nguvu dhidi ya wanawake!

Kwa mujibu wa tamko la Askofu Mkuu Víctor Sánchez Espinosa wa Jimbo la Puebla anasema kuna tahadhari ya kusitisha kila aina yoyote ya matendo yanayoondolea hadhi ya wanawake nchini Mexico.Amesema hayo kufuatia na maandamano ya wanawake yaliyotokea katika mji wa Mexico hivi karibuni ya kupinga nyanyaso ya kijinsia.Watu wote wana haki ya kujielezea na kwa namna ya pekee wanawake wanahitaji usalama katika jamii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kuna tahadhari ya kusimamisha kila aina zote za matendo yanayoondolea hadhi ya wanawake nchini Mexico kwa mujibu wa tamko la Askofu Mkuu Víctor Sánchez Espinosa wa Jimbo Kuu katoliki la Puebla. Akizungumza katika Mkutano kwa ajili ya kutangaza mwaka wa 375 wa Seminari ya  Palafoxiano, Askofu Mkuu amethibitisha kuwa “maandamano ya hivi karibuni ya wanawake, ambayo yameambatana na vitendo vya uharibifu siyo njia bora ya kuelezea mzozo”, kwani “watu wote wana haki ya kujionyesha na kujielezea, katika kesi hii wanawake wanahitaji usalama mkubwa katika jamii”.

Wanawake hawawezi kuendelea kuwa waathirika wa kubakwa, mauaji, vurugu na uharifu mwingine

“Wanawake, Askofu Mkuu amesema, hawawezi kuendelea kuwa waathirika wa ubakwaji, mauaji, vurugu na uhalifu mwingine, kwa hivyo amewahimiza katika sekta zote za jamii kupambana na tatizo kwa sababu  anathibitisha kwamba maisha ni matakatifu na lazima yalindwe. “Ninaomba kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na dhidi ya wanadamu wote visimamishwe”. Hata hivyo Tema ya kutumia nguvu dhidi ya wanawake inaendelea kuwaka moto katika nchi hiyo kama ilivyo hata mahali pengine duniani. Maandamamo ya wanawake yaliyofanyika tarehe 16 Agosti 2019 katika mji wa Mexico, labda ilikuwa ni maandamano makubwa yaliyowahi kutokea nchini humu  dhidi ya kupinga  kutumia nguvu dhidi ya wanawake ambayo yaliandaliwa katika nchi hiyo.

Wanawake nchini Mexico walishuka barabarani wakiomba hadhi yao 

Kwa hakika wanawake nchini Mexico walishuka katika barabara na mitaa na katika  viwanja vyote huku wakiomba wahehimiwe na kupewa hadhi wakati huo wakiomba kusimamisha vitendo vya ngono na ukosefu wa usalama ambao umeleta madhara makumbwa kwa wanawake nchini Mexico. Hata hivyo kwa bahati mbaya,katika maandamano hayo vilietokea vitendo vibaya vya uharibifu ambavyo vilionekana katika nafasi zote za umma,kwenye stesheni za treni, mabasi au miguu katika jiji la Mexico! Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Mexico wanaofuatilia tema hii ya ukatili dhidi ya wanawake, huku  wazingatia idadi ya kesi za unyanyasaji wa kila aina, unyanyasaji  wa kijinsia na mauaji, nchini Mexico umekuwa ni  mojawapo ya suala la hatari sana katika nchi za  Amerika Kusini kwa usalama wa wanawake. Taarifa zinaonesha kwamba ni karibu wanawake watatu wanauawawa kwa siku na zaidi kuongezea karibu wanawake 49 wanaonyanyaswa kijinsia, hivyo kusababisha hali ya tahadhari kwa idadi ya watu walio athirika, kwa mujibu wa maelezo yaliyotumwa katika chombo vya habari za kimisionari Fides.

Tangu mwanzo wa mwaka vifo vimefikia rekodi mbaya

Kwa mujibu wa data zilizotolewa na vyombo vya habari vya Mexico, katika miezi sita ya kwanza ya mwaka huu, vifo vimefikia rekodi ya wanawake 470, kati yao 111 wameuawa na bunduki, 99 na zana ya kisu cha kukata, 261 na aina nyingine ya kifaa. Miongoni mwa kesi zilizoripotiwa, kuna uhalifu wa kijinsia: takwimu zinafikia kesi 1,530 za unyanyasaji wa kijinsia zilizoripotiwa katika mwezi mmoja, na wastani wa takwimu za wanawake 51 walioshambuliwa kingono kila siku, bila kuzingatia wale waathirika ambao ambao hawajaripoti au wale wote ambao wanakaa kimya kwa kuogopa kulipizwa kisasi. Kama inavyoripotiwa kwa Fides, maaskofu wengine wawili, Benjamín Castillo Plascencia wa jimbo Katoliki la  Celaya, na Askofu  Enrique Díaz Díaz, wa Irapuato, walielezea hadharani wasiwasi wao kwa kutangaza pia wazi juu ya  hatua za kukomesha kutumia nguvu dhidi ya wanawake kwa sababu wako katika jamii ya Mexico!

22 August 2019, 15:05