Tafuta

Vatican News
Maandalizi moto moto ya kumpokea Baba Mtakatifu katika kisiwa cha Madagascar Maandalizi moto moto ya kumpokea Baba Mtakatifu katika kisiwa cha Madagascar 

Bado siku chache Papa Francisko atembelee kisiwa cha Madagascar

Kati ya nchi masikini duniani,Kisiwa cha Madagascar kinakaribisha idadi kubwa ya watawa wengi wanaojikita katika shughuli mbalimbali za kitume.Kati ya hawa ni wale wa Chama cha kitume cha wamisionari wa Padre Charles De Foucauld,tangu mwaka 1962.Chama hiki kilianzishwa na padre Andrea Gasperino wa Cuneo Italia na kwa sasa kimeenea sehemu nyingine zaidi Afrika,Brazil Asia, Ulaya Mashariki

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni katika Wiki ya kufunga kijumuiya, ambayo ni uzoefu wa sala ya kimya na kushirikishana Injili kila mwaka ambapo watu wengi hukusanyika katika mji utwao wa  Vijana huko Cuneo katika moyo wa Chama cha Kitume cha Charles de Foucauld ambapo ni maelfu ya watu hasa ushiriki wa vijana wengi. Katika wingi huo mwandishi wa Vatican News alikutana watawa watatu wanaofahamu Madagascar vizuri na mmoja ni Sr. Lucia akiwa ameadhimisha hivi karibuni miaka  60 ya maisha ya kitawa aliyekuwa na macho ya kimcheza cheza sana kwa furaha hasa ya kukumbuka miaka 25 ya utume wake alioufanya kisiwani Madagascar. 

Watu wa Madagascar ni wakarimu wanamsubiri Papa kwa hamu

Sr. Lucia katika mahojiano amethibitisha juu ya kutambua vema kipindi hiki cha watu kumsubiri Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake ya kitume, ambapo amaesema kwa hakika itakuwa ni sikukuu kubwa!. Watu wa madagascar ni wakarimu na wenye moyo mzuri. Sr. Lucia anakumbuka alipokuwa huko akitoa huduma katika meza ya watoto wadogo, na  watoto walitokea kumpenda kwa namna ya pekee. Walikuwa wakimkumbatia kwa nguvu zote. Amesema kwamba walimfundisha mambo mengi na anahisi kupokea mengi sana kutoka kwao kuliko yeye aliyweza kutoa kwao. Hadi sasa amesema, kuhisi ile shauku ya kurudi katikati ya umati wa watu hao watakao kuwa wanampokea Baba Mtakatifu kisiwani Madagascar.

Lala ni sista kutoka Madagascar, anatoa ushuhuda wa watu wake rahisi

Naye  Sr. Lala ni kijana  mtawa kutoka Madagascar, ambaye anajivunia nchi yake pia . Yeye ni mmoja wa idadi ya madada wa chama hicho cha kitume kilichoundwa na  padre Gasparino, lakini kwa sasa anaendelea kutoa huduma karibu na wamisionari wa Italia. Akielezea nchi yake anasema  “Kwa hakika katika umaskini wake, watu hawa tayari wana vinasaba na karama zao, yaani asili ya kushirikishana katika umasikini kwa upando. Anaelezea asili yake ni kutoka katika familia yenye rasilimali chache, lakini yenye kuwa na furaha ya kuishi maisha rahisi katika jumuiya nzima za vijijini. Na  matumaini yake kwamba ziara ta Baba Mtakatifu Francisko inaweza kuwapelekea watu wake matumaini, katika maisha ya kila siku na katika jitihada za kanisa. Hasa vijana na Kanisa lao huko Madagascar, kisiwa ambacho kwa dhati kimeundwa na vijana wanahitaji nguvu itokayo kwa Mungu tu amsema.

Maisha ya kutengwa, kufungwa na ukoma

Misheni  zao huko Madagascar zilizaliwa huko Anatihazo, moja ya vitongoji masikini zaidi katika mji mkuu. Hiyo ilikuwa miaka ya ukoloni wa Ufaransa. Kati ya wakazi katika  makazi duni, katika maeneo yanayokosa kila huduma muhimu na watoto wengi bila kwenda shule , ndipo kulizaliwa shuule ndogo ya watoto wadogo na kituo kidogo cha kutoa msaada wa chakula. Wamisionari hawa ni wenye mfano mwema kwani si kwamba wanaleta miundo mipya  lakini zaidi  ni zawadi ya sala ya pamoja, ya kuabudu, ya ukaribu katika roho ya urafiki. Waliendelea pia hata kufungua nyumba ya Betania katika mkondo wa nchi ya Msumbiji  kunako 2002, ili kushuhudia upendo wa Mungu unaoambatana  na ukuaji wa kibinadamu na kiroho kwa watoto na vijana wote.

27 August 2019, 14:07