Tafuta

Nchini Msumbiji wanamsubiri Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake tarehe 4-6 Septemba. Furaha ni kubwa japokuwa na matatizo mengi yanayoikabili nchi Nchini Msumbiji wanamsubiri Baba Mtakatifu Francisko katika ziara yake tarehe 4-6 Septemba. Furaha ni kubwa japokuwa na matatizo mengi yanayoikabili nchi 

Msumbiji inamsubiri Papa japokuwa na changamoto za elimu na afya

Jitihada za kimisionari katoliki ni kwa miaka mingi imekuwa na msimamo kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Tangu tarehe 4-6 Septemba Baba Mtakatifu Francisko anatembelea Msumbiji. Padre Ezio Bonomo wa Jumuiya ya Familia Takatifu anaongoza Chuo Kikuu cha Maxixe, km 500 kutoka mji Mmkuu anaelezea kwa nini ni muhimu kuwekeza juu ya madaktari na elimu bora kwa vijana.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kanisa nchini Msumbiji jana na leo, ndiyo tema iliyochanguliwa kuongoza Mkutano ulioandaliwa tarehe 21 Septemba 2019 huko  Maputo Msumbiji katika Taasisi ya mafunzo ya kijamii na uchumi. Ni fursa ya kuweza kutathimini  Mafundisho jamii ya Kanisa juu ya uhusiano kati ya Kanisa na tofauti za kidini. Ni karibu kidogo miaka 20 katika maeneo mawili ya Msumbiji, ulifunguliwa Utume wa Shirika la Familia Takatifu, lililoanzishwa huko Bergamo nchini Italia. Zaidi ya shughuli zinazozungukia parokia, ni uendeshaji wa shule za watoto wadogo 8 katika vijiji vya maeneo ya Maxixe, kituo cha vijana na Chuo Kikuu,mahali ambapo ni vijana 4500 kutoka miji na wilaya wanashiriki mafunzo hayo.

Kuwekeza juu ya mafunzo kwa vijana kwa ajili ya ukombozi wa nchi

Padre Ezio Bonomo wa Jumuiya ya Familia Takatifu anaongoza Chuo Kikuu cha Maxixe, km 500 kutoka mji mkuu ameeleza ni kwa nini  kuna  umuhimu wa kuwekeza juu ya  mafunzo ya madaktari na elimu bora kwa ajili ya vijana, kwamba “tunafikiri kuwa njia bora ya kusaidia watu ni kuwaelimisha. Na kama utajiri mkubwa wa Msumbiji,kama ilivyo Afrika kwa ujumla, sehemu kubwa ya vijana ni muhimu waweze kusoma na kuendelea katika shindano kwa ajili ya ngazi ya shule za juu. Aidha amsema ni Ni changamoto kubwa ambayo lakini imetoa matunda mema . Nchi msumbiji, asilimia 75 ya watu wengi wanao umri wa miaka 25 na wengi ni vijana. Kwa hakika sekali imekikita kuwekeza sana katika elimu ya ujumla, japokuwa amesema padre , sasa kuna changamoto ya ubora.

Hata hivyo amelezea juu ya uzoefu wa kubadilishana kwa makundi mbalimbali ya wanafunzi wanao kwenda katika vituo mbalimbali vya masomo kama vile vyo vikuu kwa mfano ametaja nchini Italia ya kwamba katika Chuo Kikuu cha Milano wanafunzi wamekwenda Afrika kufanya uzoefu, kushirikishana na vijana mahalia wa Afrika, mawazo yao na mipango yao ya uhamasishaji inahitajika. Na hii ni mpango wa kuchochea elimu ambao pia umezaa maisha ya  ukarimu nchini Italia kwa watoto wa Kiafrika amethibitisha.

Madaktari wachache kwa ajili ya dharura ya watu

Japokuwa kwa miaka hii kumekuwapo na msukumo wa ujenzi baada ya migogoro ya miaka mingi, bado kuna matatizo mengi. Hii inahusu vituo vya afya nchini Msumbiji kwani, nchi bado inaukosefu wa madaktari katika uhusiano na watu. Kwa mfano kuna madaktari watatu kwa kila watu 100,000. Ni suala lisilokubalika amesemaPadre Bonomo; je ni kwa nini upungufu huo? Jibu ni kwamba mara zote ni kutokana na uhaba wa elimu,na matokeo yake watu, bila madaktari, huamua kujiganaga wenyewe au kuwakimbilia waganga wa kienyeji na kusababisha madhara makubwa ya familia zao.

Wanaomsubiri papa siyo wakatoliki tu bali ni watu wote

Watu wengi nchini Msumbiji wanamsumbiri Baba Mtakatifu na siyo wakatoliki tu bali watu wote amesisitiza. Parokia zote zinaendelea na maandalizi. Vijana kwa miezi hii wanajiandaa hata kukusana fedha za lazima ili kuweza kupata  nauli ya kuwafikisha katika eneo la mbali mji mkuu kufanya kumkesha na Baba Mtakatifu Francisko . Kila siku Luninga za kitaifa zinatangaza habari kuhusu ziara ya Papa na utume wa ke. Kutokana na hilo ni wazi kwamba siyo wakristo tu bali watu wote. kwa hakika zipo chereko chereko nchini msumbiji kwa ajili ya ujio wa Baba Mtakatifu Franciko tarehe 4-6 Septemba 2019. Hwa wanamsubiri hasa kwa ajili ya kutiwa moyo katika imani yao na amani kwa ujumla ya nchi. Hawawezi kupoteza fursa hiyo ya katika kusikiliza ushauri kwa ajili ya matarajio ya nchi na ili Papa aweze kuwafungulia kwa ukurasa mpya wa mwelekeo na mtazamo katika utume wao, amesisitiza.

27 August 2019, 13:58