Rais Roch Marc Christian Kaboré wa Burkina Faso anasema kwamba watu wake hawataogopa kuendelea kupambania eneo lao hata kwa gharama ya maisha yao Rais Roch Marc Christian Kaboré wa Burkina Faso anasema kwamba watu wake hawataogopa kuendelea kupambania eneo lao hata kwa gharama ya maisha yao 

Burkina Faso:Maaskofu watoa tahadhari ya uwepo wa jaribio la uchochezi wa kidini!

Watu wa Burkina Faso wamekuwa imara daima katika mapambano ya muda mrefu dhidi ya magaidi,kwa mujibu wa Mkuu wa nchini,Roch Marc Christian Kaboré na kwamba hawataogopa kuendelea kupambania eneo lao hata kwa gharama ya maisha yao.Pia Rais wa Baraza la Maaskofu wa Burkina Faso na Niger ametoa tahadhari kwamba kuna jaribio la uchochezi wa kidini,kufuatia na shambulio la kigaidi nchini humo 19 Agosti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ukosefu wa msimamo nchini Burkina Faso unazidi kuleta wasiwasi mkubwa mahali ambapo tarehe 19 Agosti 2019 kumetokea shambulio la kigaidi na wanajeshi 24 kufariki dunia, wakati wengine 7  kujeruhiwa na  wenzao 5 hawajulikani walipo. Shambulio hili lilitokea mapema asubuhi mjini Koutougou, kaskazini ya nchi hiyo. Kwa mujibu wa Mkuu wa nchi hiyo , Roch Marc Christian Kaboré mara baada ya shambulio hilo amesema, “Watu wa Burkina Faso wamekuwa daima  imara katika mapambano ya muda mrefu dhidi ya magaidi na hawataogopa kamwe kupambania eneo lake, hata kwa gharama ya maisha yao.

Hatari ya uwepo wa wakristo katika nchi

Tangu mwanzo wa mwezi Agosti mwaka huu, Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Burkina Faso na Niger, Askofu Laurent Birfuoré Dabiré, wa jimbo la Dori alikuwa ametangaza kuhusu mauaji ya wakristo katika mikono ya  makundi ya kijihadi ambapo alithibitisha ni kwa jinsi gani magaidi hayo yamejiandaa vema kisilaha kama vile wanajeshi wa kitaifa na kusema kuwa, iwapo dunia inaendelea kutofanya lolote, matokeo yake yatakuwa ni kuondoa uwepo wa wakristo katika nchi hiyo.

Parokia mbili zimefungwa

Kwa mujibu wa Askofu Dabiré, makundi ya kijihadi yanafuata mkakati maalumu ili kuweka chini ya ulinzi au hata kuthibiti  maeneo ambayo daima ni mapana katika nchi. Hawa wameingia taratibu, taratibu ndani ya nchi na kuwashambulia wanajeshi, nyumba za raia na watu wake. Sasa maadui zao kwa sasa utafikiri ni wakristo”. Ninaamini kwamba wanatafuta kuzusha migogoro ya kidini”, amesema Askofu Dabiré. Aidha amesema  “ukosefu wa usalama unazidi kuongezeka na kulazimisha kupunguza shughuli zetu za kichungaji. Kwa sasa ni hatari kubwa kwenda katika maeneo fulani na nimelazimika kufunga maparokia mawili”. Amethibitisha Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Burkina Faso na Niger.

Takwimu za Kanisa katika nchi

Itakumbukwa kwamba Kanisa Katoliki linawakilisha moja ya  tano ya  milioni 16.5 ya wakazi wa Burkina Faso, ambapo serikali yake ilisaini mkataba wa makubaliano na Vatican kunako Julai 12, ikihakikisha hali ya kisheria ya Kanisa na jitihadaza za kushirikiana kwa ajili ya ustawi wa maadili, kiroho na vitu vya wanadamu na kwa  kuhamasisha ustawi wa pamoja. Sehemu za ibada za Kikristo, hasa kaskazini mwa nchi, zinazokaliwa zaidi na Waislamu, ndizo zilizokusudiwa na vikundi vya kijihad baada ya kufukuzwa rais Blaise Compaoré kunako mwezi Oktoba mwaka 2014. Na kunako mwezi  Juni,2019 maaskofu wa Burkina Faso na Niger walitamka kwamba “nchi zao kwa miaka  wamekuwa mawindo ya ugaidi”.

22 August 2019, 14:32