Tafuta

Vatican News
Biblia ya watoto inajulikana sana kwa michoro yake ya kuvutia ambayo tangu kuanzishwa mwaka 1979 imefikisha miaka 40.Imetafsiriwa hadi sasa kwa lugha 189. Biblia ya watoto inajulikana sana kwa michoro yake ya kuvutia ambayo tangu kuanzishwa mwaka 1979 imefikisha miaka 40.Imetafsiriwa hadi sasa kwa lugha 189. 

Biblia ya Watoto imefikisha miaka 40!

Shirika la Kipapa la Msaada wa Kanisa Hitaji linaadhimisha mwaka wa 40 wa Biblia ya Utoto ijulikanayo “Mungu anasema na watoto wake”. Wazo hili lilianzishwa na Padre Werenfried Van Straaten na kuwakilishwa kwa mara ya kwanza huko Puebla Mexico kunako mwaka 1979. Leo hii Biblia ya Utoto imetafsiriwa kwa lugha 189 duniani kote!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Nakala milioni 51 katika lugha 189 zimesambazwa katika mabara matano. Hii ni idadi kubwa na  maalum ya Biblia ya Utoto ijulikanayo “Mungu anazungumza na watoto wake”. Ilianzishwa miaka 40 iliyopita na Chama cha Kipapa cha Kanisa Hitaji (Acs). Ilikuwa mwezi Januair 1979, mwaka wa kimafatia wa utoto ambapo mwanzilishi wa Chama cha Kipapa cha Kanisa hitaji Padre Van Straaten, aliwakilishwa kwa mara ya kwanza Biblia ya Utoto katika Baraza Kuu la Maaskofu wa Marekani (Celam) huko Puebla nchini Mexico ambapo katika fursa ya Mkutano huo aliudhuria hata Mtakatifu Yohane Paulo II ikiwa katika  ziara yake ya kitume ya kwanza ya kimataifa.

Asili ya kuanzishwa kwake

Aliyehamasisha  saula hili alikuwa ni padre Lardo kama alivyo kuwa akijulikana. Alikuwa ni mmonaki kutoka Holand na ambaye aliaga dunia kunako 2003. Alianzisha suala hili mara baada ya kuona kuwa Kanisa mahalia mara nyingi halikuwa na uwezo wa zana za kuweza kutoa biblia kwa ajili ya watoto iliyoandikwa lugha yao asili, au wasingeweza hata kuitangaza katika Nchi ambazo Kanisa lilikuwa likiteswa. Na zaidi watoto wengi masikini walikuwa hawana uwezo wa kununua hata kitabu. Kutokana na sababu hizo ndipo akawa na ubunifu wa kutengeneza Biblia ya watoto. Yeye alikuwa akisema kuwa, “Watoto wanayo haja ya kujua jambo fulani la Utoto, kama vile sura ya Yesu ambaye anaweza kuishi katika mioyo yao”.

Mafanikio

Kuanzishwa wa suala hili mapema kulileta mafaniko makubwa kwani Maaskofu wa Amerika ya kusini wakiwa wameunganika huko Pueblo waliagiza mara moja nakala milioni 1,2 kwa lugha ya kisipanyola. Baadeye zilifuata nakala nyingine kwa lugha ya kingereza, kifaransa na kireno,na taratibu hata kuongezeka lugha nyingine za kikanda. Na mafanikio makubwa zaidi  yalitokana na wafadhili wengi ambao waliwezesha usambazaji wa bure wa nakala za  Biblia ya Utoto katika nchi masikini. Leo hii Biblia ya utoto imetangazwa katika lugha 189. Kati ya lugha hizi ni lugha ya Afar inayozunguzwa na karibia na watu milioni moja na nusu katika baadhi ya nchi kama vile Ethiopia, Eritrea na Gibuti, au Kizulu, lugha ya kibantu ambayo inazungumzwa na nchi za Afrika ya Kusini. Zaidi ya lugha zinazotumiwa na mapadre na makatekisita, lugha hizi utumika hata kwa ajili ya kuwasaidia watoto wajifunze kusona na kuandika, na kwa mtazamo wa baadhi ya makundi ya makabila ni kitabu kimojawapo cha lugha mama au asili. Kwa mfano kwa upande wa Afrika Biblia ya utoto “Mungu anazungumza na watoto wake” hii imetoa mchango mkubwa mno kwa wasio jua kusoma na kuandika.

Lugha rahisi kwa kipimo cha mtoto

Biblia ya utoto imegawanyika katika sura 99 zilizoandikwa kwa lugha rahisi sana kwa kipimo cha watoto na ndani yake kuna maandiko msingi ya Agano la Kale na Jipya. Katika toleo la sasa  la kiitaliano, Biblia hiyo imeandaliwa kwa uangalifu sana na Mtaalimungu wa Kijerumani aitwaye Eleonore Beck na sisita wa Kispanyola Miren-Sorne Gomez amabaye amechora michoro mizuri ya kuwakilisha  maneno ya Biblia.

20 August 2019, 15:53