BENIN:Upatanisho wa Kanisa unaendelea kati ya mzozo wa kisiasa nchini!
Na Sr Angela Rwezaula –Vatican News
Kanisa katoliki nchini Benin halijasita kamwe kuendelea na mchakato wa shughuli yake ya kichungaji ya kuwa kama daraja la upatanisho kati ya Serikali na nguvu za upinzani ili kutatua kipeo kigumu cha kisiasa hasa kilichotokea mara baada ya uchaguzi wa viongozi watalawala kunako tarehe 28 Aprili mwaka huu. Huo ndiyo uthibitisho kutoka katika ofisi ya habari ya Baraza la Maaskofu nchini humo wakikanusha juu ya habari zilizosambazwa na baadhi ta vyombo vya habari nchini humo ya kwamba Kanisa limejiondoa katika shughuli hiyo ya upatanisho.
Uchaguzi ulipingwa kutokana na kuondoa baadhi ya vyama vya kisiasa
Maaskofu walikuwa wametoa uwezekano wao wa kuingilia kati baada ya ghasia za upinzani dhidi ya matokeo ya kura ambayo yalikuwa yamewekwa kusimamiwa na washiriki wa vya viwili tu vilivyo kuwa karibu na Rais Patrice Talon, Chama cha maendeleo na kile cha umma. Kuondolewa kwa nguvu nyingine za kisiasa, zilizo amuliwa na Tume ya uchaguzi kitaifa (Cena), ilionesha msimamo wa kukataliwa kwa nguvu kwa wapiga kura, kama ishara ya maandamano. Ni asilimia 22.99 tu ya wapiga kura waliweza kwenda kupiga kura, ambayo ilikuwa ni ya chini kabisa katika historia ya uchaguzi nchini humo. Na tangu 1990, wapiga kura walikuwa hawajawahi kushuka kufikia chini ya asilimia 50%.
Mwezi mei ghasia zilishutumiwa na maaskofu
Mei Mosi na siku iliyofuata huko Cotonou vyama vingine vya nchi vilionyesha mapigano makali kati ya vyombo vya nguvu za serikali na mamia ya waandamanaji , tofauti ambao walikuwa wanamuunga mkono Rais mng’atuka Thomas Boni Yayi. Ghasia hizo kwa hakika Baraza la Maaskofu katoliki walikuwa wameshutumu vikali na kuwashauri wanasiasa waweza kufunganama kama uzi mzito wa majadiliano ya kweli katika kulinda amani ya kijamii, umoja wa kitaifa na dhamani ya maendeleo ya usawa na upatanishi wa nchi.
Jitihada za maskofu katika mchakato wa upatanisho kijamii nchini Benin
Katika taarifa iliyotolewa kwa siku hizi maaskofu wanathibitisha tena jitihada zao za ya kuendelea na kwao na mchakato wa kufanya kazi kwa ajili ya upatanisho na mshikamano wa kijamii huko Benin na wanakumbuka kuwa wamewashauri tena wakristo kusali na kutumaini wakati wa hija ya kitaifa ya kwenda katika madhabahu ya Dassa-Zoumé iliyomalizika Jumapili 18 Agosti 2019!