Tafuta

Vatican News
Tunapokaribia katika kilele cha Siku ya Kuombea kazi ya Uumbaji duniani tarehe 1 Septemba,ni miito mingi imeanza kutolewa na viongoz wa Kanisa juu ya kuheshimu na kulinda sayari yetu mama Tunapokaribia katika kilele cha Siku ya Kuombea kazi ya Uumbaji duniani tarehe 1 Septemba,ni miito mingi imeanza kutolewa na viongoz wa Kanisa juu ya kuheshimu na kulinda sayari yetu mama 

ARGENTINA:Wito wa maaskofu kwa ajili ya utunzaji wa kazi ya uumbaji!

Katika kuelekea kilele cha Siku ya Kuombea Kazi ya Uumbaji duniani ifikapo tarehe Mosi Septemba ijayo,Askofu Oscar Vicenta Ojea wa Argentina anatoa angalisho juu ya madhara yanayofanywa na mwanadamu katika kuharibu rasilimali tuliyo pewa na mwenyezi Mungu.Tunapaswa kukubaliana sisi sote na kuomba serikali na viongozi wa dunia ili wakae na kufikiri kile ambacho kinafanyika katika sayari hii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika kuelekea kilele cha Siku ya Kuombea viumbe duniani, tarehe Mosi Septemba ijayo, Askofu Oscar Vicente Ojea wa Jimbo la Mtakatifu Isidro nchini Argentina katika ujume wake amesema kwamba, Tumeacha kulinda kazi ya uumbaji na kunyonya rasilimali za madini, hata ukataji hovyo wa miti na wakati huu hata uchafuzi wa maji na kuendelea kuharibu ardhi yetu”. Hata hivyo amesema hayo katika ujumbe huo wakatu tunandelea kuona taarifa za kipeo cha moto unaounguza msitu wa amazonia, ambao unafikiriwa kama ni pafu la dunia ambalo sisi kama binadamu tunalitegemea.

Janga la ongezeko la joto duniani

Katika ujumbe wake  Askofu Ojae anaendelea kubainisha kwamba, Baba Mtakatifu Francisko amekuwa nabii wa kusema kuwa kwamba ni kwa haraka tunapaswa kukubaliana  sisi sote na kuomba serikali, viongozi wa dunia ili wakae na kufikiri kile  ambacho tunafanya katika sayari hii. Kwa maana hiyo anataja hata suala la kuongezeka kwa joto duniani, uchomaji wa moto  hovyo na kushauri kusikiliza kilio cha masikini na ardhi hii ambayo ndiyo kilio kimoja tu. Na katika hali halisi hii amesema, "ni ubinafsi mkubwa ambao hauwezi kufikiria".

Kutunza, kuheshimu na kulinda ardhi

Katika hitimisho la ujumbe wake katika maadhimisho ya siku hiyo, Askofu anaomba Bwana katika kipindi hiki nyeti cha maisha ya sayari yetu, ili Mungu azidi kutufundishwa kujali kutumia, kuheshimu na kulinda dada yetu, mama yetu ardhi ambaye kwa hakika anatakiwa kuheshimiwa, kutunzwa na kulindwa na kila binadamu anayeishi katika ardhi hii.

26 August 2019, 12:05