Vatican News
Washiriki wa Mkutano 18 wa Shirikisho la Maaskofu wa Afrika Mashariki na Madagascar (SECAM) wamehakikishiwa kuwa hakuna virus vya Ebola nchini Uganda Washiriki wa Mkutano 18 wa Shirikisho la Maaskofu wa Afrika Mashariki na Madagascar (SECAM) wamehakikishiwa kuwa hakuna virus vya Ebola nchini Uganda 

UGANDA:Washiriki wa SECAM wahakikishiwa hakuna Virus vya Ebola

Wizara ya Afya nchini Uganda imewakikishia washiriki wa Mkutano wa 18 wa SECAM kuwa hakuna virus vya Ebola nchini Uganda!Hayo ni maelezo kutoka katika barua uliyotumwa kwa Monsinyo Jonh Baptisti Kauta,Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Uganda (UEC) na Dk.Hnery G.Mwebesa Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Afya katika Wizara ya Afya nchini Uganda

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Tarehe 19 Julai 2019 Serikali ya Uganda imewahakikishia watakao shiriki Mkutano Mkuu wa 18 wa SECAM na maadhimisho ya Jubilei ya dhahabu kwamba, kwa sasa hakuna uthibitisho wa kesi za Virus vya Ebola. Hayo ni maelezo yaliyomo katika barua uliyotumwa kwa Monsinyo Jonh Baptist Kauta, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Uganda (UEC) na Dk. Hnery G. Mwebesa Mkurugenzi Mkuu wa Huduma ya Afya katika Wizara ya Afya Uganda, katika barua inayoonesha tarehe 11 Juni 2019  kuhusiana na suala la mlipuko wa Virus vya Ebola nchini humo, kwa upande wa Wilaya ya Kasese Kaskazini Magharibi mpakani mwa Uganda na Congo (DRC).

Kesi tatu zilijionesha mwanzoni mwa mwezi juni mpakani mwa Congo DRC

Katika barua hiyo inasema ni kesi tatu tu zilizo kuwa zimethibitisha kuwakumba  familia moja ambayo ilipokelewa huko wilaya ya Kasese wakiwa wanatokea Congo DRC, tarehe 10 Juni 2019. Na kwa bahati mbaya walifariki dunia kati ya tarehe 11 na 13 Juni 2019. Na tangu wakati huo hakuna kesi yoyote iliyo ripotiwa barua inathibitisha. Zaidi ya hayo, Dk. Mwembesa ameonesha kwamba kuwa, jumla ya watu 113 waliokuwa wameshukiwa kuwa na ugonjwa huo walitambuliwa na wanaendelea na chanjo dhidi ya Ebola. Kwa wote hao hakuna yoyote anayeonesha dalili za Ebola na 17 kati yao tayari wamekamilisha siku 21 za kufuatilia. “Kuna timu ya ufuatiliaji yenye nguvu kutoka Wizara ya Afya na vijiji vya Kasese vinavyofunika vijiji 89 vya wilaya ameandika na kwamba ufuatiliaji wa kawaida na kwa tukio hili unaendelea kufanyika. Wasafiri wote kwenda Uganda kutoka DRC wanashughulikiwa katika vituo vyote mpakani vya kutoka na kuingia”, amethibitisha Dk.Mwebesa.

Serikali ya Uganda inafuatilia hata katika maeneo ya Kampala

Serikali ya Uganda imewahakikishia washiriki wa Mkutano huo na maadhimisho kuwa hatari ya kuenea hata ndani ya Wilaya ya Kasese ambako kulizuka awali ni hatari ndogo, lakini mawasiliano na ufuatiliaji wa uangalifu unaendelea. “Hatari ya kuzuka na  kuenea mjini Kampala ambapo mkutano wa SECAM utafanyika ni vigumu sana kwa sababu nchini Uganda inabaki  na  tahadhali kubwa ya kuzuia kuenea, hasa kufuatia na mapigano yanayoendelea kati ya makabila ya Lendu na Hema katika Mashariki mwa DRC, eneo ambalo ni kiini cha kuzuka kwa Ebola nchini DRC, “ amesema Dk. Mwebesa.

Wasafiri wote wanatakiwa wawe na chanjo ya homa ya manjano

Wakati huo huo Wizara ya Afya ya Uganda inawataka  wasafiri wote wanaofika kutoka nchi au maeneo yaliyo na  hatari ya maambukizi ya homa ya manjano kuwa wanapaswa kuonesha cheti cha chanjo ya homa ya manjano. Na nchi zilizo hatari ya maambukizi ya homa ya manjano kama ilivyo kwa miongozo ya Kimataifa ya Usafiri na Afya, ikiwa ni pamoja  barani Afrika: Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Kongo, Ivory Coast, Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Guinea ya Ikweta, Ethiopia, Gabon, Gambia, Ghana, Guinea, Guinea, Bissau, Kenya, Liberia, Mali, Mauritania,   Niger, Nigeria, Senegal, Sierra Leone, Sudan, Sudan Kusini, Togo na Uganda; Nchi zilizo ns hatari katika bara la Amerika ya Kusini ni pamoja na Argentina, Bolovaria, Venezuela, Brazili, Colombia, Ecuador, Guyana ya Kifaransa, Guyana, Panama, Paraguay, Peru, Bolivia, Surinam na Trinidad na Tobago.

Jubilei ya dhahabu ya SECAM

Kuhusiana na Jubilei ya dhahabu ya  Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Madagascar (SECAM) inafanyika mjini Kampala Uganda ambapo imefunguliwa kwa  mkutano wake wa 18 kuanzia tarehe 20 Julai 2019  ambapo wajumbe zaidi 400 wanashiriki kutoka ndani  na nje ya bara la Afrika hadi tarehe 28 Julai. Kauli mbiu ya Mkutano huo na Jubilei ya miaka 50  ni  “Kanisa, familia ya Mungu Barani Afrika;Sherehekea Jubilei yako! Mtangaze Kristo Yesu Mkombozi wako”.

 

20 July 2019, 15:36