Katibu Mkuu wa AMECEA anatoa shukrani kubwa kwa niaba ya Rais wake na maaskofu wote wa Kanda kwa msaada,ushirikiano na mshikamano wa Baraza la Maaskofu Amerika USCCB Katibu Mkuu wa AMECEA anatoa shukrani kubwa kwa niaba ya Rais wake na maaskofu wote wa Kanda kwa msaada,ushirikiano na mshikamano wa Baraza la Maaskofu Amerika USCCB 

AMECEA inatoa Shukrani kwa USCCB kuendeleza msaada na mshikamano!

Katibu Mkuu wa AMECEA Padre Anthony Makunde ametoa shukrani kubwa kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani(USCCB)kwa ajili ya ushirikiano,mshikamano na usadizi ili kwamba Kanda za AMECEA ziweze kuendelea kupokea msaada kupitia Kamati ndogo ya Baraza la Maaskofu wa Marekani (USCCB) kwa ajili ya Afrika

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Katibu Mkuu wa AMECEA Padre Anthony Makunde ametoa shukrani kubwa kwa Baraza la Maaskofu Katoliki Marekani (USCCB) kwa ajili ya ushirikiano, mshikamano na kusaidia ili kwamba Kanda za AMECEA ziweze kuendelea kupokea msaada kupitia Kamati ndogo ya Baraza la Maaskofu wa Marekani (USCCB) kwa ajili ya Afrika. Ameelezea hisia zake wakati wa Mkutano wa wajumbe wote wa Sekretarieti ya AMECEA wakiwa pamoja na Bwana Fritz Zuger kutoka Baraza la maaskofu wa Marekani (USCCB ambaye kwa sasa anatembelea Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki. “Kwa niaba ya Rais wa AMECEA na Wajumbe wote ninatoa shukurani kwa dhati kwa Maaskofu wote wa Amerika na jumuiya nzima ya wakatoliki kwa jitihada zao Za kuwashika mkono kaka na dada barani  Afrika ili Kanisa liweze kuendelea” amesema. Aidha Padre Makunde amemweleza Bwana Zuger kwamba, “Ulaya na Marekani pamoja na Canada zimeinjilisha bara la Afrika na wameendelea kutoa msaada kwa Afrika katika roho ya ushirikiano, mshikamano na kushiriikishana uzoefu wa imani kichungaji na kiutumaduni”.

Uhusiano wa kitume hauna maana ya kufuatilia utekelezaji wa mipango tu

Na zaidi Padre Makunde amesema kwamba, uhusiano kati ya Kanisa katika utume na Kanisa barani Ulaya na Amerika, havina maana ya kuwa na uhusiano wa  mipango tu. “ziara ya Bwana  Fritz Zuger kuitembelea Skretarieti ya AMECEA, Baraza la Maaskofu Kenya (KCCB) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TECC) na wengine si tu kuhusu kufuatilia utekelezaji wa miradi, lakini pia ni kuimarisha roho ya ushirikiano, muungano na mshikamano  kati ya Maaskofu wa Afrika na Maaskofu wote wa Marekani (USCCB)”. “Matokeo ya ushirikiano na uhusiano  kidugu tuliyo nayo ni dhahiri kabisa. Kwa niaba ya Kanda zote za AMECEA, ninakuomba uwafikishie shukrani zetu  Maaskofu wa Marekani na wale wanaofanya kazi katika kamati maalum kwa ajili ya Afrika”, amesema Padre Makunde. Aidha ameongeza kusema, “ aidha tunashukuru kwa uwepo wa Kardinali Joseph William wa Jimbo Kuu la  Tobin Newark, New Jersey ambaye aliungana nasi wakati wa Mkutano Mkuu wa 19 wa AMECEA huko Addis Abeba Ethiopia, mwezi Julai mwaka jana. Kuwepo kwake kati yetu ulikuwa ni ishara ya ushirikiano mkubwa, msaada na mshikamano kati ya Maaskofu wa Marekani na wale wa Kanda za AMECEA.”

Ni muhimu kuwa na mahusiano na kila mmoja 

Na kwa upande wake, Bwana Fritz Zuger ameonesha kuwa tendo la kufanya kazi katika kamati ndogo kwa miaka kumi iliyopita, ameamini ya kwamba ushirikiano kati ya  Maaskofu wa Amerika (USCCB) na Maaskofu wa Afrika (AMECEA) ni ujenzi ulio mkubwa zaidi wa uhusiano na mpango wa kifedha inayotakiwa kufanyika ni mambo ambayo yanatokana na uhusiano huo. “Ni muhimu kuwa na mahusiano na kila mmoja wenu na kujenga uhusiano na  siyo kuhusu biashara na  siyo kuhusu miradi, na kuongeza kusema kuwa, zaidi ya asilimia 80% ya kazi yake ni kujenga uhusiano unaowezekana kufanya kazi pamoja.

20 July 2019, 15:25