Kardinali Charles Maung Bo,Askofu Mkuu wa Yangon na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia ameandika Ujumbe wa Pentekoste kwa maaskofu wa Asia Kardinali Charles Maung Bo,Askofu Mkuu wa Yangon na Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu barani Asia ameandika Ujumbe wa Pentekoste kwa maaskofu wa Asia 

Ujumbe wa Pentekoste barani Asia:Kuwa na matumaini katika nyakati ngumu"

Pentekoste ya mwaka huu ni maalum kutokana na Papa Francisko kutoa mwaliko wa kuishi mwezi Oktoba 2019 kama Mwezi Maalum wa Kimisionari.Katika Siku ya Pentekoste 2019 tuombe kwa ajili ya uongofu wa kweli wa kimisionari wa Kanisa.Ni sehemu ya ujumbe wa Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Barani Asia,Kardinali Charles Maung Bo na kusisitiza kuwa Roho Mtakatifu ni kisima cha maisha ya utume.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kardinali Charles Maung Bo, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya maaskofu wa Asia (Fabs) katika fursa ya Siku Kuu ya Pentekoste ametuma ujumbe wake kwa maaskofu wote wa Bara la Asia kuwa, katika Siku ya Pentekoste 2019 tuombe kwa ajili ya uongofu wa kweli wa kimisionari wa Kanisa! Pentekoste ya mwaka huu ni maalum kutokana na Papa Francisko kutoa mwaliko wa kuishi mwezi Oktoba 2019 kama Mwezi Maalum wa Kimisionari. Kardinali Bo pia anakumbusha ziara ya Mtakatifu Yohane Paulo II nchini India kunako 1999, na kwamba alipokwenda New Delhi alitangaza Wosia wake wa Kitume wa “Kanisa la Asia”, ikiwa ni tunda la jitihada za Mkutano maalum wa Sinodi ya Maaskofu kwa ajili ya Asia uliokuwa umefanyika Mjini Vatican mwaka 1998.

Matumaini katika nyakati ngumu

Katika ujumbe wa Kardinali Bo unataja Injili ya Yohane (Yh 1, 5): “Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza”, kwamba maneno haya ya matumaini ni kwa ajili ya nyakati zetu ngumu. Hata hivyo anaongeza kusema kuwa, maneno ya uhakika yaliyoandikwa na Mwinjili Yohane kuwa: “wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu” (Yh 1,12) yanawatia moyo wahudumu wa shamba la Injili katika bara la Asia, ikiwa na maana  ya wale wote wanao endelea kueneza Habari Njema katika mioyo ya watu wa Asia, licha matatizo kama vile ya mateso, ukosefu wa uvumilivu na itikadi mbaya za kidini

Kuinjilisha siyo kuuza bidhaa ni kutangaza Mungu na upendo wake

Kardinali Bo, anakumbusha kwa maaskofu wa Asia kwamba, kuinjilisha haina maana ya kuuza bidhaa. Hii ni kutokana na kwamb  tayari wana maisha ya kuweza kutangaza Mungu na maisha ya Mungu, juu ya upendo  wake wa huruma na utakatifu wake. Ni Roho Mtakatifu anayewatuma, anawasindikiza na kuwavuta. Ni yeye kisima cha maisha ya utume. Ni yeye ambaye anaongoza Kanisa kama alivyosema Baba Mtakatifu Francisko katika hotuba yake kwa wakurugenzi wa kitaifa wa shughuli za Matendo ya Kipapa ya Kitume kunako tarehe 1 Juni 2018. Na kwa kuhitimisha ujumbe wake anasema kwa njia ya sala yake ya kinyenyekevu anayoimba kwa  Roho Mtakatifu ili aweze kuwatawala kwa njia ya ushuhuda wao na ili waweze kuzaa matunda ya Habari njema.

Wajumbe wa Fabc

Shirikisho la Mabaraza la Maaskofu Asia (Fabc) linaunganishwa na Mabaraza ya maaskofu 26 ya nchi. Inayo unganishwa na  mabaraza ya maaskofu 19 wa Asia kama wajumbe kweli, pia  wajumbe 8 wengine kutoka mashirika. Lengo la Shirikisho hilo ni kuhamasisha mshikamano na uwajibikaji kati ya wajumbe wake kwa ajili ya ustawi wa Kanisa na jamii nzima barani Asia.

11 June 2019, 14:56