Mkataba wa Kharthoum  usibaki katika karatasi tu bila bila kufanyiwa matendo ya dhati maana watu wanaendelea kufa kutokana na vikosi vya wanamgambo wa kutumia silaha Mkataba wa Kharthoum usibaki katika karatasi tu bila bila kufanyiwa matendo ya dhati maana watu wanaendelea kufa kutokana na vikosi vya wanamgambo wa kutumia silaha 

Maaskofu Afrika ya Kati wanasema:inatosha basi kutumia silaha na kuzuia amani!

Baada ya mkutano wa mwaka uliomalizika hivi karibuni huko Bossangoa maaskofu wa Afrika ya Kati wametoa ujumbe mpya unaohusu umoja na mapatano,huku wakinyoshea kidole dhidi ya hali halisi ya kutisha ya wanamgambo wa kutumia silaha ambao wanaendelea kuwa kizingiti kigumu cha mchakato wa amani ya nchi.

Na Sr. Angela Rwezaula –Vatican

Maaskofu wa Afrika ya Kati wanatoa onyo kali katika ujumbe wao wa mwisho mara baada ya Mkutano wao mwaka uliofanyika kuanzia tarehe 17-24 Juni 2019 huko Bossangoa hasa wakitazama suala la hali halisi ya jamii-kisiasa  na wakiomba warudishiwe madaraka ya Serikali ya eneo lote la  taifa. Maaskofu katika ujumbe wao wanasema kuwa  watu wamechoka na unafiki wa kuweka sahini katika mikataba mbalimbali  ya nchi, wakati huo huo mikataba hiyo inakiukwa na kubaki bila utekelezwaji!

Wanamgambo wenye silaha wanazuia amani

Ni muda mfupi tu tangu kutiwa sahini mkataba wa Kharthoum mwezi Februari 2019 na  ikiwa ni sahini ya nane tangu mgomgoro uanze kunako 2013 na baada ya kujikabidhi Rais François Bozizé, lakini mchakato wa amani ni wa taratibu na mdhaifu. Wanao sababisha udhaifu huo ni wanamgambo wa kutumia silaha ambao wanaendelea kusumbua na kuhatarisha usalama wa raia.

Kufuatilia wahusika wa mauaji

Kati ya mafunzo ya hivi karibuni ya chama cha Requins cha Afrika ya Kati (yaani chama cha nyangumi wa Afrika ya Kati) kilichoundwa mwezi Januari mwaka huu, kipo karibu na Faustin-Archange Touadéra, ili kupingana na Chama cha Ulinzi wa Kitaifa na Zingo Bian ambaye anakusanya mambo kadhaa ya upinzani. Hata hivyo ni chama hicho cha  Réquins kinacholengwa ujumbe wa maaskofu na kushutumu vikali hatari iliyotangazwa tarehe 20 Juni na wanamgambo wapya ambao wanaotaka kuchukua ardhi ya Mtakatifu Jacques de Kpèténè, sehemu ambayo imegeuka kuwa uwanja wa operesheni za umwagaji damu.

Kusoma historia ya nchi ya Afrika ya kati inaonesha mfungamo wa vikundi vya kisilaha

Maaskofu wa Afrika ya Kati wanaandika kwamba, katika kusoma historia ya nchi yao, wanagundua kuwa kila utawala wa kisiasa utafikiri unafungamana na wanamgambo wa kutumia silaha kwa sababu wanataja vikosi hivyo kama vile ‘Les Abeilles’, ‘Les Karako’, ‘Les Balawa’, ‘Les Libérateurs’, ‘Les Séléka’, ‘Les Antibalaka’. Katika mantiki hiyo ukosefu wa haki na mateso, ni kwamba Kanisa linapaswa kuwa ishara na chombo cha umoja kwa ajili ya kujenga madaraja ambayo yamevunjwa wanasema maaskofu. Lakini huo  ni umoja ambao unasimika msingi wake katika Injili. Wakati wakiadhimisha miaka 125  ya unjilishaji wa Afrika ya Kati, kwa njia ya wamisionari wa kwanza, Injili bado inabaki kuwa Neno la ukumbozi kwa walioelemewa, kwa maana hiyo wanashauri watu warudi katuka haki na zawadi ya amani ya Kristo.

Wito kwa wahusika wote na kwa kila mmoja

Kwa kuhitimisha ujumbe wao, maaskofu wanatoa angalisho kwa kila mmoja ili kuhakikisha utoaji wa mchango katika kujenga na kubaki na maelewano ya kijamii yaliyo haribiwa na migogoro ya mauaji na  ambayo bado yanaendelea kuyumbisha nchi. Maaskofu kwa namna ya pekee wanaelekeza ujumbe wao kwa Serikali, makundi ya kisilaha na raia wote ili wajitahidi hasa kulingana na mkataba wa Kharthoum ili usibaki katika karatasi tu bila bila kufanyiwa matendo ya dhati.

26 June 2019, 15:05