Tafuta

Kardinali Andrea Yeom Soo-jung wakati wa maadhimisho ya misa ya maombi kwa ajili ya Amani ya Peninsula ya Korea amesema huduma ya sala ni muhimu kwa lengo la amani ya kweli Kardinali Andrea Yeom Soo-jung wakati wa maadhimisho ya misa ya maombi kwa ajili ya Amani ya Peninsula ya Korea amesema huduma ya sala ni muhimu kwa lengo la amani ya kweli 

Korea Kusini:Maelfu ya wakatoliki waungana katika sala kwa

Jimbo katoliki la Seoul nchini Korea Kusini limefanya Siku ya sala kwa ajili ya upatanisho na Korea kusini kwa sababu ya kumbukumbu tangu kuzuka kwa vita kati ya nchi hizo mbili.Kardinali Yeom amesisitizia umuhimu wa sala,msamaha na mapatano.Na kuikabidhi nchi yao BikiraMaria Malkia wa amani katika kipindi hiki msingi cha Taifa lao.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Muunganiko wa sala kwa ajili ya mapatano, umoja na amani katika  Peninsula ya Korea umesikika hivi karibuni katika Shule moja  ya  Dongsung  katika Jimbo Kuu la Seoul nchini Korea Kusini. Tukio la maombi limendaliwa na Tume ya Upatanisho kitaifa ya Jimbo Kuu la Seoul wakati wa maandalizi ya Siku ya Kitaifa ya sala iliyoanzishwa na Baraza la Maaskofu wa Korea kunako mwaka 1965. Hili ni tukio la kila mwaka ifikapo tarehe 25 Juni kukumbuka nchi ya Korea Kusini ilipovamiwa na Korea ya Kaskazini na kuanza vita mbaya sana iliyoleta majanga makubwa.

Kuhamasisha umoja na amani

Ukumbi wa shule ya Dongsun ulikuwa umejaa waamini karibia elfu tatu ambao waliweza kudhuria mpango mzima kuanza na maadhimisho ya Misa Takatifu, kusali Rosari kusikiliza somo kuhusu Kanisa nchini Korea ya Kaskazini. Mwisho wa shughuli nzima, makumi ya vijana kutoka jumuiya katoliki ya Mongolia waliweza kutumbuiza  nyimba na michezo ya utamaduni wao. Tamasha hili lilikuwa ni ishara ya kutoa  shukrani kubwa kwa ajili ya msaada wanaoupokea kutoka Kanisa la Korea na kama ilivyp pia mshikamano wa wakatoliki wa Mongolia katika kuhamasisha umoja na amani katika peninsula ya Korea. Misa Takatifu iliadhimishwa na Askofu Mkuu Kardinali Andrea Yeom Soo-jung,  wa Jimbo Kuu Katoliki Seoul kwa ushiriki wa  Balozi wa Kitume wa Pyongyang, Monsinyo Matteo Hwang, Katibu wa Kitume Padre Achilleo Chung Se-Teok na Seoul  Padre Luca Lee ambaye ni katibu wa Tume ya Upatanisho wa Kitaifa wa Jimbo Kuu Katoliki vilevile na mapadre wa Jimbo Kuu.

Umuhimu wa sala na msamaha

Wakati wa mahubiri yake, Kardinali Yeom amesisitizia umuhimu wa sala, msamaha na upatanisho ili kuweza kufikia amani katika peninsula ya Korea. Mbele ya hali halisi ngumu na jitihada anasema kwa hakika ni jitihada zilizofanyika zaidi ya mwaka uliopita kufikia kusitisha silaha za kinyuklia nchini  Korea ya Kaskazini. Hata hivyo anasema, japokuwa katika peninsula ya korea haijazalisha matokeo yoyote yanayoonekana na ambayo  inastahili yaonekane, lakini wanatambua kuwa ni muhimu sana na dharura kusali kwa moyo wao wote na nguvu zao zote kwa ajili ya malengo hayo. Sala hii pia ni huduma muhimu ambayo Kanisa lao wanaweza na wanapaswa kufanya hivyo kwa taifa lao na kwa watu wote ulimwenguni amethibitisha.

Kampeni ya sala tangu 2015

Kardinali Yeom pia amezungumzia juu ya kampeni ya sala ambayo imepewa jina, kulinda ndani ya moyo parokia ya Kaskazini, ambapo Jimbo Kuu la Seoul lilianzisha kunako mwaka 2015. Hii  kutokana na kutaka kujikata katika matendo ya dhati kwa kuitikia wito wa ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko alioutoa wakati wa mahubiri yake katika hitimisho la ziara ya  kitume nchini Korea kunako 2014.  Wito huo ni kusali kwa ajili ya parokia 57 na waamini 52,000 ambao walikuwa wanaishi Kaskazini, kabla ya mgawanyiko wa nchi.  Kutokana na kampeni hiyo Kardinali Yeom amethibitisha kwamba wanapeleka mbele kampeni hiyo kwa kuamini kwamba kadiri wanavyo wakumbuka ndivyo wanapaswa kushi na iwapo wanasali kwa ajili ya malengo hayo sala zao zitaonekana. Wanataka kuendelea kuwakumbuka na kusali kwa ajili ya ndugu kaka na dada wa kaskazini ambao wanateska kwa ajili ya kunyimwa haki zao za kibinadamu na  kunyimwa uhuru wa kidini.

Umoja wa kiroho katika mateso

Kardinali Yeom akiendelea na mahubiri yake amesema ni kumwomba Mungu aweze kuwatunza wale wote wanaoishi maisha ya imani yao kwa siri na katika mateso. Kwa kufanya hivyo, wanataka kuomba awaongoze katika umoja wa kiroho katika mateso yao, kama sadaka ya dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya wokovu wa taifa lao, ili wajitahidi kuinjilisha watu wote wa Kusini na kaskazini. Kwa mtazamo huo, kampeni hiyo inapaswa kuwa na harakati ya ufanisi wa umoja mshikamano unao unganisha, hata kama ni isiyoonekana huko Kusini na Kaskazini kwa njia ya sala!

Hakuna kupoteza matumaini

Askofu Mkuu wa Seoul kadhalika amepongeza nguvu ya sala iliyojionesha  hada sasa katika mchakato mzima wa historia yao. Na kuongeza kusema hata kama bado hawajaona matokeo ya jitihada za kufukia kukomesha silaha za kinyuklia huko Korea Kaskazini, kuwa na ubinadamu zadi na uinjilishaji wa jimuiya ya Korea kaskazini, laini pia hata amani kamili  katika pensula ya Korea, wasipoteze matumaini! Ni kukaa na kuomba daima kwa imani kwa Mungu, Bwana wa historia  ambaye mikononi mwake ameshikilia mioyo ya watu, ndipo kuna uhakika wa kuwa na uwezo wa kushinda nguvu za uovu na kufanya muujiza wa amani!

Kusitisha silaha za kinyuklia Korea ya Kaskazini

Kardinali Yeom  pia amesisitiza juu ya  amani  ya kwamba inawezekana tu kwa njia ya msamaha na upatanisho. Msamaha  ndiyo siyo rahisi, lakini ni asili ya utambulisho wa Kikristo na ni hali ya lazima ya kusamehewa na Mungu amesisitiza. “Tunapaswa kumwomba Bwana ili atupatie neema ya kusamehe, kwa sababu kujua kusamehe ni neema”, kama Baba Mtakatifu Francisko alivyosema. Ikiwa tunaomba na kufanya kazi pamoja; tunasamehe na kujipatanisha mmoja na mwingine; kwa jina la kusitisha silaha za kinyuklia ya Korea ya Kaskazini; ya ubinadamu; ya uinjilishaji wa kijamii huko Korea Kaskazini na kuwa na amani ya kweli katika Peninsula ya Korea, kwa hakika Mungu atasikiliza sala zetu” amethibitisha Kardinali Yeom.

Kuelekea maendeleo ya kweli ya Peninsula ya Korea

Askofu Mkuu wa Seoul hatimaye amemkabidhi Bikira  Maria Malkia wa amani na kwa maombezi yake katika kipindi hiki cha taifa leo na jitihada ambazo zinafanyika japokuwa na matatizo makubwa na mara nyingi katika hali nguvu ili kuweza kufikia amani ya kweli na maendeleo ya kweli ya Korea ya Kusini.

25 June 2019, 17:10