Kuna ulazima wa kuingilia kati kwa haraka ili kuzuia vijana zaidi wasiwe na msukumo wa kutafuta njia nyingine za kuhama nchi zao kutokana na hali mbaya ya kiuchumi nchini Nigeria Kuna ulazima wa kuingilia kati kwa haraka ili kuzuia vijana zaidi wasiwe na msukumo wa kutafuta njia nyingine za kuhama nchi zao kutokana na hali mbaya ya kiuchumi nchini Nigeria 

Kardinali Onaiyekan:Mgogoro wa nchi unaweza kupata suluhisho kwa njia ya kuwekeza kwa vijana!

Kuna ulazima wa kusema ukweli kuhusu hali halisi ya nchi kutokana na ukosefu wa usawa kijamii na kiuchumi ambao ni hatari hata nchi nyingine barani Afrika na vijana kuhama nchi zao wakitafuta fursa za ajira.Ni kwa mujibu wa ujumbe wa Kardinali John Olorunfemi Onaiyekan askofu mkuu wa Abuja akitaka mabadiliko chanya ambayo yaanzie ndani ya mioyo ya ngazi za chini hadi za juu nchini Nigeria.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika ujumbe wa uliotolewa na huduma ya kiliturujia wa muungano wa kidini wakati wa sherehe za  rais wa nchi anaingia katika makazi, kwenye sherehe zilizofanyika katika Kituo cha Kikristo cha Taifa katika mji mkuu, Kardinali John Olorunfemi Onaiyekan, askofu mkuu wa Abuja amesema, ili kuweza kuhakikisha mabadiliko chanya ni lazima wawe tayari kuwa na madiliko na uongofu ndani ya moyo kwa dhati kuanzia ngazi ya chini hadi kufikia ya juu. Akizungumza mbele ya Rais wa Jamhuri ya Nigeria Muhammadu Buhari aliyechaguliwa kwa kura kunako tarehe 23 Februari mwaka huu, Kardinali Onaiyekan amesisitiza juu ya ulazima wa kusema ukweli kuhusu hali halisi ya nchi na akinyoshea kidole juu ya ukosefu wa usawa kiuchumi na  ambao huko katika hatari hata katika nchi nyingi barani Afrika.

Changamoto za umasikini

Changamoto za umasikini amesema zinazidi kuongezeka siku hadi siku. Hawana matumaini na nguvu, wakati wakitazama kwa unyongo mkubwa utajiri wa walio walio wachache ambao wanaishi upande wa dunia. Hukosefu wa  ulinganifu wa namna hii kiuchumi na kijamii unazaa hasira, mivutano, ghasia na uhalifu. Lakini  hata hivyo amesititiza umuhimu wa kuepuka kukuza tofauti za kikabila na dini kwa lengo la madaraka. “ Tofauti zetu za kikabila ni mapenzi ya Mungu na hivyo lazima kuzithamini na kuzishehereka. Lazima kuwa makini kwa wale wanaojaribu kutumia tofauti hizi katika mchezo wa kutengenisha na kuutazama kwa ajili ya kukuza maslahi binafsi”, anasema. Katika ujumbe wake Kardinali Onaiyekan amesema: “katika dunia yetu ya dharura inahitaji kujikita na kuinamia katika  uzoefu wa muda mrefu wa kuishi kwa njia ya mitindo ya makabila, hivyo tusiruhusu sisi wenyewe kuachwa nyuma katika dunia ya kisasa yenye maendeleo ya haraka”.

Kardinali Onaiyekan anasisitiza kuwa wasiruhusu kutumia dini kwa ajili ya maslahi ya kisiasa

Aidha Kardinali Onaiyekan ameongeza, kamwe wasirihusu kutumia dini kwa ajili ya maslahi ya kisiasa kwa sababu ni hatari ya kuidhuru taifa ambao ameonya kuwa: “ Katiba yetu siyo kamilifu. Lakini masharti yake juu ya uhuru wa dini ni mambo ambayo ni sahihi na yanapaswa kuheshimiwa kwa wote, hasa wale wanaodhibiti vyombo vya serikali. Askofu wa Abuja daima amekuwa mwamasishaji mkuu juu ya maoni ya umma na jumuiya ya kimataifa kuhusu matatizo ya nchi kuhusu ukosefu wa usawa kijamii, ukosefu wa ajira kwa vijana na rushwa. Na kwa maana hiyo hivi karibuni amewashauri viongozi wa Nigeria wawe makini na dharura ya vijana akisema kuwa: “iwapo unaishi katika taifa ambalo wao vijana  wenyewe wanakusimulia kuwa ni bora kuishi mahali pengine, hii ni ishara ya hatari ambayo inapaswa kuzingatiwa na siyo mchezo”.

Viongozi wa Nigeria wawezeshe nchi kuwa nyumba ya wanaigeria

Kwa maana hiyo anasisitiza kuwa kuna ulazima wa kuingilia kati kwa haraka kwa maana ya kuzuia vijana zaidi wasiwe na msukumo wa kutafuta njia nyingine za kuhama. Akitoa mfano binafsi amesema: “ninakumbuka nilivyokuwa shuleni miaka kadhaa, nilikuwa napenda Nigeria na kuthibitisha wazi, kwa maana nilikuwa naitangaza sarikali ambayo ilikuwa inanilinda na mbele yangu kulikuwa na ahadi za wakati ujao. Kwa bahati mbaya hali ya kiuchumi leo hii imebadilika na mambo kuwa mabaya”. Askofu Mkuu wa Abuja amesema, viongozi wanapaswa wawezeshe Nigeria ili iweze kuwa nyumba ya kweli ya wanaigeria kama pia hata nchi nyingine za Afrika ili vijana wasikate tamaa na ambao anamesma “ tunasikia wanasema malisho ya kijani yako mahali pengine, hata kama mambo sivyo yaliyo”, kwa kutoa mfano kwamba wapo wasichana wa nigeria ambao wamepelekwa kwenye ukahaba barani Ulaya.

Asilimia 35 ya wanaigeria wanataka kuacha nchi yao

Kwa mujibu wa  Mtandao wa Utafiti wa Pan-Afrika Afrobarometer, asilimia 35% ya wanaigeria wanataka kuacha nchi yao na asilimia 11% wanathibitisha kiukweli kutaka kufanya hivyo. Na zaidi, asilimia 75% ya wanaigeria ambao wanataka kuhama wanafanya hivyo kwa sababu ya kiuchumi, hukosefu wa ajira, kukimbia umasikini na kutafuta unafuu wa fursa bora za maisha. Utafiti hata hivyo umeonesha kuwa vijana walioelimika karibia asilimia 44% ya wanaigeria wana shahada na ambao wanataka kuhama, wakati utafiti mwingine wa pili unaonesha kuwa asilini 80%  ni wenye utaalam wa udaktari. Katika hitimisho la Kardinali Onaiyekan, ameelekeza njia za kufuata kwa ajili ya kukabiliana na hali hii, awali ya yote “ seikali lazima endeleze sera za kisiasa zenye uwezo wa kuvutia na kuwekeza nchini Nigeria kwa namna ya kuweza kuunda fursa za ajira na kuwapatia misaada kwa vijana ambao wanataka kuanza shughuli za kujitegemea.

12 June 2019, 13:26