Kanisa la Kimelkiti nchini Lebanon la sambazwa Hati ya Abu Dhabi
Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican
Kanisa Katoliki la Kigiriki-Melkita nchini Lebanoni wanajiandaa kutoa nafasi kubwa ya mpango wa kichungaji hasa katika kutafakari kwa kina juu ya Hati ya udugu kibinadamu kwa ajili ya amani duniani na kuishi kwa pamoja, iliyotiwa sahihi tarehe 4 Februari 2019 huko Abu Dhabu na Baba Mtakatifu Francisko na Sheikh Ahmed al Tayyeb, Imam mkuu wa Al Azhar. Hayo yote yamethibitishwa na msemaji wa Sinodi ya Maaskofu wa Kigiriki-Melkiti walio unganika katika Mkutano wao mkuu hivi karibuni katika makao makuu ya Upatriaki wa Ain Traz, nchini Lebanon, chini ya usimamizi wa Patriaki Youssef Absi.
Mafunzo ya utafiti katika shule za Upatriaki
Katika maelezo ya msemaji wa Sindo hii amefafanua juu ya lengo azimio hili kwamba ni kutaka kuhamasaisha uelezwa zaidi katika makuzi ya kizazi kipya na endelevu kwa namna ya kuweza kijenga namna bora ya kuishi katikati ya jamii tofauti na kidini katika nchi mahali ambamo kuna hata Kanisa la Kimelkiti na mara nyingi panatokea hupotoshwaji na migogoro ya kidini na uharibifu wa kitikadi. Mpango wa maaskofu wa kimelkiti kwa mujibu wa msemaji kuhusu Sinodi hiyo unakita kwa dhati katika masuala ya kweli yakijuishwa iwe katika shughuli za elimu, hata zile za kichungaji. Hati juu ya udugu kibinadamu, itakuwa ni nyeti kwa mafunzo na utafiti katika shule za upatriaki na katika taasisi za kitaalimungu, wanathibitisha.
Maandiko ya Hati yatasambazwa kwa walei na mashuleni
Pia maandiko ya Hati hiyo yatasambazwa sana kati ya waamini walei na yaliyomo ndani ya hati yaweze kutafakariwa jwa kina katika mikutano ya majimbo na maparokia. Hata mapadre wanahimizwa kujua vema yaliyomo na malengo ya Hati hiyo ya Abu Dhambi ili waweze kuyatumia wakati wa mahubiri yao ya kawaida. Wakati wa Sinodi yao, maaskofu 24 wa upatriaki waliokuwapo wamegusia pia suala la jinsi ya kulinda watoto waathirika kwa manyanyaso kwa kwa kupitia ushauri wa Barua ya Kitume ya Baba Mtakatifu Francisko ya Vos estis lux mundi, iliyotangazwa tarehe 7 Mei 2019.
Maandalizi ya Kongamano la kiliturujia 2022 mjini Roma
Zaidi ya hayo Maaskofu wamezindua kamati ya maandalizi ambayo itasaidi kushiriki na kutoa mchango wa Kanisa la Kimelkiti katika Kongamo kimataifa kuhusu maisha ya liturujia katika Makanisa Katoliki ya Mashariki, inayotarajiwa kufanyika mjini Roma kuanzia tarehe 18-20 Februari 2022. Tukio hili litafanyika wakati wa fursa ya maadhimisho ya miaka 25 tangu kutolewa maagizo ya matumizi ya kanuni za Sheria ya Liturujia ya Makanisa ya Mashariki, iliyochapishwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki kunako mwezi Januari 1996.