Tafuta

Vatican News
Maaskofu nchini Ivory Coast  wameandika ujumbe wao kuhusiana na hali tenge ya nchi yao kuelekea katika uchaguzi 2020 Maaskofu nchini Ivory Coast wameandika ujumbe wao kuhusiana na hali tenge ya nchi yao kuelekea katika uchaguzi 2020 

Ivory Coast:Kuna hofu kubwa inayotawala katikati ya watu!

Mara baada ya Mkutano wa Baraza la Maaskofu nchini Ivory Coast,wametoa ujumbe wao wa mwisho wenye kuwalenga wazalendo na viongozi wa nchi kufuatia na hali halsi tenge katika kuelekea uchaguzi mkuu wa 2020.Kilio cha Maaskofu kwa ajili ya wazalendo wao ni kwamba hawataki kuona vita tena vinatokea!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika hitimisho la Mkutano wa 113 wa Baraza la Maaskofu nchini Ivory Coast  uliofanyika huko Agboville hivi karibunu wanaandika kwamba lazima kutambua kuwa  katika wakati wa kukaribia uchaguzi wa rais 2020, katikati ya watu kumejaa kutanawaliwa na hofu kwa watu. Kilio chao Maaskofu kwa ajili ya wazalendo wao ni kwamba hawataki kuona vita tena! Maaskofu wanaandikiwa kwamba hii ni hali halisi inayotokana na migogoro ya ndani ya jumuiya, matatizo ya ukosefu wa usalama, umiliki wa ardhi, kuvamia kwa misitu bila idhini, uchimbaji wa madini, kama dhahabu usio halali na matatizo yanayohusu utambulisho wa Watu wa Ivory Coast.

Ukaribu wa familia zenye matatizo

Maaskofu wakiwageukia waamini waowanadhibitisha, kwamba  wako pamoja nao karibu ili  kuomba kutona na upweke walio nao katika siku hizi za mwisho, na wanataka kwa  pamoja kuharibu mapepo ya kizamani ya chuki na mgawanyiko. Katika maono hayo maaskofu pia wanaonesha ukaribu wa kiroho na huruma kwa ajili ya familia ambazo zimepoteza wapendwa wao na mali zao. Na wanawaomba hata wadau wpte wa kutetea maisha ya kijamii –kisiasa ili kuweza kuzuia vita isitokee.

Kufanya kila njia ya ili kuwa na amani

Baada ya makumi miaka katika kipeo kigumu cha kiuchumi nchini humo na ambacho kimesababisha majanga mabaya katika historia ya Ivory Coast na baadhi ya miezi inayoelekea kufikia mwaka 2020, maaskofu wanasema  wahusika na ambao wanafikiri ni wenye madaraka, kwa ngazi zote wanaweze kufanya kila njia iwezekanavyo ili kuwa  na mchakato wa mapatano ya kijamii kwa namna ya kuweza kuzuia kipeo kingine kisitokee wakati huo huo kuweza kuimarisha amani.

Kufikia mwisho wa mchakato wa kusitisha silaha

Wakigeukia serikali, Maaskofu wakuu na maaskofu wa Ivory Coast wanawaomba serikali kuendelea na kukamilisha mchakato wa kusitisha silaha kwa sababu silaha zinaendelea kuzunguka nchini humo na wasema hiyo  siyo siri kwa mtu yeyote yule. Wanahitimisha wakiomba kusitishwa kwa silaha za aina yoyote ile zinazo zunguka nchini humo na kwa jina la haki ya maisha wanaomba waepuke vita kwa mara nyingine tena!

25 June 2019, 14:46