Tafuta

Vatican News
 Askofu Mkuu wa Asmara anawaalika Kanisa mahalia kufunga na kusali kwa ajili ya taifa hilo, mara baada ya tukio la serikali kuchukua uamuzi wa kufunga vituo katoliki 22 vya afya Askofu Mkuu wa Asmara anawaalika Kanisa mahalia kufunga na kusali kwa ajili ya taifa hilo, mara baada ya tukio la serikali kuchukua uamuzi wa kufunga vituo katoliki 22 vya afya 

Eritrea:Askofu Mkuu anaomba sala kwa ajili ya nchi ya Eritrea kufuatia na kufungwa vituo Katoliki vya afya!

Kufuatia na serikali kuchukua uamuzi wa kufunga vituo 22 vya afya vinavyo endeshwa na Kanisa Katoliki nchini Eritrea hivi karibuni,Askofu Mkuu wa Asmara Abune Mengesteab Tesfamariam anawaalika Kanisa zima mahalia kufunga na kusali kwa ajili ya taifa hilo.Sala na kufunga vitahitimishwa tarehe 29 Julai wakati Kanisa hilo linaadhimisha sikukuu ya watakatifu Petro na Paulo

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican

Askofu Mkuu wa Asmara nchini Eritrea Abune Mengesteab Tesfamariam anawaalika Kanisa zima mahalia kufunga na kusali. Ni maelezo yaliyomo katika barua yake kwa waamini wote wa Kanisa katoliki la Aritrea iliyoandikwa tarehe 22 Juni 2019 huku akiomba waamini wote kuhamasika katika makanisa, monasteri katoliki ya nchi na hasa kuanza sala hiyo hasa katika siku ya kufanya kumbukumbu ya Mtakatifu  Giustino de Jacobis aliyekuwa mmisionari wa Shirika Lazaro huko Abisinia na kuhitimisha maombi kwa nia hiyo tarehe 29 Julai 2019 katika Sikukuu ya Petro na Paulo kwa mujibu wa Kalenda yao ya Kiliturujia ya Kigeez.

Sala na kufunga na matumaini katika Bwana

Akiwageukia maparoko, watawa wote Askofu Mkuu Tesfamariam anaonesha kwa uchungu hali mbaya ya nchi iliyotokana na uamuzi wa Serikali ya Eritra hivi karibuni, kwa kufunga vituo 22 vya afya vinavyoendeshwa na Kanisa katoliki na katika patriaki nne nchini humo. Uamuzi huo ni kama jibu kuwalekeza maaskofu kutoka kwa Rais Isaias Afewerki,ambaye yupo madarakani tangu1993. Askofu Mkuu wa Asmara anataja nabii Nehemia. Niliposikia maneno hayo, nilikaa, nikalia na kwa siku nyingi nilikuwa na uchungu. Nilifunga na kusali mbele ya mbingu. Kutokana na hiyo anaeleza  ni Mungu peke yake anaweza kuwasaidia kuwatuliza na kutatua matatizo yao.

Karibu na wagonjwa kazi yao siyo ya bure

Tutaweza kutulizwa na Bwana anasema na kutoa wito mkuu kutoka katika Nabii Isaya: Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa na shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako. (Is 38,17).  Pia anaandika matatizo ambayo wanaishi kwa sasa lazima yawapatie nguvu badala ya kuwadhoofisha. Wazo kuu la sala linawaendelea kwa namna ya pekee wagonjwa na watawa wote ambao walijikita maisha yao yote kwa ajili yao. Huduma yao na ugumu walio upata siyo wa bure na Bwana atawakarimia kwa wingi wa neema kwa yule atakaye vumilia majaribu na Yeye.

26 June 2019, 17:23