Mkutano Mkuu wa XXI wa mwaka wa Muungano Kimataifa wa wakuu wa Mashirika ya kitawa (UISG) umewakilishwa katika vyombo vya habari Vatican Mkutano Mkuu wa XXI wa mwaka wa Muungano Kimataifa wa wakuu wa Mashirika ya kitawa (UISG) umewakilishwa katika vyombo vya habari Vatican  

Sr. Summut(UISG):Maisha ya kitawa siyo suala la idadi tu!

Sr Carmen Summut,Rais wa Muungano Kimataifa wa wakuu Mashirika ya kitawa(Uisg),amewakilisha katika vyombo vya habari Vatican kuhusu Mkutano Mkuu wa XXI wa mwaka unaotarajia kuanza tarehe 6-10 Mei.Utamadunisho,wakati endelevu wa maisha ya kitawa,ushirikishwaji katika “Laudato Si”na mazungumzo ya kidini ni mada pia zitakazoguswa.

Na  Sr Angela Rwezaula - Vatican

Sr Carmen Summut, rais wa Muungano Kimataifa wa wakuu Mashirika ya kitawa (Uisg), ambaye wakati wa kuwakilisha kwa vyombo vya habari Vatican kuhusiana na Mkutano Mkuu wa XXI wa mwaka, amesema maisha ya kitawa siyo masuala ya idadi tu, bali ni jitihada za kina kwa ajili ya Kristo katika kujikita kwa walio na mwisho. Sr Summut amewakilisha mkutano huo wa mwaka unaotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 6 - 10 Mei 2019 mjini Roma (katika Hotel Ergife) kwa kuongozwa na tema: “wapanzi wa matumaini ya kinabii”. Sr Carmen  katika fursa hiyo amesema, katika maeneo mengi miito inashuka na maeneo mengine  inaongezeka. Lakini maisha ya kitawa na faida zake ambazo zipo katika Kanisa hazitazami tu masuala ya idadi, kinachotakiwa ni jitihada za kina kwa ajili ya kuhudumia Kristo  katika walio wadhaifu na ambamo watawa wanatumwa kuhudumia.

Wakuu wa mashirika 850 kutoka nchi 80 duniani wanatarajia kuwapo

Hata hivyo taarifa kuhusu mkutano ho zinathibitisha kwamba,  katika mkutano huo wanatarajiwa wakuu wa mashirika 850 kushiriki  kutoka nchi 80 duniani na lugha 13 rasmi za kimataifa  zitatumika katika mkutano huo; Karibia wageni watoa mada 40 wamelikwa, na kati yao kutakuwa na wawakilishi kutoka Mabaraza ya Maaskofu katika mabara yote/ watawa na Mabaraza ya kipapa Vatican, wahusika wa mashirika ya wafadhili wa Umoja huo Uisg.  Vile vile masuala ya umadunisho, wakati endelevu wa maisha ya kitawa, ushirikishwaji wa nyumba yetu ya pamoja unaozungumzwa  na Baba Mtakatifu katika  Wosia wa “Laudato Si”na  mazungumzo ya kidini, ni mada msingi ambazo zitaweza kugusiwa katika siku nne za kazi ya mkutano huo.

Tarehe 10 Mei 2019 wakuu wa mashirika hao wanatarajia kukutana na Baba Mtakatifu katika mkutano faragha. Katika fursa hiyo Baba Mtakatifu atatoa tangazo rasmi la “Kampeni ya mwaka wa 10 wa Talitha Kum”, ambalo ni mtandao wa kimataifa wa maisha ya kitawa dhidi ya mapambano ya  biashara ya binadamu. Kampeni hiyo inaongozwa na kauli mbiu: “Watawa wanaponyesha Roho”. Hata hivyo taarifa zainathibitisha kwamba  anayetaka kufuatilia Mkutano huo moja kwa moja, itakuwa rahisi kufuatilia kupitia streaming.Katika kila kipindi, Sr. Summut ametangaza kuwa, watazungumza hata juu ya ulinzi wa watoto walioathirika na manyanyaso ya kingono na umakini wa kutunza walio yatima ambao wamejaa duniani kote. Vile vile amebainisha kwamba, watawa walio wengi wanajikita katika kutafuta mahali pa kuwahamishia wadogo kutoka katika majengo ya taasisi ili waweze kuishi katika jumuiya, yenye tabia ya kifamilia.

Wanapaswa kujiuliza pamoja, kwa jinsi gani wanaweza kuishi matumaini katika Mashirika yao

Naye Sr Anabela Carneiro, mama Mkuu wa Shirika la Watawa wa Hospitali ya Moyo Mtakatifu wa Yesu amesema kuwa, tema ya Mkutano huo inakwenda sambamba na matarajio yao. Wao wanapaswa kujiuliza pamoja, kwa jinsi gani wanaweza kuishi matumaini katika Mashirika yao, kwa watawa pia  wanapaswa kujiuliza  ni kwa jinsi gani wanaweza kukumbatia na kuwasaidia watu ili waweza kukumbatia wakati ujao kwa matumaini kama anavyozidi kuomba Baba Mtakatifu Francisko.

Lengo la Mkutano wa mwaka ni hatua ya lazima katika kutoa muundo wa Kanisa la kisamaria

Sr. Carneiro amesisitiza pia  juu ya  suala la  kushirikiana na kwamba  ni ishara ya umoja kwa maana  ardhi ni nyumba yetu ya pamoja. Lengo la Mkutano wa mwaka ni kufanya hatua ya lazima, hata katika kutoa muundo ili kujikita ndani ya Kanisa ambalo lazima liweze kuwa msamaria, kuwa na ukaribu kwa mamilioni ya watu ambao inakutana nao, waathirika wa vurugu na nguvu na katika utandawazi wa sintofahamu!

Hakuna mtu anayeweza kupeleka mbele utume na maisha ya kitawa peke yake

Kwa upande wa Sr Donatella Zoia Mama Mkuu wa shirika la Watawa wa Damu Azizi amesema, unabii unapitia kwa njia ya muungano, kusaidiana, uwezo wa kuunda mtandao wa mshikamano na ushirikishwaji. Aidha akisisitiza amesema, katika  muungano wa wakuu wa mashirika kimataifa (Uisg) ushirikishwaji upo kila kona ya dunia, kwa maana sehemu kubwa ya mashirika yao ni ya kimataifa, japokuwa kitu cha kimataifa ni kitu tofauti sana na kuishi utamadunisho ambao unazingatia juu ya mchakato wa kukomaa na ambao unapitia njia ya kukabiliana kati ya tamaduni tofauti. Hakuna mtu anayeweza kupeleka mbele utume na  maisha ya kitawa peke yake. Na kwa namna hiyo ndipo kuna umuhimu wa kuanzisha michakato ya mafunzo na utume katika familia zao za dini na katika kiungo kizima cha kila siku katika  huduma yao  kwa watu wa Mungu, hasa hasa kati ya watu walio dhaifu sana.

03 May 2019, 14:21