Tafuta

Vatican News
Vijana 800 kutoka majimbo katoliki 170 nchini Italia wameshiriki Jukwaa la kitaifa la kichungaji kwa vijana lililofanyika kuanzia 29 Aprili hadi 2 Mei 2019 huko Palermo Sicilia Vijana 800 kutoka majimbo katoliki 170 nchini Italia wameshiriki Jukwaa la kitaifa la kichungaji kwa vijana lililofanyika kuanzia 29 Aprili hadi 2 Mei 2019 huko Palermo Sicilia  (Vatican Media)

Kard.Bassetti:Hakuna haja ya kujua kutembea juu ya maji,bali ni katika kupiga mbizi baharini hata katika dhoruba!

Katika mkesha wa vijana 800 washiriki wa Jukwaa la kitaifa la uchungaji vijana,kutoka majimbo 170 ya Italia lililofanyika Palermo Sicilia,Kardinali Gualtiero Bassetti,Rais wa Baraza la Maaskofu Italia amehimiza vijana wakuze imani katika matumaini itakayowasaidia wasizame katika maji ya kina,ya kifo na hisia mbaya za kushindwa!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ni katika imani na katika matumaini inayosaidia ili kutoweza kuzama katika maji ya kina, kuzama katika kifo, kuzama katika hisia mbaya na maana ya kushindwa kwa mujibu wa Kardinali Gualtiero Bassetti, Rais wa Baraza la Maaskofu Nchini Italia wakati wa mkesha wa sala wa Jakwaa la Kitaifa la uchungaji wa vijana katika Kanisa la Kuu la Monereale huko Palermo Sicilia huku akiwaalika watazame wale wanaojikita kusaidia vijana. Jukwaa la XVI la  Kitaifa la Uchungaji vijana lilizinduliwa huko Terrasini (Pa) kuanzia tarehe 29 Aprili na kufungwa tarehe 2 Mei 2019. Ni tukio ambalo limefanyika likiwa linaangukia mwisho wa mwaka wa kumi tangu Kanisa la Italia lianze kujihusisha na kuelimisha na baada ya Sinodi ya vijana wa Kanisa la ulimwengu. Jukwaa hili limewahusisha wahusika wa majimbo katika shughuli za kichungaji, wahusika wa kila ngazi za vyama vya kitume na jumuiya nyingine mpya, wahusika wa mashirika ya kitawa na  kisekulali kike na kiume. Kwa maana hiyo ni Jukwaa liliwahusisha ngazi zote za utume wa kichungaji kwa vijana kwa ngazi ya kitaifa! Na kaulimbiu ya Jukwaa hili la XVI ilikuwa ni: “ kutoa nyumba wakati ujao:Maneno jasiri ya Sinodi ya vijana”

Petro anazama kwa sababu hana imani aliyonayo ndani mwake na katika sababu za matumaini

Katika mkesha wa sala tarehe 1 Mei 2019, Kardinali Bassetti kwenye tafakari lake kwa vijana, limeanzia na somo lilipondekezwa kutoka katika Injili, mahali ambapo Yesu anatembea juu ya maji. Kardinali Bassetti kwa kuwaalika vijana watazame Petro kwa niaba ya wafuasi wote waliokuwa wameogopa sana kifo cha mwalimu wao, amesema: “Petro anazama kwa sababu haamini imani aliyo nayo ndani mwake na katika sababu za matumaini ambayo yanafanya kazi daima ndani ya moyo wa kila mtu kulinganisha na mtu mwenyewe”. Aidha anaongeza kubainisha kuwa: “Petro hakuwa na imani katika sababu ya kuishi na ambayo ni imara dhidi ya dhoruba”, hata hivyo ameongeza “ni dhoruba ngapi tutapaswa kukutana na kukabiliana nazo katika maisha”!

Mwalimu anatualika kutoka nje yetu binafsi kwa ujasiri hata kwa machozi mengi

Akiendelea na tafakari hili amekumbusha kwamba, Bwana mara nyingi anarudia  kuwatia moyo  masikini kama sisi kwamba: “nenda zako imani yako imekuokoa” pia “ “Amka na tembea”. Yesu yupo kwa ajili ya kutupatia ujasiri katika ujasiri wetu, yeye yupo si kwa ajili ya kubadilisha sisi. Yesu ana imani katika imani yetu masikini na mara kwa mara anaendelea kuacha mlango wake umefunguliwa wa upendo na huruma mbele yetu. Vile vile Kardinali Bassetti amesisitiza kwa vijana kwamba, “Bwana anaamini nafsi yetu tuliyo nayo, japokuwa hawezi kutenda kwa niaba yetu”. Hakuna ambaye anaweza kuishi maisha yetu, hakuna anayeweza kushi nafasi ya maisha ya mwingine, hata Mungu na Yesu mwenyewe. Mwalimu anatualika kutoka nje yetu binafsi kwa ujasiri wote bila kujibakisha ili kuweza kuishi maisha yetu kikamilifu, licha ya kutokwa hata na machozi mengi amethibtisha.

Petro anamwambia Yesu niokoe, maana yake niokoe na hofu zangu

Kardinali Bassetti akiendelea kutafakari, amejikita kutazama neno la Petro alilomwambia Yesu kuwa, “ Niokoe”. Neno hili niokoe ni kutaka kusema, niokoe na hofu zangu, na mawazo yangu, na kivuli changu. Na Yesu mwenyewe anawaondolea  hofu hiyo kwa kusema “ siyo kivuli” hata kama mitume walikuwa wanaona vile. Hata hivyo, mesema, mara nyingi sisi tunaamini vivuli na kuunda vivuli hivyo katika maisha na mihungu ya uongo. Zaidi ya maji hayo, Yesu anamwokoa Petro na hofu na vivuli vyake. Lengo kuu,Kardinali anathibitisha, siyo kutembea juu ya maji na kuchangamotisha ulimwengu, badala yake ni kuendeleza ile nguvu ya ndani ambayo inaweza kuhakikisha unaogelea na kupiga mbizi ndani ya maji hata kama kuna dhoruba kali. Kuamini daima kunakuwezesha kutembea hadi juu ya maji yaliyo na dhoruba. Kwa kufanya hivyo lakini  inahitaji kuwa na uhusiano wa kina na Yesu, pia  hiyo inahitaji ishara ya upendo wa Yesu ambaye anampa mkono Petro na kumwokoa katika meno ya kifo!

Padre  Falabretti (Cei),miongozo ya mpango ni waraka wa kazi,wameusoma na kushirikishana na unahitaji sasa utekelezaji

Katika hitimisho la Jukwaa la siku nne kisiwani Sicilia ambapo Huduma ya Kitaifa ya  kichungaji ya vijana imeweza kukutana na wale wanaojikita katika sekta hiyo kwenye  majimbo yote katoliki nchini Italia, Mkurugenzi wa huduma ya kichungaji kitaifa, Padre Michele Falabretti, amewakilisha mipango mipya kiongozi itakayo wasaidia katika shughuli hiyo msingi. Padre Falabretti anasema “kwa pamoja elfu moja mmetuomba nini sasa cha kufanya na tumetafuta kujibu maswali yenu, kwa kuwahamasisha, lakini msisubiri kuupokea ndani ya masaa ya siku”. Aidha amesema: “Miongozo ya mpango huo  ni waraka wa kazi ambao mmeusoma na kushirikishana,na  ambao unapendekeza tabia na mambo ya dhati ya kutekeleza”.

Ni kikapu cha zana ambamo kuna zana kwa ajili ya kufanyia kazi na ambamo sasa inatuweka kujikita katika  matendo. Kwa kuipatia baadhi ya picha na mfumo mzima, wamependekeza kwa ufupi katika miaka 9 kati ya 10 ambayo wamefanya uzoefu kwa kujikita kuelimisha kuanzia na maelekezo ya elimu ya maisha ya Injili njema na kwa njia ya Jukwaa la Kitaifa la Kanisa huko Firenze, Jukwaa tatu za sekta na mchakato mrefu wa Sinodi, hati kufikia moyo wa Sinodi yenyewe na maneno yake ya kutia moyo, yenye uwezo  wa kusema ni wapi na jinsu gani ya kwenda kama ilivyojikita kundaa hata jukwa lenyewe ambalo limeongozwa na kauli mbiu “ Kutoa nyumba kwa wakati ujao”! amesisitiza Padre Falabretti.

Hatuwezi kupiga kelele ya Injili, bali inatolewa kwa  mtindo wenye haki

Akizungumza kwa wawakilishi wa majimbo 170 kutoka nchini Italia ambao wameundhuria Jukwaa la 16 la kitaifa la vijana, kama pia wawakilishi wa vyama, mashirika na jumuiya, vijana waliokuwapo wote, Mkurugenzi wa Vijana kitaifa wa Baraza la Maaskfu Italia, aidha amesema “Tunaweza kuwa kama ule moyo unaosaidia kuunganisha umoja katika jamii na katika Kanisa, lakini hatuwezi kupiga kelele ya Injili, na badala yake, inapaswa itolewe zawadi na katika mtindo wenye haki. Miongozo ambayo imefikiriwa kama utimilifu wa mihitasari mitatu iliyowekwa katika maktaba ya Sinodi  na ambayo inaakadhiwa kwa washiriki wote lakini hata kazi yao anasema, ni kukamilisha miongozo na ambapo inatakiwa kufikiria kwa mipango midogo, labda katika mpango  unaokua taratibu na kufanya hatua ndogo ndogo. Kukaa katika kipindi hiki  amesema, ni ngumu, lakini inapaswa ifanyike katika uhuru, kwa ujasiri na kwa pamoja!

Kuhusiana na miongozo ya hati hiyo

Hata hivyo Miongozo iliyotolewa kwa washiriki 800 wa tukio la Jukwaa la kichungaji kitaifa  linajikita kwa kile ambacho Kanisa limeweza kuishi kwa miaka  hii na kuendea kwa juhudi zote kuwa na dhamiri  safi na safari iliyoanza awali. Hati hiyo itaachapichwa muda si mrefu ambayo inapendelea baadhi ya maneno jasiri ya Sinodi. Hati hiyo imegawanyika katika maeneo matatu. Eneo la kwanza linatazama umakini kwa mujibu wa Mkurugenzi, kwamba ni ujuzi wa Kichungaji kwa vijana. Huu inelezea katika sura tatu zenye kuwa na maneno: Kuwapo, kutoa habari na kufungua nafasi. Kuwapo maana yake ni kusindikiza, kusikiliza na kubaki na ukaribu. Kutoa habari na kufungua nafasi kwa namna moja vinafanana, kwani ya kwanza inaeleza maeneo ya kiroho katika dunia ya kidijitali na mitandao ya kijamii, kwenye hali ya udhibiti, lakini pia hata fursa zake zinazotolewa leo hii. Na ya pili ni maeneo ya dhati, ambazo katika mwongozo ni nafasi za kuelimisha, kukutana na kusikiliza wazi kati ya wengine katika vyama na muunganiko mbalimbali. Sehemu nyingine, inajikita katika mafunzo. Hapa inapendekeza maeneo matatu na ambayo Mkurugenzi anasema: lazima yajikite kwa dhati hawa kwa viongozi wa vijana zaidi ya vijana wenyewe. Kukua na kuhisi kuitwa ndani yake na ambamo pia kuna suala la kujielezea uhusiano kati ya maisha, imani na miito; kuwajbika kwao ni kama kutoa wito katika dhamiri nafsi na kutambua kufanya mang’amuzi; kukua ndani  yake ni mahali ambamo kuna kukuza tema ya mwili, jinsia na tasaufi ambayo inaunganisha.

Na sehemu ya mwisho ya hati ya mwongozi inajikita kuelezea maisha ya jumuiya

Na sehemu ya mwisho ya hati ya mwongozo, inajikita kueleza maisha ya jumuiya na badhi ya maeneo ambayo yanasaidia kupeleka na kukutana na vijana. Hata hapa kuna maneno matatu kama ufunguo wa kujifafanua na ambayo awali ya yote ni “muungano” katika kufikiria na kutenda pamoja, baadaye kuna“ kutangaza “ambayo inapitia katika Liturujia na tasaufi yake, na hatimaye “huduma” katika kutunza, kutoa msaada wa pamoja na ushirikianoa au  kwa maana nyingine neno diaconia. Hata hivyo hati hi ya mwongozo wanasisitiza Mkurugenzi wa Cei, kuwa siyo mpango mpya wa kuelimisha, bali unajaribu kuweka mpango wa kile ambacho tayari kipo. Ni zana ambayo inafungua michakato ya safari na kuacha kupumua katika matendo mengi ya kichungaji kwa vijana. Kadhalika amesema kwamba hawakuanzisha kitu chochote ambacho wengine wanapaswa kuona kama sheria, bali  kwa namna ya kutoa fursa ya hatua ya mwanzo kwa wale wanaofanya kazi, ikiwa na maana ya timu na labda kwa jumuiya nzima ya Kikristo! Amehitimisha.

03 May 2019, 16:22