Kupambana na ubinafsi ili kujenga ustaarabu wa upendo, ndiyo  kauli ya Kampeni ya Caritas nchini Cuba Kupambana na ubinafsi ili kujenga ustaarabu wa upendo, ndiyo kauli ya Kampeni ya Caritas nchini Cuba  

CUBA:Kupambana na ubinafsi ili kujenga ustaarabu wa upendo!

Kupambana na ubinafsi ili kujenga ustaarabu wa upendo ndiyo kaulimbiu ya Kampeni ya Caritas iliyozinduliwa huko Cuba.Lengo lao ni kutaka kukuza tafakari juu ya mwenendo unaozidi kuongezeka duniani na katika jamii zao hasa suala laubinafsi.Zaidi kuhusu mahitaji na ili kujenga ustaarabu wa upendo kuanzia sehemu ya karibu hasa ya mtu jirani.

Na Sr Angela Rwezaula – Vatican

Baba yako aonaye sirini mwako atakujaza ( Mt 6,1) ni sehemu ya Injili ambayo inatumika kama kauli mbiu ya Caritas ya Cuba kwa ajili ya Kampeni ya mwaka ambayo kwa miaka miwili mfululizo itaendelea hata kwa miezi minne kuanzia Juni hadi Septemba. Lengo ni kuhamasisha watu wawe na uwelewa juu ya matatizo mengi ya kijamii ambayo yanasababisha utofauti na sintofahamu nyingi na ubaguzi kijamii. Naye Mkurugenzi wa Caritas kwa njia ya Shirika la habari za kimisionari Fides, Maritza Sánchez Abillud, ameeleza kwamba, lengo lao ni kutaka kukuza tafakari juu ya mwenendo unaozidi kuongezeka duniani na katika jamii zao huko Cuba.

Hili linahusu suala la ubinafsi na juu ya mahitaji ya kujenga ustaarabu wa upendo, kuanzia sehemu ya karibu zaidi inayomhusu mtu aliye jirani!  Shughuli mbalimbali za maonyesho na shughuli zingine zitatumika kuelimisha na kukusanya fedha katika jumuiya za kikristo za majimbo manne ya nchi. Fedha hizo zitatengwa kwa ajili ya mipango tofauti, kulingana hasa na makundi yaliyo na mazingira magumu ya kila eneo

Licha ya hali ya kiuchumi kuwa ngumu kwa  kwa watu waliowengi, mwaka 2018, Jumuiya zaidi 400 ya waamini  walishiriki kukusanya na makundi 13 ya mipango tofauti. Aidha jitihada hiza za pomoja ziliweza kufanikisha kukusanya kiasi karibia cha  Pesos 295,000 za fedha za kitaifa na zikaweza kusaidia huduma mbalimbali za mipango kwa ajili ya wazee. Mkurugenzi wa Caritas Cuba, Maritza Sánchez Abillud amesisitizia pia jitihada za Caritas jimbo kwa namna ya pekee kwa watu wa kujitolea na wahudumu wa maparokia na jumuiya.

Zaidi msaada wa wachungaji, maaskofu na mapadre, kwa njia ya barua na mahubiri vimekuwa msingi, na kwamba si tu katika mantiki ya zana, bali hata katika  umuhimu zaidi wa  kufikia lengo la kuellimisha kampeni. Kutokana na hiyo, mkurugenzi anasema kwamba, hata kama kampeni ya  Caritas ni katika mtindo wa kitaifa, lakini pia  hata wale ambao hawaishi katika nchi hiyo ya Cuba na ambao wana mapenzi mema  wa kuweza kutoa msaada wao , anawakaribisha kusoma katika tovuti yao ya Shirika la Friends of Cáritas Cuba: http://www.friendsofcaritascubana.org.

30 May 2019, 14:40