Tafuta

Vatican News
Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume Nchi Takatifu anasema waamini nchi Takatifu wanashuhudia imani yao licha ya migogoro na vurugu zilizopo Askofu Mkuu Pizzaballa Msimamizi wa Kitume Nchi Takatifu anasema waamini nchi Takatifu wanashuhudia imani yao licha ya migogoro na vurugu zilizopo  (ANSA)

Pasaka Nchi Takatifu:Ask.Mkuu Pizzaballa:bado zipo kuta na migawanyiko ndani ya jumuiya

Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa Msimamizi wa Kitume wa Nchi Takatifu akihojiwa na waandishi wa habari Vatican News,wakati tunakaribia sikukuu ya Pasaka anasema,wakristo wanashuhudia kila siku matumaini yatokanayo na Kristo mfufuka,licha ya Jumuiya ya kimataifa kuchoka na migogoro ya waisraeli na Gaza kuishi kama siku ya Ijumaa Kuu!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu Mkuu Pierbattista Pizzaballa Msimamizi wa Kitume nchi Takatifu  akihojiwa na waandishi wa habari wa Vatica News, wakati wa tunakaribia sikukuu ya Pasaka, anabainisha kwamba katika maeneo yao ya Nchi Takatifu utafikiri kuna kuta na migawanyiko mingi, hata kati ya wakristo na ambao ni kati ya watu wa imani, kwa maana hiyo anathibitisha kwamba upo umuhimu kufanya kazi ya juu ya udugu. Hata hivyo pia  wametia sahini pamoja na Mapatriaki wengine na wakuu wa Makanisa ya Yerusalemu kwenye ujumbe ambao unalenga kusisitiza tamko lililotolewa huko Rabat na Baba Mtakatifu Francisko akiwa na Mfalme Mohammed VI. Ujumbe huo unasisitiza jinsi gani mji Mtakatifu unapaswa uwe wa amani na mapatano, wakishauri kuheshimu mikataba ya kisheria ya kidini na utumaduni huko Yerusalemu, aidha anasema, ujumbe huo  ni kuhusu utambulisho wa mji wao. Yerusalemu ni mahali ambapo Mungu alijionesha na mahali ambapo wayahudi, wakristo na waislam wanakua pamoja na walitoa muundo wa sura hiyo ya mji kwa karne nyingi na wito huo lazima unabaki vili vile! 

Mji usipoteze mojawapo na mambo msingi ya kiutamaduni

Ni mji ambao kama unaweza kupoteza moja ya mambo msingi kati ya wakristo, wayahudi na waislamu, watu wa dini na walei, mji unaweza kukosa sura yake  kamili  na ya dunia nzima ambao kwa hakika ndiyo muundo huo wa asili. Pasaka kwa wakristo katika  nchi Takatifu  awali ya yote ni kukutana na Yesu aliyekufa na kufufuka na hatupaswi kusahahu hilo. Pasaka siyo tu mazoea ya ibada, lakini ikiwa na maana ya kukaa hapo na kuelekeza hata matendo yao, mawazo yao na yale yote ambayo wanatamka. Aidha akielezea juu ya suala la kimataifa kuhusu nchi Takatifu amesema: Hata katika mantiki ya kimataifa utafikiri wameweka mji huo katika mpango wa pili wa juhudi zao za kutafuta suluhisho la waisraeli na wapalestina, kwa sababu inaonesha wamechoka sana na migogoro hiyo na masuala ya Yerusalemu ambayo utafikiri daima yanakuwa magumu kufikia upatanisho wa kweli. Na kwa upande wa waamini anasema: Yesu  ndiye fursa, ndiyo mategemeo ya kutazamia hali halisi na kuona ni wapi waanzie!

Notre-Dame: hakuna lililopotea!

Hata hivyo pia amegusia suala la tukio la moto kuchoma Kanisa Kuu la Notre- Dame, jijini Paris Ufaransa, kwa maana  Askofu Mkuu ametuma naye  ujumbe wake wa mshikamano kwa niaba ya Kanisa la Yerusalem kwa Patriaki, Askofu Mkuu wa Mji wa Ufaransa Michel Aupetit, kwa kusisitiza kuwa, picha ya moto itageuka kuwa ishara ya mwanzo mpya, kwa maana hakuna lolote lililopotea. Tangu Jumatatu mjini Paris kumekuwa na mwamko na hisia za umoja, matumaini na kutaka kuzaliwa upya hasa katika Juma Kuu.  Na hii ni kutaka kuweka msukumo mpya ambao unafanana na ule wa nchi Takatifu, anasema Askofu Mkuu Pizzaballa na zaidi anaamini kuwa, kila mahali wanapaswa kufanya kazi sana juu ya urafiki, udugu, mahusiano kati ya watu, juu ya kukaa kwa pamoja na juu ya uhusiano ambao unazungumziwa kwenye  Hati ya Abu Dhabi na katika hati nyingine nyingi ambazo ni maelekezo kamili, pia kama mtindo ambao unapaswa kuigwa na kufuatwa kwa ajili ya uwepo wetu kwa wakati ujao. Kwa upande mwingine anasema, iwapo  bado tunasubiri kutoka nje, hatujui ni kwa jinsi gani tunaweza kuona furaha. Iwapo tunataka kuzaliwa ndani  tunapaswa kuwa na maamuzi ya kiundani na maamuzi wazi, yenye msimamo na ndipo hapo inawezekana kuishi amethibtisha Askofu Mkuu Pizzaballa.

Gaza ni kama Ijumaa kuu

Ujumbe wa Mapatriaki na wakuu wa Kanisa la Yerusalemu, unatoa ushauri kwa waamini kuchota nguvu zaidi za kuadhimisha Pasaka hata mbele ya vurugu, uchungu, ukosefu wa usawa na ambao unakanyagwa hadhi ya binadamu.  Ujumbe huo, unawalenga sana jumuiya zao zinazoishi katika hali ngumu zaidi na ambamo muda huo, Askofu Mkuu Pizzaballa amefikiria watu wanaishi Gaza, kwa namna ya pekee pia hata ndugu wakristo ambao wanaishi karibu nao. Kama wakristo wa nchi Takatifu wana matatizo mengi, lakini hawapaswi kusahau wakimbizi wengi ambao wamewapokea katika eneo la majimbo, kwa mfano Yordani, bila kuwasahau  Siria na Iraq na hali mbalimbali nyingi za mateso yanayo wazunguka.

Matumaini yanayo zaliwa kutoka kwa Kristo Mfufuka

Kwa upande mwingine Pasaka ni kifo na ufufuko wa Bwana na kama wakristo wote tunaalikwa kutoa ushuhuda huo daima na bila  kuruhusu hata kifo na kipige ngumi, anasema Askofu Mkuu Pizzaballa. “Kifo hakina maana tu ya kufa kimwili, lakini hata maana ya kukaa hivi hivi bila kubadilisha maisha. Kutokana na hiyo  anasisitiza, kama  wakristo hatutaibadili dunia, hatutaibadili kwa hakikahata  hatima ya milioni mbili ya watu wanaoishi Gaza”. Anaongeza kusema, lakini kitu ambacho tunaweza ni  mahali tulipo  kutoa maana ya upendo  ambao tuna uwezo nao, hata kama ni kidogo lakini ni katika kuunda uhusiano wa aina ya pekee katika mwanga penye uwezekano. “Duniani kote anahitimisha, kuna vivuli vingi vya kifo na katika dunia nzima tunahitaji kupeleka ushuhuda huo mdogo, lakini wenye maana na wenye uamuzi thabiti wa ushuhuda wa matumaini yanayozaliwa na Kristo!

 

20 April 2019, 09:23