Vatican News
Wakimbizi  nchini Mexico wanatafuta kila usafiri wa miguu au wa kubahatisha kwa matumaini ya kuingia nchini Marekani Wakimbizi nchini Mexico wanatafuta kila usafiri wa miguu au wa kubahatisha kwa matumaini ya kuingia nchini Marekani  

MEXICO:Maaskofu wanashukuru msaada wa Papa kwa wahamiaji!

Maaskofu wa Mexico wameandika ujumbe wao kwa kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kujibu msaada wa dharura ya wahamiaji nchini mwao huku wakitoa hata taarifa zaidi ya hali halisi inayohusu misafara.Wakimbizi wanatembea maelfu ya kilometa kwa miguu na wakati mwingine kwa usafiri wa kubahatisha kwa matumaini ya kufika nchini Marekani.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Maaskofu wa Mexico wameandika ujumbe wao kwa kumshukuru Baba Mtakatifu kwa kujibu msaada wa dharura ya wahamiaji nchini mwao, wakati huo wakitoa taarifa zaidi ya hali halisi wanasema :“shukrani kubwa kwa Baba Mtakatifu Francisko tumepata jibu la maombi ya msaada wa mshikamano ili kukukabiliana na dharura ya wahamiaji kwa upendo wa kikristo katika nchi yetu”. Aidha wanaandikia kipeo kibaya cha kibinadamu, kinaendelea katika nchi yetu. Kuna idadi kubwa ya msafara wa wakimbizi wa nchi za Amerika ya Kati walioingia katika nchi yetu kuanzia mwaka 2018. Kwa mwezi Februari 2019 tu walikuwapo wahamiaja 75,000 na mwezi Machi 100,000 kwa mujibu wa habari kutoka mamlaka ya Amerika ambao walifika na kukatawa mpakani  kusini wakitafuta namna ya kufika Marekani.

Ni wahamiaji wengi wanaotaka kuingia nchini Marekani

Kati ya ndugu wahamiaji wanaokatisha nchini mwao, maskofu wanabainisha kuwa, wapo ambao wanaosubiri jibu la  maombi ya hifadhi ya ukimbizi katika nchi ya Marekani; kuna ambao wamerudishwa nyuma kutoka Marekani;kuna wale ambao wanatafuta kukatisha mpakani bila kuwa na vibali halali na wengine ambao wanatoka katika sehemu za Jamhuri ya nchi ya Mexco wakisubiri kupata fursa mpya ya kuingia nchini Marekani na hatimaye ambao wanatabaki moja kwa moja nchini Mexico.

Idadi kubwa ya mawakala na mashirika ya kidini wanasaidia wakimbizi

Idadi kubwa ya mawakala wa kichungaji katoliki maaskofu wanaandika, wanajaribu kuwasindikiza na kuwasaidia misafara hii ya wahamiaji katika safari ya kuelekea Marekani wakikimbia umasikini na ghasia wanazo kumbana nazo katika nchi zao asili. Kufika kwa misafara mipya ilitangazwa katika miezi ya mwisho, hivyo kipeo cha kibinadamu kitaendelea kuongezeka. Na kaka na dada wahamiaji ambao wamepokelewa katika makambi na ambao wanahudumiwa na Kanisa Katoliki, vilevile hata mashirika mengine mengi ya kiraia na makanisa mengine kwa kutoa  masaada wa kibinadamu, kimaadili na kiroho. Ni lazima kwa kiasi kikubwa na ubora wa kushirikiana kati ya nguvu za muundo wa kichungaji na kitaifa wa Kanisa Katoliki na Serikali zote, wanasema maaskofu, lakini pia wanabainisha kwamba, kwa bahati mbaya uhusiano huo haupo, hata kwa kiasi kinacho tamaniwa au kilichokuwa kimependekezwa mbele ya dharura hii ya asili.

Mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu baraza la maaskofu waliunda chombo 

Tarehe 15 na 16 Februari 2019 ulifanyika Mkutano wa Kitaifa wa vongozi wasimamizi wa nyumba za kukaribisha wahamiaji. Katika mkutano ulioandaliwa na Kitengo cha maendeleo fungamani ya watu cha Maaskofu na Mexico uliweza kusikiliza mahitaji msingi ya wakimbizi. Na mwisho wa mwezi Februari mwaka huu, maaskofu wanaandika kwamba, walialika kuunda chombo na  kushughulikia mipango kwa ajili ya kuwatunza wahamiaji wahitaji na ili sadaka iliyotolewa na Baba Mtakatifu yenye thamani za Dola 500,000 iweze kugawanyika kwa namna nzuri hasa ya kuweza kukidhi dharura ya wahamiaji na ufanisi mzuri katika nyumba zinazowakaribisha wahamiaji. Kati ya mipango 27 iliyopokelewa kutoka katika majimbo 16 ya nchi, mipango 13 imeidhinishwa.  Maskofu wanaomba serikali nchini Mexico na Marekani kuwapokea na kuwashirikisha maelfu ya wahamiaji walioko katika nchi yao, na vyombo vya habari waweze kutoa habari zenye malengo mema ya misafara ya wahamiaji ambao wanaendelea kufika na ambao wanaishi katika nchi zao, katika kuwatazama kwa upendo na huruma kaka  na dada wahamiaji wanaoteseka na wakati huo huo bila kufunga mioyo na kuendelea kuwasaidia. Mwisho wanamwomba Mama Maria wa Guadalupe awaombeee ndugu kaka na dada kwa mwanaye Yesu Kristo ili awaongezee nguvu katika safari yao.

 

 

 

30 April 2019, 14:44