Tafuta

Shirika la Mungu Mwokozi (SDS) wajulikanao Wasalvatoriani, wameweka mkataba  wa ushirikiano na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ili kupambana na Ukimwi Afrika Shirika la Mungu Mwokozi (SDS) wajulikanao Wasalvatoriani, wameweka mkataba wa ushirikiano na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ili kupambana na Ukimwi Afrika 

Makubaliano kati ya Wasalvatoriani na Jumuiya ya Mt.Egidio ili kupambana na ukimwi Afrika

Shirika la Mungu mwokozi au Wasalvatoriani na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,kwa pamoja wameweka mkataba wa kupambana dhidi ya Ukimwi Afrika.Ni makubaliano yaliyotiwa sahini wiki iliyopita 2019 mjini Roma ili kuwa na ushirikiano wa kuendesha mpango wao wa Dream katika nchi ambazo Wasalvatoriani wanatoa huduma.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Shirika la Mungu mwokozi SDS au wajulikano kama Wasalvatoriani na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,kwa pamoja wametia  sahini ya mkataba wa kuweza kupambana dhidi ya Ukimwi Afrika, janga ambalo bado linatishia dunia bila mchezo. Hayo ni  makubaliano yaliyotiwa sahini wiki iliyopita,  tarehe 26 Machi 2019 mjini Roma ili kuweza kujikita kuwa na  ushirikiano wa kuendesha mpango wao ujulikanoa  Dream katika nchi ambazo Shirika la Wasalvatoriani wanatoa huduma. Mpango wa Dream kwa upande wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio umenzishwa kunako mwaka 2002 kwa ajili ya kupambana na Ukimwi Barani Afrika.

Hata hivyo watangungua nchi Kenya mahali ambapo Wasalvatoriani wapi na baadaye nchini Tanzania kwa mujibu wa mratibu wa mipango kwa ajili ya Afrika uitwao Sofia Global, katika ofisi ya wasalvatoriani ambayo inajikita katika shughuli za misaada kimataifa, na ndiyo mahali ambapo wanafanyia mipango yao kwa ajili ya kuupanua. Vile vile anasema Mratibu kwamba hii ni habari njema katika mpango wa Chuo Kikuu cha Wasalvatorian (Jordan) kilichopo Morogoro Tanzania. Na baadaye, wanatarajia kwenda kisiwa cha Komoro mahali ambapo Askofu wake ni mwanashirikia wa Kisalvatoriani, kwa mujibu wa maelezo ya Mratibu wa mipango ya Sofia Global.

Katika ufafanuzi wa mpango huo wa Dream, Mratibu huyo anasisitiza kuwa janga la  Virusi vya Ukimwi inaonekana kusahuliwa taratibu na kumbe ni makosa makubwa ambayo yanaweza kujitokeza! Hata hivyo jambo zuri ambalo linaonekana katika vituo vya Jumuiya ya Mtakatifu Egidio nchini Msumbiji na Tanzania, ni yale mabadiliko ya dhati ya wagonjwa wa Ukimwi, kwa maana ya kutoka katika hali ya kuhisi kutelekezwa, na badala yake wagonjwa wenyewe kuwahamasha wengine waweze kujongelea tiba katika jumuiya zao binafsi, familia na jamii kwa ujumla. Kwa maana hiyo ni kuthibitisha kwamba mpango wa Drean wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, inakwenda sambamba na tasaufi ya wasalvatoriani ambao wanajikita kutoa huduma yao kwa  kushirikiana kati ya watawa na walei.

Hata hivyo, mpango wa Dream katika vituo vya Wasalvatoriani, unatazamia kwamba wahusika wa Mpango wa Dream wajikite kuonesha fahamu zao kwenye programu ambayo inaruhusu udhibiti kwa njia ya mitandao yenye lengo msingi wa wagonjwa wote waliosajiliwa na kuweza kupata huduma ya matibabu, pamoja na kutoa ripoti kuhusu madawa, hivyo uwezekano wa kupokea madaktari bingwa ambao wako Ulaya, Marekani na katika Ulaya ya kaskazini kuhusu  wagonjwa walio na matatizo zaidi au ambao wana matatizo ya afya huko Afrika. Hata hivyo pia utahakikishwa mchakato wa mafunzo ya kuendeleza rasilimali za binadamu, ambapo wataajiliwa katika vituo vya afya na  ambapo Wasalvatoriani wataweza kutumia katika programu hiyo.

02 April 2019, 15:45