Tafuta

Sasa kuna  toleo jipya la kitabu chenye jina:“Kuipaka rangi dunia:Ekolojia fungamani ya Papa Francesco"katika kutaka kumasisha mwangwi halisi wa Laudato Si' Sasa kuna toleo jipya la kitabu chenye jina:“Kuipaka rangi dunia:Ekolojia fungamani ya Papa Francesco"katika kutaka kumasisha mwangwi halisi wa Laudato Si' 

Toleo jipya la Kitabu:Ekolojia fungamani ya Papa Francisko!

Toleo jipya la kitabu chenye jina:“Kuipaka rangi dunia:Ekolojia fungamani ya Papa Francisko”,limetolewa baada ya miaka michache tangu kutangazwa kwa Wosia wa Laudato Si, kunako mwaka 2015.Hili ni toleo linalotaka kutoa tafakari ya pamoja na yenye furaha katika hali halisi ya maono ya Kanisa na msimamo wa kulinda na wazo la kiekolojia

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Baada ya miaka michache ya kutangazwa kwa Wosia wa Laudato Si’ (2015) sasa, limetolewa toleo jipya la kitabu chenye jina:“Kuipaka rangi dunia.Ekolojia fungamani ya Papa Francisko”. Lengo la kitabu hiki ni kutaka kutoa mwamko hai wa tafakari ya pamoja  na yenye furaha hata katika  hali halisi ambayo imejionesha kwenye maono ya Kanisa na msimamo wake thabiti wa kulinda na wazo la kiekolojia.

Toleo jipya ni mkusanyiko wa hotuba nyingi za tafakari kuhusu Wosia wa Laudato Si

Toleo la kitabu kipya linakusanya hotuba nyingi za siku ya tafakari ya mafunzo katika Mkutano uliojikita kutafakari na kusoma kwa karibu Wosia wa Laudato Si, hususani Mkutano uliofanyika mjini Yerusalemu mwezi machi 2018 na ambao uliongozwa na  tema  ya “Ekolojia fungamani ya Papa Francisko kwa ajili ya kutunza nyumba  ya pamoja”. Mkutano huo uliandaliwa na Ndugu mdogo Giorgio Vigna mhusika mkuu wa Tume ya Haki, Amani na fungamani ya  kazi ya uumbaji kwa upande wa Shirika la Mtakatifu Francisko, Nchi Takatifu. Toleo la kitabu hicho kama anavyoeleza ndugu mdogo Vigna, katika utangulizi wake anasema, ni mkusanyiko wa  sauti nyingi, hususani wa Padre Francesco Patton Msimamizi wa nchi Takatifu, ambaye anawakilisha sababu  na hatima ya mkutano huo, uliofanyika nchi Takatifu; Beatrice Guarrera, mwandishi wa habari katika Nchi Takatifu  kutoka Yerusalem ambaye alitoa  utangulizi wa Wosia wa  Papa na kuelezea ufahamu wa wosia huo kwanza na sehemu zake zote; Mohammed S. Dajani Daoudi Profesa wa Chuo Kikuu, nchini Palestina na mdau wa amani, ambaye alionesha nini maana ya muungano kati ya ujumbe wa Papa Francisko na mafundisho mengine yatokanayo na utamaduni wa kiislam.

Mkuu wa kiyahudi David S. Rosen wa Yerusalemu ambaye alijikita kuelezea  ugunduzi wa ekolojia fungamani na kama unavyojionesha katika Tolah, yaani Kitabu Kitakatifu cha Wayahudi na tamaduni ya kiyahudi; Kardinali Peter K. Turkson, Rais wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya watu, aliyejikita kuelekeza njia na maana halisi iliyo ndani ya Wosia wa Baba Mtakatifu Fracisko na aliye pendelea kuwaelekeza kila mkazi wa Nchi Takatifu, bila ubaguzi wa utamaduni au dini; na hatimaye mchumi Stefano Zamagni, rais mpya wa Baraza la Kipapa la Elimu ya Sayansi jamii ambaye alijikita kutoa  baadhi ya maswali mengi ya kutafakari kuhusu nafasi ya huruma katika maendeleo fungamani ya binadamu!

Baadhi ya masuala yanayokubaliwa na dini zinazo sadiki Mungu mmoja

Katika picha ya hali halisi ya Yerusalemu, wataalam na kati yao wa dini inayo sadiki  Mungu mmoja, wanakubaliana  na mambomuhimu ya Wosia ulioelekezwa na Baba Mtakatifu Francisko katika mambo kama yafutayo: “Uhusiano wa karibu kati ya maskini na udhaifu wa sayari; imani ya kwamba, kila kitu duniani kinao uhusiano wa karibu; kukosolewa kwa dhana mpya na aina za nguvu inayotokana na teknolojia;  mwaliko wa kutafuta njia nyingine za kuelewa uchumi na maendeleo; thamani ya kila kiumbe; maana  ya ubinadamu na ekolojia; haja ya kuwa na mjadala wa kweli na wa uaminifu; jukumu kubwa la sera za siasa za kimataifa na za nchi mahalia; utamaduni wa kibaguzi na pendekezo la mtindo wa kuwa na maisha mapya” (Ls 16).

Aidha katika suala la  haki msingi kwa ajili ya amani na ekolojia ambavyo vinakwanda pamoja na maono ya Baba Mtakatifu Francisko, vinafikiriwa kuwa fungamani, anasema Ndugu mdogo Giorgio Vigna na ndiyo kitovu cha matendo ya kuhamasisha na kuelekezwa kwa siku zile za utafiti na majadala; na sasa zimeweza kwa hakika kuwekwa katika toleo jipya la kitabu, hasa baada ya kusikilizwa na kutakariwa, lazima kufuata katika jitihada binafsi, kama anavyosisitiza msimamizi wa Nchi Takatifu. Hata hivyo anasema,hatua ya uamuzi wa mwisho itakuwa juu ya kila mmoja katika kujikita kwenye uwajibikaji wa mabadiliko, hasa mabadiliko ya mawazo binafsi na mtindo wa maisha, katika uhusiano wa uumbaji. Mabadiliko hayo yatahitaji baadaye uamuzi wa kina ndani ya jumuiya za kidini na raia wake mahali popote!

Wosia wa Laudato Si umezaa vichipukizi vingi duniani kote

Hata hivyo Ndugu mdogo Giorgio Vigna anafafanua kuwa, katika Wosia  wa Baba Mtakatifu, umeweza kwa sasa kutoa vichipukizi vingi sana kila mahali duniani, hasa kwa kuanzishwa mambo mengi yanayojikita kutafsiri misingi ya matendo ya dhati na zaidi kuwaalika watu wote kwa upya ili waweze kuweka kipaumbele juu ya utunzaji wa mazingira nyumba yetu ya pamoja. Katika Wosia wa Laudato Si, Baba Mtakatifu Francisko zaidi anasisitiza kuwa, dini zinaweza kutoa utajiri wa aina yake, katika kutafakari ekolojia fungamani na maendeleo kamili ya binadamu. Katika roho hiyo ya kidini ndipo imezaliwa kitabu, ambacho wataalam wengi wa ngazi za juu na viongozi wakuu wa dini tatu kutafakari kwa mapana na marefu kuhusu tema na mwongozo fungamani il kuweza kulinda ardhi au mazingira nyumba yetu ya pamoja. Ni kitabu muhimu sana, ambacho kinatoa msukumo wa kutafakari kwa kina na zaidi Wosia wa Laudato Si, ili uweze kusomwa na kufanyiwa utafiti kila kona, kuanzisha mambo mengi mapya na hatimaye Wosia huu upeleke mwangwi katika maandishi na katika dini kwa watu wa imani tofauti wa kisayansi na watu wa wakati wetu!

20 April 2019, 10:40