Tafuta

Wakristo duniani wanazidi kuongezeka tangu mwaka 2010-2017 na zaidi katika bara la Afrika Wakristo duniani wanazidi kuongezeka tangu mwaka 2010-2017 na zaidi katika bara la Afrika  

Idadi ya wakatoliki duniani imeongezeka tangu 2010-2017!

Idadi ya wakatoliki duniani kote imeongezeka kwa mujibu wa takwimu za Kanisa Katoliki kuanzia 2010-2017.Lakini ongezeko hili linatofautiana hali halisi ya kidunia. Ongezeko zaidi kwa data za kidunia ni Bara la Afrika kwa 26,1%; Asia 12,2%;Australia 12,4% wakati sehemu mbili za kijiografia ni ndogo kwa 0,3% Ulaya na 8,8% Amerika.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Uso wa Kanisa umebadilika kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wakatoliki hadi kufikia wakatoliki bilioni 1,3 duniani, lakini wakati huo huo inarekodiwa kushuka kwa miito ya utawa na ukuhani. Kwa miaka saba, watawa wamepungua kwa kiasi cha asilimia 10% na wakati huo huo ongezeko linaonekana kwa walei hai  ambao kati yao ni Makatekista na wamisionari. Katika mtazamo huo, taarifa inathibitisha kwamba ndiyo unawezekano wa kuona  uso mpya wa Kanisa katika kambi za kimisionari. Hii ni taarifa kutoka Gazeti la Ossevatore Romano ambalo limefanya tathimini ya idadi ya wakatoliki kuanzia mwaka 201-2017.

Bara la Afrika linaonesha ongezeko la asilimia 26,1  

Taarifa kutoka Gazeti la Osservatore Romani linaandika kwamba idadi ya wakatoliki duniani, imeongezeka kati ya mwaka 2010- 2017 kutoka asilimia, 9.8  na kukaribia milioni 1. 196 kwa mwaka 2010 hadi milioni 1.313 kwa mwaka 2017. Lakini ongezeko hili linatofautiana katika hali halisi kiduniani. Inarekodiwa hata ongezeko zaidi kwa data za kidunia katika Bara la Afrika kwa asilimia 26.1, Asia asilimia 12.2, Australia asilimia 12.4 wakati sehemu mbili za kijiografia zinatofautiana kutokana na thamani ndogo ya asilimia 0.3% ya Ulaya na ile asilimia zaidi ya 8.8 kwa upande wa bara la Amerika. Kuanzia mwaka 2010 mapadre wanawakilishwa katika mantiki ya dunia kuwa na utofauti, kwa maana ya kuonesha ongezeko kubwa kwa mwaka 2014 lakini baadaye kuendelea kushuka.

Hali ya kupungua kwa miito pia ni kwa upande wa watawa wa kike

Hata hivyo hali ya kuendelea kushuka zaidi inajionesha kwa  upande wa watawa wa kike na kiume. mwaka 2017 kulikuwa na jumla ya watawa 648,910 kwa kipimo; ikilinganishwa na mwaka 2010, kikundi hicho kilirekodiw kushuka kwa asilimia 10.1 duniani kote. Kupungua huku kunahusisha mabara matatu (Amerika, Ulaya na Oceania), na tofauti hasi, ikiwa ni pamoja na umuhimu  wa asilimia 16.3% katika bara la Amerika, asilimia  19.1% katika bara la Ulaya na asilimia 19.4% katika bara la Australia. Bara la Afrika na Asia, kinyume chake ongezeko lake ni zaidi ya asilimia 1.,5 ikiwa ya kwanza  na asilimia 4.6%  ikiwa ya pili. Kipeo cha kushuka  katika miaka kinawahusu watawa waliofunga nadhiri kulingana na utafiti uliofanyika na kuchapishwa na gazeti la Vatican.

Idadi ya walei wamisionari na makatekista wanaongezeka

Vile vile taarifa za takwimu hizi zinaonesha kuwa idadi ya wamisionari walei kwa upande mwingine imeongezeka kutoka vipimo vya 335,502 kwa mwaka 2010 hadi kipimo cha 355,800 kwa mwaka 2017, kwa ongezeko la asilimia 6.1 katika miaka saba. Pia kuna ongezeko kubwa la makatekisti, ambao wanaunda  kiukweli wa halisi zaidi, ya idadi ya ongezeko kwa  maana kwa  uwiano wa kipimo zaidi cha  milioni 3.12 mwishoni mwa 2017. Asia na Afrika zinaonyesha mienendo mizuri ya kuendelea na uhai wake katika miito na  viwango vya ukuaji mkubwa wa harakati za kimisionari, wakati Ulaya na Amerika zinaonyesha kushuka kidogo!

29 April 2019, 16:17