Tafuta

Vatican News
Kanisa lazima liwepo katika dunia ya teknolojia ya kidigitali kwa ajili ya kueneza Injili kwa kadiri iwezekanavyo Kanisa lazima liwepo katika dunia ya teknolojia ya kidigitali kwa ajili ya kueneza Injili kwa kadiri iwezekanavyo 

AMECEA:Kanisa lazima liwepo na kujiandaa katika dunia ya kiteknolojia ili kuinjilisha!

Katika dunia ambayo teknolojia inazidi kupanuka,Kanisa lazima liwepo na kujiandaa ili kutumia mitindo hiyo mipya kwa ajili ya uinjilishaji.Ni uthibitisho wa Askofu Mkuu wa Philip Anyolo,Rais wa Tume ya Mawasiliano ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki,wakati wa Kozi ya mafunzo kuhusu dunia ya digitali mjini Nairobi,Kenya.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Askofu Mkuu wa Philip Anyolo, Rais wa Tume ya Mawasiliano katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki, katika fursa ya Kozi ya mafunzo kuhusu dunia ya digitali, amewashauri kwa niaba ya maaskofu wa AMECEA,waandishi wa habari na vyombo vya habari katoliki kwamba, wazungumze daima ukweli juu ya masuala mbalimbali yaliyopo ndani ya jamii, na jukumu lao ni kuhakikisha wanatoa Habari Njema na iweze kuonekana katika jamii ya kisasa. Kozi hiyo imehitimishwa hivi karibuni  katika Kituo cha Huduma ya Mafunzo ya Vijana cha Don Bosco mjini Nairobi Kenya. Shirika la habari za kimisionari Fides, linaeleza kuwa, Askofu Mkuu Anyolo amethibitishwa kwa vijana washiriki kutoka katika maeneo mbalimbali ya nchi kwamba, dunia ambayo teknolojia inazidi kupanuka, Kanisa lazima liwepo na kujiandaa ili kutumia vyombo hivyo kwa ajili ya uinjilishaji kadiri ya uwezo wake wote.

Askofu Mkuu Anyolo, pia amekukumbusha washiriki wa kozi hiyo kuwa,hawali ya yote Mungu ndiye kwanza mpasha habari na kwa maana nyingine kama mtoa habari . Kwa kuthibtisha hili anasema,tangu mwanzo alikuwa anawasiliana na Adamu na Eva. Na kwa maana hiyo hata leo Mungu yupo mahali popote anawasiliana na ubinadamu kwa namna nyingi. Ni jukumu letu sasa  anasisitiza, kumsikiliza! Na zaidi amesisitiza kwamba katika dunia ya sasa, ambayo inazidi kukuza na kuenea kwa teknolojia kwa njia  nyingi za mawasiliano na mikondo mingi ya mawasilianoa, vyombo vya habari pia vina kazi muhimu hata kwa Kanisa Katoliki na hasa  ile ya kujikita katika mahusiano na kuunganisha Kanisa katika  ulimwenguni, na ili kueneza Injili hara iwezekanavyo.

Na hatimaye Askofu Mkuu Anyolo , ameaalika  waandishi wa habari katoliki  wawe na taaluma inayofaa na ubunifu, kwa ajili ya kuweza kutoa umakini  juu ya uzalishaji na utoaji wa habari za kweli, na kwa kushirikisna na wadau wa kichungaji wakati wa kukusanya na kushirikishana habari kwa njia ya vyombo vya habari na kwa maana nyingine ili kuweza kutangaza sura ya dhati ya Kanisa mahalia. Hata hivyo vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Kanisa katoliki viptakiwa kuwa mstari wa mbele kuangazia maswala ya Kanisa na jamii katika hali halisi na ya kweli. Umuhimu wa vyombo vya habari vya Kanisa katoliki kwa hakika ni lazima viwe na ushirikano baina yao ili kutoa taswira dhabiti kuhusu msimamo wa Kanisa katika maswala mbali mbali yanayokumba Kanisa mahalia lakini pia hata katika ulimwengu kwa ujumla. Hii inatambulika wazi kwamba vyombo vya habari Katoliki licha ya tasaufi yake na ambayo ni ya kijamii sharti viwe katika mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa amani, upendo,ushirikiano na mshikamano.

 

03 April 2019, 14:35