Tafuta

Kardinali Nzapalainga wa Jimbo Kuu la Bangui Afrika ya Kati,aliadhimisha misa kwa wafungwa 500 katika jiji kuu la nchi yake wakati wa Pasaka Kardinali Nzapalainga wa Jimbo Kuu la Bangui Afrika ya Kati,aliadhimisha misa kwa wafungwa 500 katika jiji kuu la nchi yake wakati wa Pasaka 

Afrika ya Kati:Ni wajibu wetu kuonesha huruma na upendo kwa wafungwa!

Kardinali Dieudonné Nzapalainga Askofu Mkuu wa Bangui nchini Afrika ya Kati aliadhimisha Misa Takatifu ya Pasaka kwa wafungwa 500 katika Gereza la Ngaragba kwenye mji mkuu wa nchi na wakati wa mahubiri yake amesema ni wajibu wao kuonesha hata wao huruma na upendo!

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Tare 21 Aprili 2019 Kardinali Dieudonné Nzapalainga Askofu Mkuu wa Bangui Afrika ya Kati ameadhimisha Misa Takatifu ya Pasaka kwa wafungwa 500 katika Gereza la Ngaragba kwenye mji mkuu wa nchi na wakati wa mahubiri yake amesema ni wajibu wetu kuonesha hata wao huruma na upendo.

Siku maalum ya Pasaka waamini wa Bangui waliandaa zawadi kwa ajili ya wafungwa

Hata hivyo katika kuonesha siku maalum ya Pasaka, waamini wa Mji Mkuu Afrika ya Kati, huko Bangui wamejikusanya kwa pamoja na kuandaa chakula na zawadi ili kuwapelekea wafungwa nao waweze  kuonja  furaha  kama ndugu kaka na dada, anasema Kardinali Nzapalainga. Vile vile anabainisha kwamba, wametumia fursa ya kipindi hicho kuwabatiza wale wote ambao kwa utashi wao wameamua kubadilisha maisha yao ya kuishi. Kwa njia hiyo Kardinali, amewaomba wahusika wa Gereza la Ngaragba, waweze kuwasaidia wafungwa ili wasikandamizwe na badala yake wawachukuliwe vema na kuheshimiwa  hadhi yao kama binadamu! Na baada ya mahubiri yake, Kardinali Nzapalainga ametoa sakramenti ya Ubatizo kwa wafungwa 25

Mvua zinaponyesha, wafungwa wengi wanaloa nje kutokana na kukosa nafasi

Katika siku hiyo mwakilishi  wa wafungwa wa Ngaragba, amethibitisha juu ya hali halisi  ya maisha ya gereza kuwa magumu sana na kwa namna ya pekee hali mbaya ambayo baadhi yao hutumikia kifungo na hukumu zao lakini kwa mateso. Mvua zinaponyesha, wanalazimika kubaki nje na kunyeshewa mvua kwa sababu nafasi hazitoshi ndani ya gereza. Kutokana na hiyo wanaomba msaada ili majengo yaweze kukarabatiwa na kupanuliwa.  Magereza hiyo ilijengwa kunako mwaka 1947 ikiwa na uwezo wa kuwahifadhi wafungwa 400, lakini kwa sasa, magereza hiyo ya Ngaragba ina wafungwa zaidi ya maradufu.(Agenzia Fides).

29 April 2019, 15:43