Ziara ya Papa Francisko jijini Rabat, Marocco tarehe  30 -31 Machi 2019 Ziara ya Papa Francisko jijini Rabat, Marocco tarehe 30 -31 Machi 2019 

Wakristo wa Morocco wanaomba kuwa na uhuru wa dini

Ikiwa bado wiki mbili Baba Mtakatifu Francisko aweze kutembelea Morocco tarehe 30-31 Machi 2019, Kamati ya wakristo imemtumia barua ya wazi ikiomba Vatican kuingilia kati kuhusu mada ya uhuru wa dini nchini humo

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Bado wiki mbili Baba Mtakatifu Francisko atembelee nchini Morocco, katika ziara inayotarajiwa  tarehe 30-31 Machi na wakati huo Kamati ya kikristo nchini Morocco imemtumia Baba Mtakatifu barua ya wazi kwa kuomba kuwa Vatican ingilie juu ya tema ya  ya  uhuru wa dini katika nchi ambayo wanathibitishwa inakiukwa.

Wabatizwa katika nchi hiyo wanawakilishwa na asilimia 1.1% tu ambayo ni watu karibia 380,000 kati ya wakazi milioni 33,6 ambao sehemu kubwa ni dini ya kiislam na wakristo wali wengi ni wa madhehebu ya kiinjili. Katika brua ya wazi uliyotangazwa na Gazeti la kila siku “Al Massae” na baadaye kupelekwa kwa Shirika la habari za kimisionari Fides inaeleza wazi juu ya baadhi ya ukiukwaji wa uhuru wa dini ya wakristo na Kamati hiyo inashutumu vikali, huduma ya usalama nchini Morocco kwa sababu ya kuwatesa wakristo kutokana na matukio yanayoendelea hata kuwakamata bila sheria.

Aidha, Kamati hiyo inasema kuwa baadhi ya maafisa wa polisi nchini Morocco wamewamatwa, na kuwatesa vibaya hata kunyimwa hati za utambulisho wa badhi ya  watu, kwa sababu ya kukikiri adharani imani ya dini yao au baada ya kwenda katika sala kwenye makanisa yao ya siri. Vile vile Mamlaka imefukuza wageni kwa kutuhumiwa kuwa ni wafanya propaganda. Kamati inaunga mkono Chama cha cha Haki za kidini na Uhuru,Morocco na Chama cha Haki za Binadamu nchini Morocco lakini vyombo ambavyo havijulikani rasmi kwa Taifa hilo na kwamba, vinalinda uhuru wa kidini, vinaorodhesha kila aina ya ukiukwaji na kuwakaribisha Waashii,Wabaddi  Wahmadis na Wakristo.

Hata hivyo barua inakiri kuwa Mfalme Mohammed VI anaitambua Kamati hiyo  na amekuwa akipeleka mbele mipango muhimu iliyoanzishwa na kamati hiyo  ili  kufanya Morocco iwe nchi yenye kuvumilia. Licha ya hayo barua pia inasema kwamba:hatupaswi kusahau juu ya Mkutano wa haki za dini zilizo na wafuasi wachache katika nchi za Kiislam, uliofanyika mwaka 2016. Japokuwa na mkutano  lakini  bado kuna viongozi wengi nchini Morocco ambao huchangia kubagua wakristo!

 

19 March 2019, 14:13