Vatican News
Kanisa Kuu la Rabat huko Marocco wanamsubiri Baba Mtakatifu Kanisa Kuu la Rabat huko Marocco wanamsubiri Baba Mtakatifu 

Papa Morocco:mazungumzo na waislam na mkutano na wahamiaji

Saa 8 masaa ya Ulaya,Baba Mtakatifu Francisko anatarajia kuwasiri katika uwanja wa ndege wa Rabat nchini Mrocco,mahali ambapo atakutana na watu katika uwanja wa Hassan, atatembelea jengo la Kifalme na Taasisi ya mafunzo ya amani iliyoanzishwa na Mhammed VI kwa ajili ya kutaka kupambana dhidi ya itikadi kali za kiislam

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Baba Mtakatifu atetelemka katika uwanja wa ndege wa Tour Hassan II, jina la mfalme wa Morocco aliyefariki kunako 1999 na ambapo Mtakatifu Yohane Paulo II alitembelea huko Casablanca miaka 33 iliyopita akiwa ni papa wa kwanza kutembelea ardhi hiyo katika moyo wa Rabat na  mji mkuu wa Falme hiyo. Hata hivyo katika nchi hiyo wanamsubiri kwa furaha kubwa kumpokea Baba Mtakatifu Francisko!

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko wa njia ya video amegusia juu ya undugu kati ya waislam na wakristo na ambapo anathibtisha kwamba dunia kwa hakika inahitaji amani na udugu, katika kuheshimiana tofauti zote. Ujumbe huo umeweza pia kutangazwa kwa njia ya vyombo vya habari vya Taifa la Morocco ikiwa na tafsiri ya lugha ya kiarabu. Kutokana hiyo, hata Padre Manuel Corullòn, ndugu mdogo mfransiskani na ambaye ni msimamizi wa maandalizi ya  maadhimisho ya liturujia Papa katika ziara hii ya kitume Morocco anathibitisha kwamba ujumbe wake umepongezwa na wengi.

Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe kwa njia ya video anasema, kwa kufuata nyayo za mfuasi wake Yohane Paulo II, anakwenda kama mhujaji wa amani na udugu, ambao unahitajika sana katika dunia. Aidha anathibitisha kwamba, kama wakristo na waislam wanaamini katika Mungu mmoja Muumbaji na wa huruma ambaye  aliumba watu na kuwapatia dunia ambayo wanaishi ndugu wote, katika kuheshimiana tofauti na kusaidiana katika mahitaji. Yeye aliwakabidhi wao ardhi na nyumba yetu ya pamoja ili kuilinda kwa uwajibikaji na kuitunza kwa ajili ya kizazi kijacho.

Vile vile  Baba Mtakatifu anaongeza kusema, itakuwa furaha kubwa kwake, pia kushirikishana moja kwa moja misingi hiyo aliyoitaja katika mkutano utakaofanyika huko Rabat. Na zaidi katika safari hii itakuwa kwake fursa kubwa ya kutembelea jumuiya ya kikristo iliyopo nchini Morocco, ili kuwatia moyo katika safari yao. Na kama itakavyo kuwa ile ya kukutana na wahamiaji, ambao anathibitisha, wanawakilisha watu katika kujenga kwa pamoja dunia ya haki na yenye mshikamano. Kwa kuhitimisha, anawashukuru wazalendo wote wa Marocco kwa moyo wote kuanzia sasa kwa ajili ya makaribisho yao wanayo msubiri na zaidi kwa ajili ya sala zao, akiwahakikishia naye kuombea nchi yao pendevu.

30 March 2019, 10:03