Rais wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Katoliki Duniani anasema tunawezaje kuthibitisha wanawake ni wahamasishaji wa matumaini iwapo bado majeraha yaliyofunguka? Rais wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Katoliki Duniani anasema tunawezaje kuthibitisha wanawake ni wahamasishaji wa matumaini iwapo bado majeraha yaliyofunguka?  

Ujumbe wa Rais wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Katoliki Duniani

Ujumbe Rais wa Rais wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Katoliki Duniani katika kilele cha maadhimisha ya Siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2019 unaongozwa na mada ya wanawake ni wahamasishaji wa matuamaini.Anawataka wanawake wajikite zaidi kuhamasisha matumaini katika sayari iliyo jaa mambo mengi ya uharibifu!

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Ujumbe wa Rais wa Umoja wa Mashirika ya Wanawake Katoliki Duniani (UMOFC), Dk. María Lía Zervino Servidora katika fursa ya Siku ya Wanawake Duniani 2019 ambayo inaadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 mwezi machi. Ujumbe wake umeongozwa na mada wanawake ni wahamasishaji wa matumaini. Dk Servidora anataja mambo mengi ambayo yanaikumba jamii katika sayari kuwa: Haya ni majeraha ya Yesu katika ulimwengu wa leo: uhamiaji wa watoto bila kusindikizwa, utengenisho wa kulazimishwa wa familia; wakimbizi kwa sababu ya vita na migogoro ambayo inakumba binadamu jatika kuishi; biashara ya watu kwa lengo la ukahaba, kazi isiyostahili, biashara ya viungo vya binadamu, uzazi wa kubadilishana; waathirika wa biashara ya silaha na madawa ya kulevya; wanawake waliojeruhiwa, wanaonyanyaswa, wanaobagulia na utamaduni dume; utamaduni haribifu unaotaka utoaji mimba na kupunguza watu zaidi walio maskini, ukosefu wa ugawaji sawa wa utajiri na rasilimali; familia ambazo hazina makazi wala elimu, bila chakula na bila kazi na wakati  sayansi na teknolojia zimewekwa katika ekolojia fungamani ili kuwezesha kuishi kindugu na kutunza mazingira nyumba yetu ya pamoja.

Asilimia 71% ya watu milioni 40 leo hii wanateseka na mitindo mipya ya utumwa

Wanawake wanaunda asilimia 71% ya watu milioni 40 leo hii wanateseka na mitindo mipya ya utumwa. Wakati huo huo anasema,  sisi tunaalikwa kuwa wahamasishaji wa matumaini. Kwa namna hiyo anaongeza, wanahitaji jamii zetu na Kanisa, wanawake wenye uwezo wa kuangaza huruma  kutoka katika tumbo lenyewe; wanawake ambao wanatafuta kutoa maisha na siyo kufuta au kupunguza kamwe na ambao wanakwenda kukutana na wale ambao wanateseka na kuwasindikiza wenye kuhitaji zaidi. Wanawake wanaotenda  kwa njia ya upendo wa kimama na wenye uwezo wa kutoa sadaka yao kwa ukimya na wabunifu wa hali ya juu, ni wanawale ambao wanainjilisha na kutumia lugha na ishara ya huruma, wanwake ambao wanatoa faraja katika majereha yaliyofunguka ya Bwana wetu.

Ni wanawake wanaotenda kwa dhati na siyo kulipiza,kwani wanauhakika wa kubadili dunia

Ni wanawake ambao wanatenda sio kwa njia ya kulipiza, bali wakiwa na uhakika, kwamba wanaweza kubadili dunia ambayo unatuzunguka na ambamo sisi sote ni wawajibikaji. Kwa utambuzi ni jamii ambyo inatafuta kujenga siku hasi siku, pole pole  kwa njia ya kazi ya kushirikiana na wanaume na wanawake sawa na hadhi na utofauti katika utambulisho wao. Kwa mwaka 2019  anaongeza Bi Servidora kuwa: tunaweza kutoa faraja kadiri ya kipimo cha majeraha yaliyofunguka kwa yule ambaye amesulibiwa, kwa sababu sisi ni wabebaji wa matumaini. Na iwapo tutachangia kuendeleza kila siku upendo mbunifu, tutakabiliana kwa nguvu dhidi ya vishawishi vya kushusha mikono yetu na kujitahidi katika matendo yetu binafsi na kijumuiya! Iwapo tutashirikishana mawazo na kufanya kazi na wanaume ambao nao wanayo shauku ya kutunza dunia kama familia yao binafsi na wakati huo huo ni katika kuilinda jumuiya zaidi iliyo athirika. Kama anavyo shauri Baba Mtakatifu Francisko, tuweke matendo yetu ya  dhati kwa furaha na kujitoa kwa ajili ya mazingira pamoja na udogo ambao unaweza kuwapo ili kutafuta suluhisho la  majanga ambayo leo hii  yanaikumba. Wanawake twende mbele na tuwe wahamasishaji wa matumaini! anahitimisha ujumbe wake.

 

 

08 March 2019, 13:20