Tafuta

Wajumbe wa bodi tawala ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA) Wajumbe wa bodi tawala ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Afrika Mashariki (AMECEA) 

Uganda:Kozi kwa zaidi ya waseminari 300 kuhusu jumuiya ndogo ndogo za kikristo

Kitengo cha shughuli za kichungaji cha AMECEA kimaeandaa kozi hivi karibu kuhusu kuhamasisha na kukuza Jumuiya ndogo ndogo za kikristo katika kanda.Kozi hiyo ilifanyika katika Seminari kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Maria huko Ggaba nchini Uganda na kuudhuliwa na zaidi ya waseminari 300 wa Uganda

Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kitengo cha kichungaji cha Amecea kimaeandaa kozi hivi karibu kuhusu kuhamasisha na kukuza Jumuiya ndogo ndogo za kikristo katika kanda. Kozi hiyo ilifanyika katika Seminari kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Maria huko Ggaba nchini Uganda. Nia kuu ua kazoo hiyo ni kutaka kuwa na mtindo mmoja katika uendeshaji wa shughuli  za kichungaji katika jumuiya ndogo ndogo za kikristo katika Kanda zote za Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika Mashariki (AMECEA). Kozi ilianza tarehe 28 Februari na kumalizika tarehe 4 Machi 2019 katika Seminari Kuu ya Gbaga na  wanafunzi hao pamoja na majirani zao kutoka Seminari Kuu ya  Mtakatifu Mbaaga, Jimbo Kuu la Kampala. Kutoka katika Seminari Kuu ya kitaifa ya Mtakatifu Maria wanafunzi walikuwa ni 212 pamoja na waseminari Kuu ya Mtakatifu Mbaaga wakiwa ni 183 pamoja na wakufunzi wao na wahudumu wa seminari hizo.

Naye Mkurugenzi wa kitengo cha kuchungaji cha Amecea Padre Emmanuel Chimombo aliyeandaa kozi hiyo kwa waseminari amesema kuwa kama mapadre watarajiwa wanahitaji kuwa kuwa na nyenzo ya uelewa mkuu ili waweze kuwa wahudumu wa jumuiya zao watakazo kuwa wamekabidhiwa. Jumuiya ndogo ndogo za kikristo siyo programu au mpango bali ni njia ya maisha ya kila mkatoliki mbatizwa. Hawa wanajilezea kama Kanisa katika ukaribu kwa sababu wanabadili parokia kuwa na muungano wa jumuiya ndogo ndogo, amethibitisha Padre Chimombo na kuonesha kuwa, wazo la idadi  inapaswa kuwa 15 na kwa maana ya kitovu cha jumuiya  ni Neno la Mungu na  kama waamini wanapasa wakutane angalau kila mwisho wa wiki kutafakari juu ya Neno la Mungu, hasa Injili ya Jumapili inayofuata kuiweka katuka matendo ya maisha yao.

Na kwa mujibu wa Padre John Baptist Kaganda, Mkurugenzi wa kichungaji Kitaifa wa Baraza la maaskofu Uganda (UEC) anasema, tangu mwaka 1973 mkutano wa mwaka wa Amecea ulijadili na  kuthibitisha kuwa jumuiya ndogo ndogo za kikristo zitakuwa kama njia ya kuendeleza mbele Kanisa, na liwe hali halisi mahalia ambapo liwe ni Kanisa linalojitegemea, linajihudumia, lenye kujitangaza na kujisadia lenyewe! Hata hivyo amebainisha kwamba kwa upande wa Uganda bado kuna majimbo ambayo jumuiya ndogo ndogo katoliki bado hazijasimika mizizi yake kwa dhati  na kwa maana hiyo bado kuna haja kubwa ya kuhamasisha na kukuza Jumuiya ndogo ndogo katoliki kama mpango wa kichungaji wenye kupewa kipaumbele.

Ni lazima kuunda miundo na maana thamani yake ya lazima katika  kukuza jumuiya ndogo ndogo za kikristo, kuzipanua katika majimbo ambapo kila mmoja anaitwa kujihusisha kwa ari ili kuzikuza  katika Kanisa mahalia, ameshauri Padre Kaganda. Vilevile taarifa zinasema kuwa AMECEA ilikuwa imesha andaa kozi nyingine kama hiyo  kwa wasemnia katika Majimbo makuu ya Nairobi na Nyeri nchini Kenya. Kozi hii ilisaidiwa na Seminari Kuu ya Kitaifa Ggaba, Kitengo cha kichungaji cha AMECEA na wafadhili binafsi. Kozi hii mara nyingi zinaombwa na waseminari wenyewe. Lakini licha ya waseminari kuomba pia  kozi nyingine ambazo zimefanyika kijimbo ni kutokana na maombi ya maaskofu. Nchini Uganda, Kitengo cha kichungaji cha Amecea kimendesha hata kozi nyingine katika Jimbo Kuu la Tororo na katika makambi ya wakimbizi kutoka Jimbo la Arua na Jimbo Kuu la Gulu.

 

06 March 2019, 14:44