Licha ya sahini ya makubaliano ya amani nchini Sudan, hali halisi bado inaendelea kuwa ya ghasia na vurugu Licha ya sahini ya makubaliano ya amani nchini Sudan, hali halisi bado inaendelea kuwa ya ghasia na vurugu 

Maaskofu Sudan Kusini wanasema mkataba wa amani Addis Ababa haufanyi kazi!

Kwa mujibu wa Maaskofu wa Sudan Kusini wanasema,Llicha ya makubaliano yaliyotiwa sahini ya amani,hali halisi ni vurugu na ghasia zinaendelea,kwa maana hiyo wanatoa wito kwa sehemu zote mbili za kisiasa,jumuiya ya kimataifa ili kuingilia kati kwa ajili ya wema wa jamii nchini humo

Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Licha ya makubaliano yaliyotiwa sahini ya  amani, hali halisi ni vurugu na ghasia zinaendelea. Ndiyo wasiwasi mkuu wa maaskofu wa Sudan Kusini katika ujumbe wao baada ya Mkutano wao wa mwaka uliofanyika mjini Juba kuanzia 26-28 Februari 2019.  Katika Hati yao ya pamoja maaskofu wanaelezea kuwa ilikuwa ni hatua ya kwenda mbele kuhusiana na makubaliano ya amani yaliyotiwa sahihi tarehe 12 Septemba 2018  na Rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar, huko Addis Ababa ili kuweza kufikia mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu mwaka 2013.

Ujumbe wa maaskofu wanasema pamoja na kuweka saini hiyo hali halisi kwa hakika katika kambi hiyo , kwamba hakuna lolote linalofanyika la kukabiliana na sababu za kina za migogoro nchini Sudan. Kwa namna ya pekee mtindo wa kushirikishana madaraka katika kuwatia moyo sehemu zote mbili ili kuweza kufanya kazi pamoja kwa ajili ustawi wa  wa nchi.

Waraka wao  pia unakumbusha baadhi ya makubaliano yaliyotiwa saini hawazingatii na wala kuhesimu  makubaliano hayo. Na zaidi hali halisi ya makubaliano hayo yamechelewa na utafikiti hali  halisi kama migogoro ni kama imefunguliwa kwa upya na sehemu zote mbili zimejihusisha katika mapambano au katika kuandaa silaha. Thamani ya maisha na hadhi ya kibinadamu imesahuliwa wa kwa sababu ya kuendelea na ukiukwaji wa haki za binadamu: katikati ya mauaji, nyanyaso kijinsia, wizi, kuvamia ardhi na mali za raia. Wakati wakizungumza amani, maneno hayaendani na matendo.

Kutokana na hili, ndipo maasikofu wanatoa wito kwa sehemu mbili za viongozi wa kisiasa, na kijeshi, kwa wale walio tia sahini ya makubaliano (R-ARCSS) na kwa sehemu nyingine ambao hawakutia saini ya makubaliano wa IGAD, jumuiya ya kimataifa na watu wote wenye mapenzi mema kushirikiana kwa pamoja ili  kutafuta makubaliano ya kweli ya amani ambayo yanakweza zaidi ya upeo wa sasa.

04 March 2019, 15:20